Malecela avunja ukimya!

Malecela avunja ukimya!

Kuhani,

Mkuu wangu usisahau WATU na MAZINGIRA hata siku moja..Mzee Malecela kukuita wewe kijana haina maana kuwa wewe ni nchovu fulani ila ni mila na desturi zetu ktk kujitambulisha.. mbona mnatuita Wazee humu JF, kwa uzee gani tuliokuwa nao!..

Ewaaaa...umemaliza hili Mkandara. Ni mara ngapi humu tunaitana ma Yakhe kwa mfano? Au mjomba? Au Mazee (ambayo ndio hiyo hiyo mzee).

Nyerere alikuwa akiwaita watu "nyie Waswahili"...(affectionately) lakini sio wote aliokuwa akiwaita hivyo ni Waswahili.

Jamani, huu ubishi mwingine, huu ukosoaji mwingine usio na mbele wala nyuma ndo mambo ambayo husababisha watu kulumbana humu ndani. Kama mtu huna cha kukosoa ni bora kujikalia kimya tu.
 
- Alikuwa na title ya uwaziri tu, ya ubunge alianza kuwa nayo from 1975, sasa nisaidieni kabla ya 1975 alikuwa what pamoja na kwamba alikuwa akiingia bungeni kama waziri, lakini hapewi haki za ubunge mpaka 1975 aliposhinda ubunge?

William.

Mwalimu hakuruhusu mishahara miwili hivyo ukiwa mbunge then ukachaguliwa kuwa Waziri utachukua marupurupu na mshahara ulio juu, nao ni wa Uwaziri, maneno mengine ni upotoshaji wa habari. Kuna watu Kama Asha Rose Migiro aliteuliwa kuwa Mbunge na kuwa waziri wa Akina Mama, watoto etc etc, in that context akiwa refered to Waziri wa akina Mama etc etc does not mean hakuwa Mbunge. Haya Mabadiliko ya kuwa Mbunge wa kuteuliwa then kupewa uwaziri ni maboresho ya vitu vilivyo kuwepo hapo Mwanzo kupitia sijui nafasi za Vijana, wanawake, Wasiojiweza na Raisi ana nafasi zake 10, infact ni njia ya Raisi kuweza kuwaweka watu wake kwenye Serikali either wanafaa technically au kisiasa. Sasa Kama Mwalimu Sheria ilikuwa ina mruhusu kuteuwa Waziri ambaye hakuwa Mbunge wa kuchaguliwa, then by Default huyu Mtu ni Mbunge. Eg ya Maboresho ya Sasa ni ya AG kuingia Bungeni kama Mbunge Ex-Officio mwanzohilo jambo halikuwepo.
 
Ni vile sijui identity za watu lakini brother W.J anasound sana kama FMES....Kuja ukate issue mkuu FMES,Taifa liko njia panda hili.
 
Hivi Mzee Malecela amewafanyia nini wananchi wa Mtera kwa kipindi chote alichokuwa Mbunge. Kieleimu, kiafya, miundombinu na huduma nyingine za jamii kama maji, umeme nk.

Nini hasa alichowafanyia cha kujivunia kuwa mbunge wao mvua zote hizo?
 
Hebu jadili hoja usijadili mtoa hoja. Tabia hiyo ndiyo ya OVYO kabisa inayopotosha mada na mara nyingi inatumiwa na watu kama Rostam ambaye baada ya kushindwa katika Dowans sasa akakumbuka kuhusu Power Pool ya Mwakyembe.

Nilishawahi kusema, tusipindishe hoja kwa sababu tu zimetolewa na fulani. Itafika mahali hatutakuwa na hoja kabisaaaa!!!! Maana utataka kujua 'halisi' ni nani, kama ni Rostam basi hana haki ya kusema kuna wezi pale Ubungo Tanesco. Leo hii mimi naamini hata Rostam, Chenge, Jeetu Patel, pamoja na uchafu wao, wana haki ya kuzungumzia uchafu wa wengine lakini wajue hiyo haiwasafishi kwa kuzingatia kwamba maji taka hayaogwi na kuchafua wengine hakuwasafishi na mwizi akikamatwa hata akitaja wenzake haachiwi na pia wasitunge.

