Awali kasema ccm ni chama cha masikini. ni kweli nchi imeubariki umasikini? tunajivunia kuwa nao? Pili kasema kuwa Kikwete hana mpinzani 2010. na wanaojaribu wasahau. inamaanisha ile demokrasia ya miaka mitano mitano kwishnei?
Big Nooo! Mkuu FMEs
Malecela ametufundisha kuwa WANAFIKI ili mradi ya kwetu binafsi yametunyookea.Je, ina maana kwenye milioni 40 ya waTZ au milioni 4 ya wanaCCM hakuna anayeweza kuwa mtendaji bora kuliko alivyotenda Kikwete?
- Kama Kikwete alipoingia madarakani nchi ilikuwa haina umeme na sasa hivi hali ni mbaya zaidi je hayo ni mafanikio yanayohitaji kuzawadiwa?
- Kama Kikwete alipewa ripoti ya Bunge juu ya rushwa ya Richmond lakini hadi leo hajashughulikia madondoo yake, je huu ni utendaji unaohitaji kuzawadiwa mvua 5 nyingine??
- Kama hali ya elimu imezidi kuwa mbaya, hospitali hazifai mpaka upelekwe India, SA, UK n.k., vyuo vikuu ndio usiseme, je haya yanahitaji zawadi?
- Kama imeshindikana kuwashughulikia wala rushwa wa, EPA, BOT, RadarGate n.k., ambao habari zao zimezagaa kila kona ukiachia hao wachache anaotumia kututengenezea viini macho, je hii sio failure??
- Kama mpaka leo nikitaka kwenda Mwanza ni lazima nipitie Kenya, je haya ni maendeleo??
- Kama inakuwa nafuu kwa mfanyabiashara wa Tanzania kuingizia mizigo yake bandari za Durban au Mombasa badala ya bandari ya Dar es salaam, je huku ni kwenda mbele au ndio twafa hivyo??
Ingawa namheshimu sana Mzee Malecela, lakini emetudhihirishia wazi kuwa kwake yeye, maslahi binafsi ni bora mara 100% kuliko maslahi ya nchi.
[/QUOTE]Ingawa namheshimu sana Mzee Malecela, lakini emetudhihirishia wazi kuwa kwake yeye, maslahi binafsi ni bora mara 100% kuliko maslahi ya nchi. [/SIZE][/B][/COLOR]
Nashauri tuyataje maslahi binafsi ya Malecela katika safu hii, na mimi naanza:
-JK alimteua kuwa mjumbe wa kudumu katika CC bila ridhaa ya chama ili kumpangusa machozi ya kukosa urais. Kawaida Makamu angekuwa mjumbe NEC ingetosha.
-JK alikubali ushauri wa Melecela kumgeuka Lowassa na kumtapeli. Awali walikubaliana aandike barua ya kujiuzuru lakini sisikubaliwe. Kwa ushauri wa Malecela, JK akaikubali.
-Wabaya wa Malecela katika mtandao wanashughulikiwa na JK, kwa hiyo mzee huyo anachekelea.
-JK kufuata ushauri wa Malecela unamharibia mambo ndani ya chama. Yakiharibika, Malecela anacheka pia na kutumabia yeye ndiye angefaa na siyo JK. Wengine ongezea.
Hana chochote huyu cha kutufundisha Watanzania. Mawazo yake yamepitwa na wakati.
Inakuwaje mtu anayekemea press conferences awe anatufundisha ukweli na uwazi?
- Mkuu amelazimisha akiwa kama nani? mbona mnapenda kukuza maneno hivi, yeye ameongelea chama chake cha CCM na wewe ongelea chama chako cha siasa,
- hii fear inatoka wapi kwa sababu ya maneno ya mzee mmoja tu amabye maepitwa na wakakti, hana akili, ni mzee na balh! baln! sasa vilio vyote hivi ni vya nini kwa sababu ya mzee asiye na lolote kwa taifa?
FMES!
Mkuu FMES, kauli ya Mzee Malecela sio ya kupuuzia hata kidogo. Mzee huyu ni mwanasiasa mzoefu katika nchi hii, amewahi kushika madaraka makubwa sana katika Taifa na ana influence kubwa vile vile (ndani na nje ya CCM). Siwezi kuthubutu kusema wala kufikiria licha ya kukubali kuamini kuwa hana akili, amepitwa na wakati wala ni Mzee wa Blah blah kama ulivyosema. Huyu ni mtu wa maana na ataendelea kuwa hivyo mpaka siku yake ya mwisho.
Kauli aliyoitoa inawataka CCM wote waache kufikiria kutafuta nafasi za kugombea uRais 2010, kwakuwa utamaduni wa chama hauwaruhusu na kwamba JK anatakiwa kuwa ndie mgombea wa CCM katika uchaguzi mkuu ujao. Sina ubaya na matokeo hayo, ila sidhani kuwa ni vyema kwake kuwakaisha tamaa wana CCM kupata nafasi hiyo ya kikatiba kuomba kuchaguliwa.
- Sasa mkuu haya ni mawazo yako, kwa nini unataka yawe na yake pia? yaani kutokuwa na mawazo kama yako kunamfanya Mzee kuwa mnafiki? Haya ni mawazo yako tu mimi nina yangu na kila mtu ana yake, na sio lazima kwa kuwa tofauti na mawazo yako basi tunakwua wanafiki ni hoja finyu sana mkuu, kiasi kwamba inaondoa hata ladha ya baadhi ya hoja nzito ulizozitoa hapo juu.
- Acha name calling ili ueleweke unasema nini bro, hizi za yeye kuhomngwa na rais sijui unazitoa wapi? Kwa nini usiweke ushahidi wa yeye Mzee kuhongwa na rais?
FMES!
- Labda ungeongelea utamaduni wa upinzani tu mkuu, maana ni kwa maneno yako kwamba utamaduni wa CCM haukuhusu, sasa why waste time na utamaduni usiokuhusu tena wa CCM na wala sio taifa? Bwa! ha! ha! ah!
- Utamaduni wa CCM haukuhusu basi ongelea unaokuhusu, yaani utamaduni wa Upinzani, au?
FMES!
- Mkuu it does not matter what CCM is or not, kinachojali vipi utamaduni wa chama chako cha siasa ukoje?
- CCM haimzuii yoyote kugombea urais, kama ambavyo Obama atapita bila tatizo ndani ya Democratic Party, next time je nao huko US hawana demokrasia?
FMES!
- Sasa kwa nini toka juzi kuhangaika na kiongozi aliyepitwa na wakati, kwa nini thread kila kona kwa ajili ya kiongozi asiyekuwa na anyhting to offer? Why hata kupoteza muda kuja ku-comment on his comments?
- Wakuu vipi mbona maneno yenu hayafanani na matendo, kiongozi aliyepitwa na wakati siwezi kuwa na muda hata wa ku-comment on his comment only yule tu mwenye umuhimu na siasa za taifa langu ndio nita-comment.
Inaonekana aliyosema ndio yatakayokuwa, saafi sana kutoka kwa kiongozi aliyepitwa na wakati, hebu tutajieni ambao hawajapitwa na wenye mapya, au Zitto? Bwa! ha! ha! ah i mean this is fun!
Wazee wa sauti ya umeme FMEs!