Hali ya kisiasa kwa sasa kwa mtazamo wako ikoje?
Hali ya Siasa kwa sasa naifananisha na tanuri la moto uliochochewa mara saba. Tanzania yetu inapita katika kipindi kigumu sana ambacho hatujawahi kukiona tangu kuanzishwa kwa taifa letu.
Ule Uhuru wetu,
Ule Umoja wetu,
Ule Mshikamano wetu,
Ule Udugu wetu,
Ule Muungano wetu na;
Ile Amani yetu ambayo tumejisifia tunayo kwa zaidi ya miaka Hamsini (50) sasa inapimwa.
Na lazima ikumbukwe kwamba hizo tunu zetu tajwa hapo juu haziwezi kupimwa wakati wa furaha bali kipindi kama hiki ndiyo kitathibitishia dunia kwamba sisi ni watu wa namna gani.
Kama tulijenga nyumba yetu juu ya Mchanga au Juu ya mwamba...(Gharika hii ndiyo ndiyo inatupima)
Tukiamua kugawana fito na kusema liwalo na liwe kisa tu kumchukia Raisi Magufuli ambaye yeye siyo mmiliki wa hii nchi bali mpitaji tu ni lazima jahazi hili litazama na tutakuwa hatuna tofauti Paka ambaye ananyea Unga wakati ana njaa.
Pia tukisema tukae turidhike na kuwategemea wanasiasa hasahasa vyama kwamba ndiyo vitatuletea maendeleo basi tutakuwa tumepotea sana kwa kiasi kikubwa. Ni lazima ifike wakati watanzania tuwafundishe hawa wanasiasa kwamba nani ndiye mwenye makali na nani mwenye mpini....Ni lazima tuwafunge lijamu wanasiasa ili hata wakiangalia kwenye vioo waone taswira zetu sisi wananchi wa kawaida.
Ukweli mchungu ni kwamba maendeleo hayataletwa na rundo la Makaratasi yanaitwa katiba,...Maana katika ya Kwanza kabisa ni wananchi wenyewe katika nadharia ya Social Contract kwamba "From today onwards the government and its instrument pledges fidelity to WE the PEOPLE OF Tanganyika and Zanzibar and will only remain valid and legitimate as long as it remains royal to the cause it was established for..
As from there we can seal this pact in a written Evidence called The Constitution..(Katiba ya kwanza kabisa ni sisi wananchi na jinsi tutakavyoamua kufanya mfumo wetu wa maisha uwe)
NB: Marekani ni moja ya taifa kubwa sana hapa duniani kwasababu lilipitia vipindi vigumu sana na mwishowe walitoka katika hayo majanga wamoja kuliko hata walivyokuwepo kipindi cha Uhuru.
Nchi ilimeguka vipande viwili, na dunia ikashuhudia ndugu wawili wakiuana. Falme za Ulaya zilitumia mwanya wa Demokrasia ya Marekani kuleta machafuko. Lakini wananchi wa Marekani walijua kwamba tatizo siyo vita bali ni jinsi watavyo-react dhidi ya hiyo vita wao kama Wamarekani.
Kuna watu walitaka kugawana fito za nchi kisa Rais Abraham Lincoln lakini wakaja kujua kwamba Lincoln ni mpitaji tu na Marekani ni kuwa kuliko kila mtu.
Hivyo na sisi Watanzania,
Tukumbuke kwamba wakina CCM,CHADEMA, ACT, Lowassa, Magufuli, Mbowe, Lissu, Zitto na wengineo ni mivuke ambayo inapita kwa muda tu lakini hutoweka. Hawa wanasiasa wana umuhimu wao sana lakini ni lazima tujue kwamba Tanzania ni kubwa sanaa kuliko hawa wapitaji....
Ni hayo tu kwa kifupi mkuu......