Malcom Lumumba Live: Tusemezane...

Malcom Lumumba Live: Tusemezane...

ahsante mkuu kwa majibu yako mazuri mkuu, najifunza vingi.pole kwa maswali mengi..

Je NK anapata wap tecnolojia ya kutengeneza siraha,mbona yeye silaha zake anatengeneza na anauza kwa bei rahisi??

kwa mtazamo wako je kuna dalili marekani ikakubali NK kuwa na nuclear weapon??, ikitokea imekubali vipi kuhusu SK au Japan watakubali kuachia ipite hivi hivi??

Usijali mkuu.
Haya mambo nilishawahi kuyazungumzia huko nyuma na mkuu izzo
Unaweza kuyapitia hapa kama ukipenda kusoma zaidi:
1.North Korea wanapata wapi fedha za kuendesha project za silaha na kijeshi wakati wanavikwazo vya kiuchumi?
2.Kila mtu na mbabe wake. Je, Korea Kaskazini ni mbabe wa Marekani
 
Mkuu Malcom kuna sehem unasema wairani ni watu wengine kabsa na si wakuwalinganisha na walibya wala wairaq. Tafadhali unaweza kutupa CV ya warain inayowatofautisha na waarabu wengine?
 
Mkuu Malcom kuna sehem unasema wairani ni watu wengine kabsa na si wakuwalinganisha na walibya wala wairaq. Tafadhali unaweza kutupa CV ya warain inayowatofautisha na waarabu wengine?

Mkuu,
Kwanza kabisa,
Wairani siyo Waarabu.
Wale ni Indo-Europeans, kundi la wahamaji waliotokea Ulaya na kuchangamana kidogo na Indo-Pakistan.
Hata lugha yao ni kufursi (Farsi) ambayo ni wanahistoria wanasema ni Indo-European tofauti kabisa na Kiarabu.

Pili,
Iran ni taifa lenye nguvu sana Kijeshi tofauti na mataifa mengi ya Mashariki ya kati.
Nguvu ya kijeshi ya Iran pale mashariki ya kati inalinganishwa na hasimu wake mkubwa Israel.
Taifa lile limewekeza sana kwenye elimu ya kujitegemea hadi kufikia hatua kwamba hawategemei sana silaha kutoka nje.

Baada ya kuanguka kwa Urusi mwaka 1991,
Mipango mingi sana ya Kijeshi ilikwamba kwasababu walikuwa hawana mapato ya kutosha.
Kilichofanyika ni kwamba Warusi walianza kuuza silaha nje ya nchi yao kwa wingi ili kufanya viwanda vyao visife kabisa.
Waliuza silaha nyingi sana kwa Uchina na Iran hivyo kupelekea hizi nchi kuanza kujijenga sana kijeshi miaka ya 90

NB 1: Waziri mkuu wa Urusi wakati huo Evgen Primakov alienda kuunza urafiki na Iran ambaye alikuwa ni adui yao mkubwa. Urusi alipendekeza kwamba kwasababu hawana pesa basi ni lazima wafanye Joint Military Projects na nchi kama Uchina, India na Iran. Hawa waajemi walikubali kununua silaha nzito na teknolojia kutoka Urusi hadi kupelekea The Pentagon kusema kwamba biashara anayoifanya Boris Yeltsin na waajemi imekuwa kubwa sana kiasi cha kuhatarisha usalama wa mashariki ya kati. Rais wa Iran Akhbar Heshimi Rasfanjani alinukuliwa akisema kwamba anafurahia sana huu uhusiano mpya wa kijeshi ambao upo baina ya Iran na Urusi, akiwapa hamasa waajemi wauendeleze kwa ukaribu.

Hadi kufika miaka ya 2000,
Iran walishakuwa wanatengeneza silaha zao kama ndege vita, vifaru, manowari, nyambizi, radar, makombora na mzinga.
Walisomesha sana vijana wao kwenye nchi kama Korea Kaskazini, Uchina na Urusi hivyo wakajijenga sana kijeshi. Ukiangalia sasa, mataifa mengi ya kwenye Ghuba ya Uajemi (Persian Gulf) yanategemea sana Silaha kutoka Marekani, Uingereza, Ujerumani na Ufaransa. Hata Iran kabla ya mapinduzi ya kiislamu ya mwaka 1979 alikuwa ananunua sana silaha kutoka nchi hizo.

NB 2: Ukisoma The Primakov Imperial Line au The Primakov Doctrine utajua kabisa Warusi walijipanga sana kuzitumia Iran na Iraq kuzuia nguvu ya Marekani pale Mashariki ya kati baada ya kuanguka kwa Umoja wa kisovieti. Walijipanga kumpa Saddam Hussein mikopo mikubwa ya Silaha lakini baadae Saddam Hussein akapigwa na Wamarekani.
Warusi baada ya kuona Saddam Kaanguka basi wakaamua kuhamia kabisa nchini Iran na kuwa na mahusiano nao ya Ukaribu zaidi hadi kuzaa matunda ambayo dunia imeyashuhudia kule nchini Syria.