Jambo la msingi kwenye mada hii, ni tusiibue hoja za kutungwa alizorushiwa Mzee Malecela na wenzake kama Dk. Salim na wengineo. Najua baada ya hapa watu wataanza kumshambulia ili kumnyamazisha, hawatafanikiwa ng'o!

Kwenye demokrasia ya kweli ukishachafuka huwezi tena kuwa na maana, maadili kwa jamii yako. Huwezi kusema mwizi au fisadi ataweza kuongelea kitu chochote zaidi ya kutetea mambo yake au yao.

sasa huyo Malecela umemsikia na huo upuuzi wake. I dare to say he is nothing to me.
 
Hivi Mzee Malecela amewafanyia nini wananchi wa Mtera kwa kipindi chote alichokuwa Mbunge. Kieleimu, kiafya, miundombinu na huduma nyingine za jamii kama maji, umeme nk.

Nini hasa alichowafanyia cha kujivunia kuwa kiongozi wao mvua zote hizo?

Mkuu ubunge mara nyingi hutumika tu kama njia ya kufikia malengo yao, na ndio maana pia kuna hiyo sheria ya kuwa mbunge kwanza kabla hujawa waziri kwani sijui utawatumikia vipi wananchi wako waliokuchaguwa bila ku compromise interests zao. Hilo lilikuwa sawa tu wakati wa chama kimoja kwasababu wanakubaliana kwenye mambo mengi kutokana na kuwa na itikadi moja....Utashangaa mtu ni mbunge say wa Kigoma lakini yeye na Zimbabwe,ama wengi wao wanadili zaidi na siasa za kitaifa kwasababu malengo yao ni uwaziri nk.
Ukweli ni kwamba mpaka hapo wabunge watakapokuwa wanawakilisha maslahi ya wananchi waliowachagua,then tunaweza kupata maendeleo,naona kuna udhaifu mkubwa sana wa mfumo wetu wa utawala kwani mbunge anazungumzia mambo ya jimbo wakati wa kuomba kura na akishachaguliwa issue ni za tofauti kabisaa...Kwasababu umasikini ni mkubwa basi wananchi wanadanganyika kiurahisi sana,na hivyo kamradi kamoja tu will keep them on the quite.
Sasa najiuliza sana mara nyingi,ni wakati gani mbunge anawatumikia wananchi waliomchagua(wa jimboni kwake) na ni wakati gani anaitumikia serikali ama Taifa?
Siwezi kuelewa hapo maana mishahara wanalipwa mikubwa sana lakini wanachofanya kwa wanachi sikioni,tena na huu ubinafsishaji ndio basi kabisa,ni halali kuuza hata mali zao.

Dk Malecela alipewa majukumu mengi sana tu kama uwaziri,ubalozi nk, na kuna kipindi ilikuwa si lazima uwe mbunge kuwa iili kuwa waziri,je hatuwezi kuurudisha utaratibu huo na wakati huo huo tukajitahidi kusiwe na loophole za kujaza mawaziri kwa maslahi binafsi? Maana kama tusipoanzia huko kwenye majimbo yetu,tutaendelea kuwa masikini tu kwa kupenda sifa,angalia ni nchi ngapi tulizozisaidia hata kwenye kupata uhuru na sasa wako mbele zaidi yetu? Je tunaweza ku strike balance kati ya uzalendo na kuhakikisha tunapata maendeleo? Je maendeleo yanapingana na uhuru? kama sivyo kwanini hatuna maendeleo licha ya "Uhuru" tulionao? Wananchi wanamchagua mbunge aende kuwatumikia,mbunge anasema yeye anatumikia maslahi ya Taifa,at the same time haki za wananchi huko bungeni si maslahi ya Taifa, kwani hata huko bungeni ni lazima kuzipigania haki za wananchi na unaweza kufukuzwa bungeni ukujidai ngangali,sasa kama si siasa za kujitafuna wenyewe kama vichaa ni nini?

Ni wakati wa kufikiri sana kuhusu suala hili ili tuweze kuona ni kwa kivipi wabunge watawatumikia wananchi wao moja kwa moja na si kutumia nafasi hiyo kwa maslahi binafsi ambayo usipokuwa makini unaweza kudhani ni ya kitaifa kama wabunge hao wanavyodai...Kwasababu kama ni maslahi ya kitaifa,je Taifa limefika wapi na utitiri wote huu wa wabunge wenye kulipwa ghali na wengi wao kazi yao ni kulala na ufisadi?
 
