strong star
Member
- Jul 15, 2021
- 36
- 42
Watoto wetu wa leo ndio taifa letu la kesho, Ikiwa tutawaandaa vyema tutatengeneza jamii na taifa bora pia lenye nguvu baadae na kufikia malengo kwa haraka zaidi .
Tukitaka kufikia malengo na kuwa na taifa bora na lenye nguvu kwanza tunatakiwa kujenga misingi imara kwa watoto wa kike kwani:
- Ana uwezo mkubwa wakufikili na kutatua changamoto sawa au pengine zaidi ya mtoto wa kiume.
- Ni ukweli kwamba amesahaulika katika jamii hasa katika shughuli za maendeleo .
- Ananyanyasika na kudhalaulika katika jamii.
- Kumkomboa mtoto wa kike nikukomboa taifa la kesho.
- Juhudi zake na maumivu yake ayathaminiki katika jamii.
- Mtoto wa kike wa sasa ndie mama wa baadae hivyo tukimuandaa vyema tutajenga taifa bora.
Hivyo basi, yatupasa kufahamu nakutendea kazi njia bora zaidi za kumkomboa mtoto wa kike katika jamii na kutengeneza taifa bora la kesho,
Mwezeshe kujiamini zaidi
Tangu akiwa bado mdogo wazazi au walezi yatupasa kumuandalia mazingira yatakayo mfanya mtoto wa kike ajiamini zaidi dhidi ya jamii yenye unyanyasaji wa kila aina kama vile ndoa za utotoni,ukeketaji, na kila aina ya mateso juu yake ili aweze kupinga nakufanya maamuzi yeye mwenyewe na kujitegemea
Usawa katika malezi na usimamizi
Bado jamii pamoja na wazazi/walezi tunashindwa kuhakikisha tunaweka usawa kati ya watoto wa kike na wa kiume katika hali zote kama vile kazi za nyumbani,muda wa kupumzika na kujisomeea, kujiendeleza kielimu hasa ikitokea mtoto wa kike kashindwa kuendelea.
Elimu ya kutosha ili aweze kujitegemea
Yatupasa kuhakikisha mtoto wa kike anapata elimu ya kutosha ili aweze kujitegemea na kujisimamia mwenyewe na kuingia moja kwa moja katika shughuli za uzalishaji mali na kutumia fulsa na nyazifa mbali mbali za uongozi.
Uhuru wa kufanya kazi na mawasiliano
Jamii inapaswa kuhakikisha inampatia uhuru wa kuchagua kazi ya kufanya, pia mawasiliano na mwingiliano wa kutosha ili kuhakikisha anajiona mwanajamii moja kwa moja na kutatutua changamoto zake mwishowe kujiletea maendeleo na jamii kwa ujumla.
Mfanye ajiheshimu na kujipenda
Tangu akiwa chini kabisa jamii pamoja na walezi yatupasa kuhakikisha unamuandaa mtoto wa kike kujieshimu na kujipenda ili jamii iweze kumheshimu na kumpenda na kutambua mchango wake zaidi na sio jinsia yake kwani bado jamii nyingi zinaangalia sana jinsia na sio mchango wa mtu katika maendeleo.
Muandae kuwa mpambanaji na asiyekata tamaa
jamii yatupasa kumwandaa na kumjengea roho ya upambanaji zaidi ili katika makuzi yake aweze kuvuka changamoto zake na kushinda majalibu yake yeye mwenyewe kama ilivyo kwa watoto wa kiume.
Mfanye aitambue thamani na mchango wake katika jamii
Jamii yatupasa kuhakikisha ulinzi wa kutosha wa kila unyanyasaji kwa watoto wa kike kama vile ndoa za utotoni, ukeketaji, ndoa za kulazimishwa, nadhalika. Pia kuhakikisha anatambua thamani, umuhimu na mchango wake katika jamii husika .
Kwa hakika, haya yakitekelezeka tutajenga taifa bora la sasa na la baadae katika kuleta maendeleo katika taifa letu.

Upvote
3