Sema Tanzania
JF-Expert Member
- May 18, 2016
- 251
- 466
Katika miaka ya hivi karibuni malumbano ndani ya nyumba zetu yameshika hatamu. Tumeshuhudia tabia iliyozoeleka kwa wazazi - baba na mama wakipigana, kurushiana maneno, matusi na kadhalika mbele ya watoto tena bila aibu. Kisaikolojia mtoto hujengeka zaidi na kuwa mwenye furaha kutokana na kuwepo kwa hali ya amani na upendo wa wazazi. Kutofautiana kimtazamo hakuepukiki katika familia ingawa licha ya kuwepo kwa tofauti za hapa na pale, haitakiwi hata kidogo watoto wetu wakapata kuingizwa katika malumbano. Watoto hawapaswi kushuhudia mivutano kati yenu. Mkiweza vumilianane hadi pale mnapopata wasaa kukaa faraghani kuzozana.
Kimsingi yapo madhara makubwa ambayo mtoto huweza kuyapata pindi anaposhuhudia wazazi wakigombana kila kukicha makala haya yanalenga kuangazia madhara hayo hapa chini.
Mtoto anaweza kupoteza muelekeo wa kimasomo sambamba na kushuka kitaaluma au hata kuamua kuacha shule. Ukitulia ukafanya tafakuri makini ya kwa nini baadhi ya watoto hawafanyi vizuri darasani bila shaka mazingira ya nyumbani hayako rafiki. Badala ya kuwafokea kwa kuwashinikiza kuwa wamezidi michezo na ndiyo maana hawafanyi vizuri katika masomo, hebu tujiulize, mtoto atawezaje kujisomea ikiwa nyumbani hakukaliki? Vurugu mtindo mmoja. Badala ya kufikiria masomo, mtoto ataanza kuwaza hali ilivyo nyumbani. Yatupasa kubadilika na tutambue kwamba sisi ndiyo manahodha kwenye familia zetu.
Kupatwa na msongo wa mawazo ulio juu ya uwezo wake hivyo kupoteza furaha na kujihisi mnyonge kila wakati. Hatupaswi kuwafanya watoto wetu wawaze sana kuhusu matatizo yetu badala yake sisi ndiyo wenye jukumu la kuwawaza wao. Tusiwafanye watoto wakose kujiamini mbele ya watoto wenzao, wakubwa zao na hata jamii kwa ujumla.
Mtoto anaweza kuondoka nyumbani na kuamua kuishi maisha yake kwa sababu upendo umetoweka nyumbani. Hali kama hii inaweza kutokea kwa kuwa malumbano yenu yatamfanya mtoto ahisi ushirikiano wa kumlea haupo tena na hivyo anaamua kujiweka huru. Vilevile, anaweza kuondoka ili kuepuka malumbano anayoyashuhudia ndani ya nyumba. Swali ni kuwa, huyu mtoto atakua mgeni wa nani? Ataishi wapi? Atakula nini? Kwa kiasi kikubwa, mazingira kama haya huchangia ongezeko la watoto wa mitaani na waishio kwenye mazingira magumu.
Tunao ushahidi wa baadhi ya watoto wanaoishi mtaani kwa sasa kuwa walikimbia majumbani mwao kuepuka misuguano ya baba na mama. Mazingira rafiki ya malezi ni pamoja na kuvumiliana baina ya watu wazima mliopo ndani ya nyumba mnamo-lelea watoto wenu. Ikishindikana kuvumiliana bora mpumzishane kwa kutengana na hata talaka. Vyote hivi ni kuepuka kuwapa watoto misongo na mizigo isowahusu.
Tujitahidi kudumisha mahusiano yetu ili tuwalee watoto na kuwajengea muelekeo sahihi kwani misingi bora ya maisha yao ya baadae huanzia kwetu wazazi. Yatupasa tukumbuke usemi usemao majuto ni mjukuu, huja kinyume! Malezi ya watoto yanahitaji mabadiliko makubwa ya tabia za wazazi. Ukitaka kuzaa lazima uliwaze jukumu hili kinagaubaga. Uzazi ni zaidi ya kuitwa baba. Kuitwa mama. Uzazi ni wito wa kubadili maisha yako ili maisha wa watoto unaowalea yaweze kuwa bora sasa na hata watakapokuwa wakubwa.
Kwa maoni na ushauri tupigie simu namba 116 ambayo ni maalumu kwa huduma za mtoto nchini. Huduma hii haitozi malipo toka mitandao yote nchini. Vilevile unaweza kutupata kupitia ukurasa wetu wa Facebook: Sema Tanzania; Twitter: @SemaTanzania na www.sematanzania.org