Last edited:
Honestly speaking kwa hayo aliyoyasema ni bora angejinyamazia tu kwa kuwa at the end of the day press conference yake haikukisaidia chama chake wala Rais and now wananchi tunajiuliza who's next to come out may be Msuya let's see and who's benefit from this conferences.Nobody we need action sio porojo kama kweli unaipenda nchi yako na influence uliyo nayo huna haja ya press conference nenda kampe ushauri Rais for the issue that really matters to us. William help us to path this please.


SAHIBA.
 
Mwalimu hakuruhusu mishahara miwili hivyo ukiwa mbunge then ukachaguliwa kuwa Waziri utachukua marupurupu na mshahara ulio juu, nao ni wa Uwaziri, maneno mengine ni upotoshaji wa habari. Kuna watu Kama Asha Rose Migiro aliteuliwa kuwa Mbunge na kuwa waziri wa Akina Mama, watoto etc etc, in that context akiwa refered to Waziri wa akina Mama etc etc does not mean hakuwa Mbunge. Haya Mabadiliko ya kuwa Mbunge wa kuteuliwa then kupewa uwaziri ni maboresho ya vitu vilivyo kuwepo hapo Mwanzo kupitia sijui nafasi za Vijana, wanawake, Wasiojiweza na Raisi ana nafasi zake 10, infact ni njia ya Raisi kuweza kuwaweka watu wake kwenye Serikali either wanafaa technically au kisiasa. Sasa Kama Mwalimu Sheria ilikuwa ina mruhusu kuteuwa Waziri ambaye hakuwa Mbunge wa kuchaguliwa, then by Default huyu Mtu ni Mbunge. Eg ya Maboresho ya Sasa ni ya AG kuingia Bungeni kama Mbunge Ex-Officio mwanzohilo jambo halikuwepo.

- Unapokuwa mbunge kuna marupu rupu ya ubunge unayopewa baada miaka mitano, ambayo hayajali kama ulikuwa au haukuwa waziri, ni lazima kwa wabunge wote wanaotambuliwa kisheria, lakini sio ma-RC ambao nao huhudhuria bunge lakini sio wabunge.

- Katika miaka mitatu ya uwaziri wake wa nje, DK. Malecela hakuruhusiwa kuhudhuria vikao vya wabunge wa TANU, wala wa Commonwealth., na wala kupewa title ya ubunge kama sasa baada ya kuchaguliwa kuwa mbunge.

Ahsante.

William.
 
- Unapokuwa mbunge kuna marupu rupu ya ubunge unayopewa baada miaka mitano, ambayo hayajali kama ulikuwa au haukuwa waziri, ni lazima kwa wabunge wote wanaotambuliwa kisheria, lakini sio ma-RC ambao nao huhudhuria bunge lakini sio wabunge.

- Katika miaka mitatu ya uwaziri wake wa nje, DK. Malecela hakuruhusiwa kuhudhuria vikao vya wabunge wa TANU, wala wa Commonwealth., na wala kupewa title ya ubunge kama sasa baada ya kuchaguliwa kuwa mbunge.

Ahsante.

William.

Je nini marupurupu ya Rc akimaliza kipindi chake iwe miaka 3, 4 au mitano au anapoacha kuchaguliwa tena? au nini marupu rupu ya waziri akitoka madarakani? Hapa inabidi uujue muongozo wa mafao ya Viongozi. Kuanzia Raisi, Waziri Mkuu, Mawaziri, Wabunge, Majaji, Ma Rc, mmpaka Ma Dc, na Makatibu wakuu. Sasa kwa kuwa kipindi ni kirefu toka jambo lilipo tokea, labda mtu akiwa na ule waraka wa SCOPO etc
 
Its high time now tuwe na limits kwa terms za ubunge........
 
Nitajaribu tena,

- Kabla ya 1990, rais alikuwa na uwezo wa kumchagua anybody kuwa waziri bila ya kuwa mbunge, ingawa mawaziri na ma-RC siku zote wamekwua wakishirki bungeni.

