Malengo yangu mwaka 2021 ni kuacha pombe, umalaya na ku-bet

Malengo yangu mwaka 2021 ni kuacha pombe, umalaya na ku-bet

Mimi nimefanikiwa kupunguza pombe kwa asilimia 80 ingawa hela zinawasha Sana mfukoni
Nakushauri ufanye kazi bila malipo ili usipate huo usumbufu wa mwasho. Or else, kumbuka wasio na jinsi ya kupata japo mlo wa siku. Ukiwasaidia hao, maisha yako yatakuwa yenye furaha na amani zaidi. Bill Gates anatumia mali yake perecentage kubwa kwa ajili ya philanthropy.
 
kwa mtazamo wangu atakuwa ametoka kwenye kifungo kimoja na kuingia kifungo kingine. labda kama hawezi kujiongoza basi itambidi aokoke ili vitabu vya dini vimwongoze badala yake.
Truth be told, hakuna mwanadamu anayeweza kujiongoza mwenyewe kwa akili yake, hata angekuwa genius mara elfu na nusu ya Stephen Hawking ama Newton and Albert Einstein. Our beings are, as it were, ensamples of automobiles -- whether automatic ama robotic -- there has to be someone somewhere "pulling strings" to ensure smooth navigation.
 
Wakuu salaam!

Mwaka 2020 Nimeamua na nimedhamiria kuacha mambo haya:

1. Pombe
2. Umalaya
3. Ku-bet

Hii combination inafanya natumia zaidi ya laki 6 kwa mwezi wakati kipato changu ni chini ya 500k, najikuta katika madeni ya kijinga kijinga.

Nimedhamiria kumrejea Muumba, yaani kwa dhambi nilizotenda na nilizonazo natamani hata nisali Dini zote!

MARRY X MASS & HAPPY NEW YEAR IN ADVANCE

NB: MNIWEKE KATIKA MAOMBI
Namba moja na namba mbili vinanisumbua Sana.Mkuu tupeane mbinu tutanyeje.
 
ni wewe wasema! ila amini ya kwamba kila kitu kinawezekana endapo ukiamua hivi vitu ni swala la mindset
Truth be told, hakuna mwanadamu anayeweza kujiongoza mwenyewe kwa akili yake, hata angekuwa genius mara elfu na nusu ya Stephen Hawking ama Newton and Albert Einstein. Our beings are, as it were, ensamples of automobiles -- whether automatic ama robotic -- there has to be someone somewhere "pulling strings" to ensure smooth navigation.
 
Jitahid kutafuta kitabu kimoja kinaitwa POWER OF YOUR MIND.(kina pages chache sana kama

Mfano: MTU unataman kuacha pombe,lkn unajikuta baada ya siku mbili tatu unakunywa tena zaid kama umerogwa.

Au unakataa kununua mala.ya unajikaza lkn unajikuta unatongoza na kununua baada ya muda na kupoga three some KBS...

Hii sio umerogwa Bali POWER OF YOUR SUBCOSCIOUS MIND PLAYS PART.
Tunakuombea ufanikishe adhma yako.
Doh....hiki hata mm kinanihusu,kinapatikana wapi?
 
Hutaweza lolote hapo maana huna nia ya kuacha dhambi bali ukosefu wa pesa ndo unakufanya ujilazimishe.
Ukipata pesa mbona nyuchi zitaimba hallelujah..
 
Shetani nae hapendezwi na mipango yako, Maana wafuasi wake watapungua. Atakuletea pisi kali zinazokunywa pombe badala ya kuacha pombe utaongezewa zaidi wanywaji na kampani kama hizo usingetangaza maana umetangaza vita na shetani.
Kweli mkuu, mara na odd mikeka zinakuwa zakupendeza. Hivyo mkuu kama anataka mabadiliko ya kweli basi aanze mapema kutafuta njia mbadala kuliko kutangaza. Shetani pia yupo kazini
 
Hutaweza lolote hapo maana huna nia ya kuacha dhambi bali ukosefu wa pesa ndo unakufanya ujilazimishe.
Ukipata pesa mbona nyuchi zitaimba hallelujah..
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Namba moja na namba mbili vinanisumbua Sana.Mkuu tupeane mbinu tutanyeje.
Angalia unakojikwalia siyo unapoangukia; root ya problem ni mindset finyu ambayo haioni maana bora ya maisha. Usiendeshe maisha yako as if huna busara. Usiruhusu mwili utawale akili, ndiyo matokeo yake hayo.
 
ni wewe wasema! ila amini ya kwamba kila kitu kinawezekana endapo ukiamua hivi vitu ni swala la mindset
Mindset + decisive action (power to act). Unaweza kuwa na mtazamo mzuri tu, lakini kitendo husika ndiyo kila kitu.
 
Kweli mkuu, mara na odd mikeka zinakuwa zakupendeza. Hivyo mkuu kama anataka mabadiliko ya kweli basi aanze mapema kutafuta njia mbadala kuliko kutangaza. Shetani pia yupo kazini
Hata usipotangaza, kama huna msimamo na nia madhubuti ya kubadilika, hapo Shetani kukukwadua ni ada. Unaweza kumficha Iblisi siri gani kimfano??? Siri pekee anayoogopa Iblisi ni wewe kujificha kwenye mionzi ya nuru kutoka juu.
 
Hutaweza lolote hapo maana huna nia ya kuacha dhambi bali ukosefu wa pesa ndo unakufanya ujilazimishe.
Ukipata pesa mbona nyuchi zitaimba hallelujah..
Wakati mwingine Mungu akitaka kukuokoa anaruhusu mirija ya hazina zako zinazokupa nguvu, ufahari, afya, kiburi, ujasiri na mishemishe kibao zidorore kwa muda ili utimamu wa akili na mtazamo sahihi wa maisha vikurudie. Ndivyo alivyofanya kwa MICHAEL SON, sasa anaelewa kuwa kuendelea kuendekeza starehe duni za jinsi hiyo ni kazi bure tu na haina tofauti kubwa na kupalilia kwa hiari ugonjwa sugu usiopona.
 
Sawa, ila kipato kikiongezeka atarudi palepale, maana kikwazo ni pesa.
 
Sawa, ila kipato kikiongezeka atarudi palepale, maana kikwazo ni pesa.
You are missing a crucial point. Kukubali hoja yako ni sawa na kusema kwamba kila mwenye mafanikio na utajiri na mali na pesa ni malaya, mlevi na mgonjwa wa kubeti. Haya mambo ni maradhi ya akili na moyo uliochanganyikiwa haujui hasa thamani na maana ya maisha -- kwa watu kama hao, kunavyokucha ndiyo hivyo tu, kesho ipo na tutaona cha kufanya. That kind of mindset is not only self-delusive but also short-sighted and purposeless.
 
Ushauri wangu kama umedhamiria kuacha mshirikishe mungu juu ya hili, funga angalau hata siku 3 alafu andaa sadaka na uwe unaiombea ndani ya hizo siku ukimwomba mungu akusaidie uweze kuyaacha hayo mambo, uanze mwaka mpya 2021 na mambo mapya. Hapo utafanikiwa, ila ukitumia akili zako mwenyewe ni vigumu kwa sababu hayo mambo yanasukumwa na shetani na kumshinda shetani bila kumshirikisha mungu haiwezekani.
 
Well said. No more, no less!!!
 
Back
Top Bottom