Mkuu Mawia, nakukubali kwa jinsi unavyojitahidi kujijengea matumaini mithili ya mfa maji.
Unajua ukweli kwamba vyama vya upinzani Tanzania, hadi sasa, vinaongozwa na viongozi wanasiasa wachanga, wachumia tumbo na wanaharakati. Badala ya kujijenga kwa jamii ya wapiga kura, wanafanya hivyo kwa jamii yenye uwezo wa kutumia TEHAMA. Kutwa watajinasibu mitandao ya kijamii au kutumia vyombo vya habari. Wanayongoea huko zaidi ni ya kinadharia, kama siasa za zamani za kutoa ahadi hewa, au kutafuta huruma ya wasomaji.
Hivyo basi kulinganisha Malawi na Tanzania ni sawa na kulinganisha chui na paka. Serikali ya CCM imegusa kila sehemu ya maendeleo ya mpiga kura kwa vitendo, jambo ambalo viongozi wengi wa Bara la Afrika na hata nchi zote zinazoendelea, wameshindwa.
Naamini hapo ulipo, japo unashutumu kwa minajiri ya kujifariji, Tanzania ya leo siyo ya jana.
• Wanao, kama unao, wanasoma bure;
• Iwapo una gari lako mwenyewe barabara zimeboreshwa;
• Kama uko Chuo, mkopo unapata kwa wakati;
• Wewe ni mjasiriamali, basu husumbuliwi hovyo kana zamani; nk