- Mh. Abdulaziz ni Mbunge wa jimbo na RC anashiriki bungeni, lakini RC wa Dar sio mbunge wa kuchaguliwa jimboni lakini anashirki bungeni kama RC huyu sio mbunge as legally. Hawezi kuhudhuria mkytano wa wabunge wa CCM bungeni.

- I hope imesaidia, naona niende sasa kabla sija-overstay the wellcome.


William.

Mkuu W. J. Malecela, kwa kweli sikubaliani na wewe hata kidogo kuhusu nafasi ya Uwaziri bila kuwa Mbunge. Haijawahi kutokea kwenye Katiba yetu kuwa Waziri aliwahi kuteuliwa bila kuwa Mbunge hata mara moja.

Kilichokuwa kikitokea ni kwamba, kwa miaka mingi (enzi ya Mwalimu J. K. Nyerere), Rais alikuwa na uwezo wa kuteua Wabunge kwa idadi fulani (zaidi ya ilivyo sasa) ili kupata idadi ya kutosha kueua Baraza la Mawaziri aliowataka. Baada ya kipindi cha Mwalimu kuisha, sheria hiyo ilibadilishwa na Rais akaondolewa nafasi zake za uteuzi wa Wabunge hadi miaka ya 90 ndipo iliporudishwa tena.

Hakuna Waziri yeyote ambae amewahi kutumikia nchi hii bila kuwa Mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (either kwa kuteuliwa au kuchaguliwa). Kipindi cha nyuma, Wakuu wa Mikoa pia walikuwa Wabunge kwa mujibu wa nafasi zao tu. Hivyo walikuwa na haki sawa na waBunge wengine na walihudhuria vikao vya bunge na kupewa maslahi yote ya kiBunge. Zaidi ya hayo, Wakuu wa Mikoa pia walikuwa ndio makatibu waKuu wa Chama Mkoa.

Tangu sheria ibadilishwe, Wakuu wa mikoa si wabunge tena, na hawahudhurii vikao vya Bunge kabisa.

Utakumbuka Mzee J.S. Malecela alikuwa karibu sana na watu hawa na aliweza kujenga support base kubwa sana kwao kwa kuwa walikuwa na madaraka makubwa kichama na serikali.
 
- Mkuu wangu kisheria ya Tanzania ya bunge, DK. Malecela legally alianza kuitwa mbunge rasmi baada ya kushinda uchaguzi wa jimbo mwaka 1975, na not before that, na kwa mara ya kwanza alianza kupewa legal rights za ubunge lakini not before that.

- Ingawa alikuwa waziri wa nje na anaingia bungeni, how do you call that sijui, lakini hakuwa mbunge, na hakuwahi kuitwa mbunge period, mpaka aliposhinda legally mwaka 1975.

Hakuna Waziri yeyote wa Jamhuri hii ambae hakuwa Mbunge. Labda kabla ya Uhuru. Katiba iko wazi sana kuhusu suala la nafasi ya Uwaziri na Ubunge.

Katika miaka ya nyuma, Wabunge walikuwa wakiitwa kwa heshima mbalimbali. Kuna wakati walikuwa wakitambulishwa kama Ndungu Mbunge/Spika, Mheshimiwa Mbunge/Spika n.k. insi ya kumuita Mbunge haina maana, chenye maana ni nafasi yake katika Bunge (ipo/haipo).

Mtu yeyote asie Mbunge, hawezi kuhudhuria vikao vya Bunge na kuchangia lolote. Hata Makamu wa Rais au Rais wa ZNZ (sio sehemu ya Bunge) huingia kwenye ukumbi wa Bunge baada ya Spika kuliomba Bunge kutoa ruhusa hiyo. Hakuna Katibu mkuu, au kiongozi yeyote wa serikali ambae si Mbunge anaeweza kuingia kwenye ukumbi wa Bunge kwa sababu zozote ziwazo, bila Bunge kuidhinisha na kutoa nafasi ya yeye kufanya hivyo.
 