Tatu,
Iran ina uwezo mkubwa wa kuendelea kwasababu ya mfumo Imara wa Kisiasa.
Iran ni nchi ya Kiislamu lakini kuna baadhi ya vitu ambavyo wameviingiza vinawafanya wawe tofauti kabisa na mataifa mengi ya kiislamu yaliyopo kwenye Ghuba ya Uajemi. Pale juu kabisa ya Utawala wa nchi kuna kiongozi wa Dini "The Ayyatullah" ambaye wao wanamuita The Supreme Leader.

Tofauti kubwa ni kwamba,
Nchini Iran Serikali yake ni ya Kiislamu lakini inawajibishwa kisiasa na waislamu.
Mfano mzuri kabisa kuhusu nchi ya Iran:

1. Kuna raisi anayeteuliwa na wananchi. (The President)
Tangia mwaka 1980 mpaka leo Iran imekuwa na maraisi 7 tofauti na kwa kipindi tofauti.
Wanafanya Uchaguzi na wanashindwa tena hawathubutu kabisa kuchakachua kitu, kama ambavyo Ahmedinejad alishindwa mwaka 2013 dhidi ya Hassan Rouhani. (Waarabu hawana uwezo wa kufanya hivi)

2. Kuna Bunge la wananchi. (The Majlis or Legistature)

3. Kuna Baraza la Wataalamu (Assembly of Experts) - Hawa ndiyo wanamchagua au kumfukuza kiongozi mkuu wa nchi ambaye ni "Ayatollah" A.K.A The Supreme Leader.

4. Kuna Baraza la Wasimamizi (The Guardian Council)
Hawa ni wataalamu wa Dini na Sheria.. Hawa kazi yao ni kusimamia na kutasfiri katiba ya nchi ya Iran. Hivyo wanafanya kazi kama Mahakama maalumu ya katiba au The Constitutional Court. Raisi kabla hajateuliwa au Baraza la wataalamu halijateuliwa hawa ndiyo wanawafanyia ukaguzi mzito na wa maana.

Bunge likipitisha Miswada ambayo haina mbele wala nyuma,
Hili Baraza lina nguvu ya kuweka kura ya hapana au "VETO" na huu ndiyo ukawa mwisho wa mambo.
Huu mfumo uko kama wa Uingereza mnamo miaka ya nyuma mbapo The House of Lords (Mahakama Kuu) ilikuwa na uwezo wa kupinga miswada ya Bunge la Uingereza (The House of Commons) kwa kutoa sababu za msingi kwanini wanafanya hivyo. Siku hizi huu mfumo Uingereza haupo

NB 3: Iran ina hulka ya udikteta lakini kwenye masuala ya Uongozi hawaangalii undugu kabisa.
Kila kiongozi wa nchi anateuliwa kwa vigezo maalumu kabisa ambavyo vinathibitishwa mbele ya mabaraza maalumu.
Ni nchi ya Kiislamu lakini imejitahidi sana kuachana na mifumo ya Usultani ambayo ipo sana kwenye nchi nyingi za Kiarabu: Wameweza kuweka UWIANO baina ya Elimu ya Akhera na Elimu Dunia, baada ya kuona umuhimu wa zote hapa duniani.

Huu mfumo unafanya kitu kinachoitwa The Di-Mystification of Power,
Watu wanakuwa hawaishutumu Serikali yote kwa ujumla kwa hujuma za kisiri (Conspiracies) kwasababu mambo yanakuwa nje kwa kila mtu. Hii inaleta imani kwamba nchi hii ni yetu sote na kila mtu anaweza kufika juu kama atakuwa na bidii. Hata kama bado hawajafika kule kunakotakiwa na wana safaru ndefu sana lakini mpaka hapa wamejitahidi sana kujenga Serikali ya watu. Nchi ina katiba ya Wananchi na katiba hiyo imefanyiwa marekebisho mara kadhaa naamini kama walifanya marekebisho hadi kufika hapa walipo kukidhi haja za wananchi basi hawatashindwa kufanya hivyo huko mbeleni.

Nchi kama Iraq, Libya, Qatar na Saudi Arabia,
Wanajihadi sana lakini uongozi wa kule ulikuwa umekaa Irrational Sana kama ambavyo Prof. Max Weber anasema kwenye Bureaucratic Theory yake. Kwamba serikali imara ni ile inayoundwa na taasisi na siyo kutegemea mtu tu bila sababu za msingi. Sasa Libya walifika pazuri lakini uongozi ulikuwa umewekwa kwenye Serikali ya Muhamar Ghaddafi na familia yake au nchi Iraq watoto wa Saddam kama wakina Udday walikuwa wanafanya wanavyotaka na pesa za nchi bila kuwajibishwa. Hata kama walikuwa ni watu wema Propaganda zinapokuja ni rahisi sana kuwazoa watu wenye akili ndogo.
Serikali inabidi zijiepushe sana na utawala wa kindugu na kidini bila sababu maana mwisho wa siku vitu Irrational vinaweza kufanyika lakini kwasababu ni mtu wa familia yangu au dini yangu basi yanaishia juu juu tu.

