Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mmetoka kivipi?Tumeambiwa sana ujinga na bado tumetoka fureshiii tu, endeleeni kuiga kwenye tamthilia.
Mmetoka kivipi?
Sifa kubwa ya mtoto kutokuwa na dukuduku moyoni,mtoto abebi mambo moyoni na pia sifa nyngne ya watoto hawabaguani hata ukisema usicheze na yule hatokuelewa tuishi kwa upendo na kuwajali watotoMimi baba yangu alikua bandidu balaa.
Nakumbuka nilikua msingi kila nikimletea report home niko wa kwanza darasani baasi akawa ananifokea balaa. Ananiambia sio unafikiri kuwa wa kwanza ni issue hakuna atakae kusifia hapa unatakiwa ukaze buti uendelee kuwa hapo maana hiyo ni kazi kubwa. Baasi mpaka nilikua nalia yaani nasema huyu mzee vipi badala afurahi ananigombeza.
Sema baadae ananinunulia soda na kuku baasi maneno yake yoote ya shombo natupa kule naji noma vitu vizuri.
Mpaka sasa hivi ana principle yake moja kwamba mtoto wa kiswahili usimuonyeshe jino. Yaani usimchekee. Dah hili kwa kweli alilitekeleza maisha yetu karibia yote ya utoto. Yaani baba atacheka na wenzake tukiingia tu sisi anaweka wa mbuzi. Kakunja uso. hahahahaha.
Hizi principle zake bhana kijeshi sana na nimeshindwa kabisa kuzi implement kwa mwanangu. Ujeshi mwingi sana aisee, Japo mwanangu akifanya kosa kichapo cha mbwa koko kinamuhusu then baada ya hapo tunacheza kama watoto vile.