Huyu mzee ni mvumilivu na anastahili pongezi kwa hilo.
hivi wakuu huyu mzee kwanini alikuwa tishio sana kwa nyerere mpaka nyerere kutishia kujitoa ccm kama hataaondoa jina lake 1995?mbona alikuwa na uhakika wa kuwaondoa kina msuya,lowasa,kikwete,msekwa et al kwenye vikao vya mchujo hata kwa mizengwe lakini hakutaka kabisa jina la malecela liingie kwenye mchakato ule.kuna sababu nyingine ukiacha serikali ya tanganyika na kampeni yake kufadhiliwa na waarabu?

Nyerere aliamua kuweka msimamo huo baada ya J. S. Malecela kuonekana ku-support serikali tatu wakati akiwa Waziri Mkuu na Makamu wa Pili wa Rais (awamu ya Pili). Hili pamoja na kuvunjwa kwa Azimio la Arusha vilimfanya Nyerere kutokuwa na imani nae.
 
Malecela: Ni Kikwete tu 2010

2009-03-26 12:38:03
Na Joseph Mwendapole

Makamu Mwenyekiti Mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, John Malecela, amesema kuwa mwanachama yeyote wa CCM atakayejitokeza kuchukua fomu kupambana na Rais Jakaya Kikwete katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, atakuwa anapoteza muda wake.

Yeye binafsi ameweka msimamo wake wazi kuwa hatajitokeza kuchukua fomu kugombea kiti cha urais mwakani tofauti na alivyofanya mwaka 1995 na mwaka 2005 na jina lake kuondolewa na vikao vya Kamati Kuu (CC) ya chama hicho.

Alisema mwanachama wa CCM mwenye fikra hizo ni vyema akazifuta mapema na atumie fedha ambazo angetumia kwenye kampeni za urais kuendeleza familia yake.

Aliyasema hayo jana nyumbani kwake Sea View, jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na waandishi wa habari kutoka vyombo vya habari vya IPP.

Alitoa jibu hilo baada ya kuulizwa iwapo atawania urais mwaka 2010 baada ya jina lake kuchujwa katika kinyang`anyiro cha Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005.

``Rais Kikwete ameifikisha nchi sehemu nzuri sana, hakuna wa kumpiku, ametuendesha vizuri tangu tumpe usukani mwaka 2005 na lazima wananchi na wanachana wa CCM wajue kuwa mwaka 2010 ni kituo tu Kikwete hajafika mwisho....mwisho wake wa urais ni 2015,``alisema na kuongeza kuwa yeye hatagombea urais badala yake ataendelea kuwania ubunge katika jimbo lake la Mtera, mkoani Dodoma.

Alipoulizwa kuhusu dhamira yake kutokana na kuondolewa na Kamati Kuu (CC) ya chama hicho katika kinyang`anyiro cha urais mwaka 2005 na kuamua kukata rufaa Halmashauri Kuu (NEC), alisema hadi sasa hana kinyongo.

Alikemea malumbano yaliyotokea hivi karibuni baina ya Mbunge wa Igunga (CCM), Rostam Aziz, na Mbunge wa Kyela (CCM), Dk. Harrison Mwakyembe, kuhusu mjadala wa ununuzi wa mitambo ya Dowans.

Alisema wakati huu wa hali mbaya ya kiuchumi, viongozi wanapaswa kuweka mikakati ya kumsaidia Rais Kikwete ambaye amekuwa akiizunguka dunia kutafuta misaada ya Tanzania, badala ya kuendekeza malumbano.

Alisema badala ya kulumbana hadharani, wanapaswa kupeleka masuala hayo katika Bunge, Serikali au katika chama.

``Kwa kweli tumechoshwa na malumbano haya, hakuna sababu ya kuendeleza malumbano kwani kama suala linahusu serikali kwanini lisipelekwe huko likajadiliwa?

Kama ni la Bunge, kwanini lisipelekwe bungeni? na kama ni la chama kwanini lisipelekwe kwenye chama mpaka watu wanasutana katika magazeti,`` alihoji Malecela ambaye pia aliwahi kuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais kuanzia mwaka 1990 hadi 1995.

Alisema lipo kundi la watu wanaojidanyanga kuwa ipo siku CCM itameguka endapo watajitoa katika chama na aliwataka kufanya hivyo haraka iwezekanavyo.

Alisema hata wakiondoka chama kitabaki imara na hakitatetereka.