HITIMISHO:
Hii mifumo ya kuweka watu wako mbele na kuwekeza sana kwenye Elimu ndiyo kumewafanya Waajemi wawaogopeshe Wayahudi, Waarabu na Wazungu kila uchwao. Wanafanya maajabu ya kiteknolojia kila siku, wamebebwa na Mataifa ya Urusi, Korea Kaskazini na Uchina lakini wao nao wanabebeka sana. Leo hii Saudi Arabia akifa Mfalme Salmani au yule kijana wake Saudi Bin Abdulaziz al Saudi nchi inaweza kuyumba kwasababu kuna ndugu wengi wanataka kiti cha Ufalme hicvyo kupelekea vurugu zisizo na msingi tu au hata vifo vya watu. (Au vurugu zinaweza zisitokee kabisa, kwasababu huu ni mtazamo wangu nikifanya ulinganishi na nchi nyingi zenye mifumo hiyo)

Huu ni mtazamo wangu tu mkuu.
Mengi niliyosema hapo yanaweza kuwa sahihi au siyo sahihi.
Nakushauri ufanya utafiti wako mwenyewe ili ujenge mwono thabiti zaidi ya huu wangu.
 
Ombi.

Naomba links za nyuzi zako zoooote Ulizoanzisha majukwaa ya Jf Intell,, zInternational etc nikaongeze maarifa..
Mboma nilikuita kwenye zote mkuu ???
Pia mada nyingi mimi huwa nachia tofauti na kuanzisha.....
 
Kwa mfumo wa uongozi wa nchi yetu... Embu weight kwa muda miaka 10 ijayo tutakuwa Wap kama nchi!! Ki usalama,uchumi,na kijamii!.

Je ni kweli sisi nchi hatuchagui raisi, ila tunampitisha baada ya system kufanya vetting???
Malcom Lumumba
 
Kwa mfumo wa uongozi wa nchi yetu... Embu weight kwa muda miaka 10 ijayo tutakuwa Wap kama nchi!! Ki usalama,uchumi,na kijamii!.

Je ni kweli sisi nchi hatuchagui raisi, ila tunampitisha baada ya system kufanya vetting???
Malcom Lumumba

Mkuu,
Pitia uzi namba #25 nimejaribu kuweka mwangaza kidogo!
 
Mkuu kama unaweza naomba softcopy ya vitabu unavyosoma nami niwe kama ww

Contrary to the main belief, reading books doesn't make you wise.
But reading books is a trait of many wise men in the world...
The challenging part of knowledge is not about gaining it, but applying it...!
I've seen people read books, but still end up being damn..they only use it for the sake of argumentation.
And, one can tremendously apply the knowledge in his field of expertise (A place where his talents lie)
Apart from reading books you need discipline and years of practice to nourish your talents and gifts.

My advice,
Don't try to be like Malcom just be yourself and deploy your gifts and talents (This is imperative to any human achievement)
I could give you a container of books and after 100 years still find you the same man. So do what you are just good at doing and don't fake trying to be someone else (Aristotle became distinguished because he did not want to be like his teacher, PLATO).....

NB: Kubwa kuliko haya yote,
Hekima na Maarifa vinatoka kwa MUNGU.
Take time alone with God and in the end you will be very wise: This is the biggest secret many people Ignore!!!
 
Contrary to the main belief, reading books doesn't make you wise.
But reading books is a trait of many wise men in the world...
The challenging part of knowledge is not about gaining it, but applying it...!
I've seen people read books, but still end up being damn..they only use it for the sake of argumentation.
And, one can tremendously apply the knowledge in his field of expertise (A place where his talents lie)
Apart from reading books you need discipline and years of practice to nourish your talents and gifts.

My advice,
Don't try to be like Malcom just be yourself and deploy your gifts and talents (This is imperative to any human achievement)
I could give you a container of books and after 100 years still find you the same man. So do what you are just good at doing and don't fake trying to be someone else (Aristotle became distinguished because he did not want to be like his teacher, PLATO).....

NB: Kubwa kuliko haya yote,
Hekima na Maarifa vinatoka kwa MUNGU.
Take time alone with God and in the end you will be very wise: This is the biggest secret many people Ignore!!!
Daaah it so deep indeed, mkuu kama hutajali naomba nije pm kwako tuzungumze..
Please I beg you
 
Back
Top Bottom