Hivi Mzee Malecela amewafanyia nini wananchi wa Mtera kwa kipindi chote alichokuwa Mbunge. Kieleimu, kiafya, miundombinu na huduma nyingine za jamii kama maji, umeme nk.
Nini hasa alichowafanyia cha kujivunia kuwa kiongozi wao mvua zote hizo?
Mkuu ubunge mara nyingi hutumika tu kama njia ya kufikia malengo yao, na ndio maana pia kuna hiyo sheria ya kuwa mbunge kwanza kabla hujawa waziri kwani sijui utawatumikia vipi wananchi wako waliokuchaguwa bila ku compromise interests zao. Hilo lilikuwa sawa tu wakati wa chama kimoja kwasababu wanakubaliana kwenye mambo mengi kutokana na kuwa na itikadi moja....Utashangaa mtu ni mbunge say wa Kigoma lakini yeye na Zimbabwe,ama wengi wao wanadili zaidi na siasa za kitaifa kwasababu malengo yao ni uwaziri nk.
Ukweli ni kwamba mpaka hapo wabunge watakapokuwa wanawakilisha maslahi ya wananchi waliowachagua,then tunaweza kupata maendeleo,naona kuna udhaifu mkubwa sana wa mfumo wetu wa utawala kwani mbunge anazungumzia mambo ya jimbo wakati wa kuomba kura na akishachaguliwa issue ni za tofauti kabisaa...Kwasababu umasikini ni mkubwa basi wananchi wanadanganyika kiurahisi sana,na hivyo kamradi kamoja tu will keep them on the quite.
Sasa najiuliza sana mara nyingi,ni wakati gani mbunge anawatumikia wananchi waliomchagua(wa jimboni kwake) na ni wakati gani anaitumikia serikali ama Taifa?
Siwezi kuelewa hapo maana mishahara wanalipwa mikubwa sana lakini wanachofanya kwa wanachi sikioni,tena na huu ubinafsishaji ndio basi kabisa,ni halali kuuza hata mali zao.
Dk Malecela alipewa majukumu mengi sana tu kama uwaziri,ubalozi nk, na kuna kipindi ilikuwa si lazima uwe mbunge kuwa iili kuwa waziri,je hatuwezi kuurudisha utaratibu huo na wakati huo huo tukajitahidi kusiwe na loophole za kujaza mawaziri kwa maslahi binafsi? Maana kama tusipoanzia huko kwenye majimbo yetu,tutaendelea kuwa masikini tu kwa kupenda sifa,angalia ni nchi ngapi tulizozisaidia hata kwenye kupata uhuru na sasa wako mbele zaidi yetu? Je tunaweza ku strike balance kati ya uzalendo na kuhakikisha tunapata maendeleo? Je maendeleo yanapingana na uhuru? kama sivyo kwanini hatuna maendeleo licha ya "Uhuru" tulionao? Wananchi wanamchagua mbunge aende kuwatumikia,mbunge anasema yeye anatumikia maslahi ya Taifa,at the same time haki za wananchi huko bungeni si maslahi ya Taifa, kwani hata huko bungeni ni lazima kuzipigania haki za wananchi na unaweza kufukuzwa bungeni ukujidai ngangali,sasa kama si siasa za kujitafuna wenyewe kama vichaa ni nini?
Ni wakati wa kufikiri sana kuhusu suala hili ili tuweze kuona ni kwa kivipi wabunge watawatumikia wananchi wao moja kwa moja na si kutumia nafasi hiyo kwa maslahi binafsi ambayo usipokuwa makini unaweza kudhani ni ya kitaifa kama wabunge hao wanavyodai...Kwasababu kama ni maslahi ya kitaifa,je Taifa limefika wapi na utitiri wote huu wa wabunge wenye kulipwa ghali na wengi wao kazi yao ni kulala na ufisadi?