``Baba wa Taifa aliwahi kusema kuwa bila CCM imara nchi itayumba, lakini hakumaanisha kuwa chama hiki kitameguka, sasa hao ambao wamekuwa wakitoa vitisho kila kukicha kitameguka ni heri waondoke tumechoka na vitisho vyao,`` alisema.

Alisema CCM haitakubali watu wachache waruhusiwe kuiyumbisha nchi kwa sababu wanazojua wao.

Vile vile, Malecela alisema kamwe CCM haitaruhusu matajiri kuongoza chama hicho na kwamba wanaojaribu kufanya hivyo wanajidanganya.

Alisema chama hicho kitaendelea kuwa chama cha wanyonge na wafanyakazi.

Kuhusu mjadala wa Dowans, Malecela alisema ni sawa na kuchapa bakora mzoga kwani suala hilo lilishajadiliwa na kumalizwa na Bunge.

Alisema anayeona mjadala huo unamaana tena anaweza kuwasilisha hoja yake bungeni.

Kuhusu madai ya wizi wa fedha za umma zinazomwandama Mbunge wa Bariadi (CCM), Andrew Chenge, Malecela alisema hizo ni tuhuma tu na kwamba Mahakama pekee ndiyo yenye uwezo wa kumtia hatiani.

Alisema mtu yeyote anaweza kutuhumiwa hivyo haoni ajabu kwa yanayosemwa kuhusu mwanachama huyo wa CCM.

``Watuhumiwa wako wengi hapa nchini na hata wewe unaweza kuwa mtuhumiwa wakati wowote tu na kisheria mtuhumiwa hana hatia mpaka Mahakama itakapomwona na hatia,`` alisema.

Wakati huo huo, Malecela, ameishauri serikali iyafunge magazeti ambayo yamekuwa yakiandika uongo na mambo binafsi dhidi ya watu mbalimbali.

Alisema magazeti hayo yanakosa habari na badala yake yanaandika uongo na uzushi.

``Imefika wakati sasa serikali ifanye kazi yake...magazeti haya sasa yamekuwa mengi mno na yamefikia hatua mbaya ya kuandika mambo ya uongo,`` alisema Malecela.

Aliongeza kuwa serikali isiendelee kuyafumbia macho na kwamba lazima ionyeshe kuwa haikubaliani nayo kwa kuchukua hatua madhubuti ikiwa ni pamoja na kuyachuja.

Alisema mpaka sasa ripoti zinaonyesha kuwa Tanzania ina magazeti mengi kuliko nchi yoyote barani Afrika.

``Imefikia wakati yanaingilia mambo ya watu binafsi ya ndani kabisa na kuyachapisha..lazima tujiulize haya yanafanyika kwa faida ya nani?`` alihoji.

Aidha, alisema kuwa anaamini vyombo vya habari vimeanzishwa kwa ajili ya kuelimisha umma na si kuandika uongo na kuendeleza malumbano.

Alitahadharisha kuwa hali hiyo ikiendelea, wananchi wanaweza kudhani kuwa uhuru wa vyombo vya habari ni watu kutukanana na kukashifiana.

Hivi karibuni, kumeibuka kundi la magazeti ambayo yamekuwa yakishambulia watu wanaopambana na ufisadi.

Magazeti hayo yamekuwa yakiandika habari za uongo na za kutunga dhidi ya watu wanaomuunga mkono Rais Kikwete katika kupambana na vitendo vya ufisadi.

SOURCE: Nipashe
 
Bubu nakubaliana nawe mia kwa mia, hii tabia yapaswa itokemezwe mbali kuzimu. Huyu mzee kachoka nahisi anawezaje kuamua kwa ajili ya wengine huu kama si uchizi ni nini? Kama yeye hagombei si awaache wengine wagombee yanamhusu nini yeye? Au hii ndio demokrasia ya CCM?

