Malezi: Mambo 20 ambayo hutakiwi kumwambia mtoto wako

Kati ya Joyce Mkuya na Konyagi ni nani alimwangusha mh Mbowe?
 
Tumeambiwa sana ujinga na bado tumetoka fureshiii tu, endeleeni kuiga kwenye tamthilia.
 
Reactions: BRB
Umekataza kila kitu sasa tutawafokea nini watoto zetu 🙄
 
Namba 5 napinga.

Hiyo unaweza kumuharibu mtoto au akawa anaharibika bila wewe kujua au kwa kujua kisha ukamuacha.
 
Mbwa wewe!! Mama kamtukana mwanae! Nikadakia, habari "mama mbwa " akaja juu mwisho nikamshinda kwa hoja. Acheni hizo!!

Sent from my TECNO-N2 using JamiiForums mobile app
 
Reactions: Auz
Hapo point kubwa ni kutomtusi mtoto tu. Hayo mengine yanafuatana na mazingira.

Mf. Kuna tatizo gani kumwambia mtoto "niache nipumzike?" Au katoto kamevaa sketi unakaambia "wavulana hawafanyi/hawavai hivyo?'
 
Naona sasa humu ndani mmeanza kuvuka mipaka hadi mnatufundisha jinsi ya kulea eehhhh....
 
Namba moja mpaka ishirini asiambiwe lolote,litakuwa toy lisilukuwa na betri na siyo mtoto.
 
Hiyo namba 5 hiyo utawapoteza watu.

Huo utaratibu wa kuwalea watoto open minded kwamba wakikua watakuja kuchagua wanataka kuwa nani utajikuta umekuza wa kina delicious.
 
Sifa kubwa ya mtoto kutokuwa na dukuduku moyoni,mtoto abebi mambo moyoni na pia sifa nyngne ya watoto hawabaguani hata ukisema usicheze na yule hatokuelewa tuishi kwa upendo na kuwajali watoto
 
Hiyo namba 15, wazazi wengi hawajui kuwa watoto hawabaguani hata siku moja sifa kuu ya watoto kupendana hata ukipandikiza chuki utafeli ww
 
Najaribu kuwaza nisingeadhibiwa na wazazi wangu pale ninapokosea sijui ningekuwa kwenye mazingira gani.nahisi ningekosa adabu kwa kiwango kikubwa mno.

Watoto wangu watakapofanya makosa,adhabu lazima iwepo 💯.nitakuwa Rafik yao sana lakini wakileta uzembe watachezea mikwaju.

Hiyo ya kusema ngoja baba yako aje!😅😅nahisi haitokuja kutoka kinywani kwangu hata siku moja(nafikiri ni kwa sababu na mimi sikuwahi kuisikia ikitoka kinywani mwa mama yangu).

Mtoto ukimlegezea sana anakuja kukuaibisha aiseh.mlee vizuri,mpatie anachostahili kwa wakati husika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…