Amenichekesha zaidi anapomsifu rais kwa kuzunguka dunia nzima na bakuli la kuomba misaada huku akiacha kile kilichopo (rasilimali) kinaliwa na wachache nyumbani. Mzee Malechela ni nani aliyekuambia tunaweza kuendelea kwa misaada pasipokutumia vyema rasilimali zetu? Mungu wangu kama wewe pia unafikiri hivyo then we have a long way to go as a country.
 
mzee anapalilia kitumbua chake, si mnajua yeye ni mjumbe wa kamati kuu ya ccm kwa maisha yake yote?

hili la kugombea tena jimbo la mtera sasa simwelewi kwa kuwa ana miaka75 by the time anamaliza muhula wake atakuwa na umri wa miaka 81
 
- Hivi kuna tatizo gani mimi nikisema ni lazima Dr. Slaa awe rais kwenye uchaguzi ujao? Sasa kama DK. Malecela anamtaka Rais Kikwete aendelee tatizo likpo wapi kwani hatakiwi kuwa na choice zake binafsi na kuzisema wazi kama sisi raia wengine?

- Naomba elimu hapo?

FMES!
 
- Hivi kuna tatizo gani mimi nikisema ni lazima Dr. Slaa awe rais kwenye uchaguzi ujao? Sasa kama DK. Malecela anamtaka Rais Kikwete aendelee tatizo likpo wapi kwani hatakiwi kuwa na choice zake binafsi na kuzisema wazi kama sisi raia wengine?

- Naomba elimu hapo?

FMES!

FMes,

Wewe ukisema wala haina shida. Mie pia, BAK, MJKK nk. Ila huyu ni John Malecela. Hiyo ndiyo tofauti. Kwa umri wake na uzoefu wake na .... zake maana sijui niseme nini kuonyesha ukubwa wake huyu Mtani wangu ni kuwa HERI AKAE KIMYA. Akija Clinton wa Tanzania na amuondoe Mchekaji, atakuja kusimama na kumwangalia usoni huyo mtu?
Inabidi tu kujua kuwa , hata Ma-DJ siku hizi wanakuwa Marais. Kwa mana hiyo Malecela inabidi aangalie anasema kitu gani. Heri akae kimya au aseme ndiyo Demokrasi, ila yeye hagombei.

Tuseme William Malecela agombee Urais na ashinde. Alete mabadiliko makubwa sana Tanzania design ya Putin vile. Mali zote ziwe za Watanzania tena. Umeme kibao, maji safi, hospital zina nafuu, maji taka hamna, mji msafi na usafiri una nafuu..... je Mzee Malecela atamwambia nini mwanaye? Atamlaani kwa kumuondoa Kikwete na kuleta maendeleo hayo au ataanza kumsifu? Na akisifu, watu wakamkumbusha maneno yake........
 
FMes,

Wewe ukisema wala haina shida. Mie pia, BAK, MJKK nk. Ila huyu ni John Malecela. Hiyo ndiyo tofauti. Kwa umri wake na uzoefu wake na .... zake maana sijui niseme nini kuonyesha ukubwa wake huyu Mtani wangu ni kuwa HERI AKAE KIMYA. Akija Clinton wa Tanzania na amuondoe Mchekaji, atakuja kusimama na kumwangalia usoni huyo mtu?
Inabidi tu kujua kuwa , hata Ma-DJ siku hizi wanakuwa Marais. Kwa mana hiyo Malecela inabidi aangalie anasema kitu gani. Heri akae kimya au aseme ndiyo Demokrasi, ila yeye hagombei.

Tuseme William Malecela agombee Urais na ashinde. Alete mabadiliko makubwa sana Tanzania design ya Putin vile. Mali zote ziwe za Watanzania tena. Umeme kibao, maji safi, hospital zina nafuu, maji taka hamna, mji msafi na usafiri una nafuu..... je Mzee Malecela atamwambia nini mwanaye? Atamlaani kwa kumuondoa Kikwete na kuleta maendeleo hayo au ataanza kumsifu? Na akisifu, watu wakamkumbusha maneno yake........

- Mkuu sijaona popte pale unapojibu swali, Obama ameichagua timu ya North Carolina kushinda ubingwa wa NCAA what is wrong with that?

- Mkuu haya mambo wakati mwingine mnaya-over do, DK. Malecela anayo haki kama wananchi wengine wote kusema anayofikiri na ndio demokrasia yenyewe tunayoitaka, otherwise ni ku-reveal our inferior na fear.

- Kwenye demokrasia huwezi kumwambia mwananchi yoyote akae kimya kwa sababu hutaki mawazo yake, that is low mkuu! Badala ya siasa na great thinkers mnashusha hadhi wakuu!
 
Back
Top Bottom