Malezi: Mnaotumia condom wasaidieni wanaopaswa kutumia P2 kesho msikose watoto

Malezi: Mnaotumia condom wasaidieni wanaopaswa kutumia P2 kesho msikose watoto

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
Kununua na kutumia kondom unachangia uchumi, unadhibiti magonjwa na unalinda mimba zisizotarajiwa. Hakuna side effects kwenye via vya ndani vya uzazi na ni njia salama.

2. Watoto wangu Mnaotumia P2/ 72 hrs na nyingine nawapongeza kuchangia uchumi na kudhibiti mimba zisizotarajiwa. Ila amkwepi gono Wala VVU hivyo hii siyo njia salama. Bora mimba kuliko VVU.

3. Natambua mwili unahitaji Tiba na Katika makuzi kujizuia ni ngumu. Ila naumia kuwataarifu kwamba maamuzi yenu ya kutumia vidonge kupata yanaambatana na maamuzi yakutokuzaa HUKO mbeleni endapo utafanikiwa kuvuka bila vvu.

4. Kwa watoto wangu wa kiume, unapotoa pesa Kwa ajili ya P2 jiulize mkeo mtarajiwa HUKO aliko ametumia kiasi gani Cha P2. Usipotoa pesa ya P2 may be utamlinda mkeo mtarajiwa asipate matatizo ya uzazi lakini pia kavu Ina vvu. Jilinde.

Niwaombe watoto wangu wa kike sisitizeni condom mpunguze matumizi ya P2. Tumieni kalenda ila mtembee na vipimo vya vvu. Mkidhamiria mtaweza. Mahusia ya mama, nataka kuona mnapata watoto. Msiombe kukosa uzazi it pains regardless the amount of wealth you have.
 
Hivi ndiyo kusema hakuna kabisa mipira ambayo ni laini kuliko hii iliyo jazana madukani?

Yaani ukijaribu kuitumia wakati umelewa, unakuta humalizi tu! Mwisho unaamua kuuza mechi. Ulabu ukiisha, unajikuta unajuta kweli kweli! 😫
 
Mada gani tena hizi wajameni wikendi yote hii tumejiachia kwa raha zetu,,,mwisho utukimbizie ving'asti. weita ongeza kama tulivo!
 
Waambieni wagunge hadi ndoa. Mbona sisi tuliweza? Hii mi-broiler sijui itaweza kuvumilia na kujizuia nini tu?
Kwamba wote waliomo ktk ndoa hawafanyi ngono hatarishi?
Hawachepuki na kufanya kavu kavu?

Sijaelewa umetumia mantiki (logic) gani kutoa kauli au ushauri huu?!!
 
Kununua na kutumia kondom unachangia uchumi, unadhibiti magonjwa na unalinda mimba zisizotarajiwa. Hakuna side effects kwenye via vya ndani vya uzazi na ni njia salama.

2. Watoto wangu Mnaotumia P2/ 72 hrs na nyingine nawapongeza kuchangia uchumi na kudhibiti mimba zisizotarajiwa. Ila amkwepi gono Wala VVU hivyo hii siyo njia salama. Bora mimba kuliko VVU.

3. Natambua mwili unahitaji Tiba na Katika makuzi kujizuia ni ngumu. Ila naumia kuwataarifu kwamba maamuzi yenu ya kutumia vidonge kupata yanaambatana na maamuzi yakutokuzaa HUKO mbeleni endapo utafanikiwa kuvuka bila vvu.

4. Kwa watoto wangu wa kiume, unapotoa pesa Kwa ajili ya P2 jiulize mkeo mtarajiwa HUKO aliko ametumia kiasi gani Cha P2. Usipotoa pesa ya P2 may be utamlinda mkeo mtarajiwa asipate matatizo ya uzazi lakini pia kavu Ina vvu. Jilinde.

Niwaombe watoto wangu wa kike sisitizeni condom mpunguze matumizi ya P2. Tumieni kalenda ila mtembee na vipimo vya vvu. Mkidhamiria mtaweza. Mahusia ya mama, nataka kuona mnapata watoto. Msiombe kukosa uzazi it pains regardless the amount of wealth you have.
Kwa hiyo watoto wafanye ngono kwa kutumia condom?
 
Elimu itolewe zaidi kuhusu matumiz ya hicho kidonge faida na hasara zake nadhani itawasaidia mabinti wengi kuacha kutumia vidonge hivyo kiholela.
 
... mbona rahisi; serikali izuie importation ya hizo p2/72.
 
ongeza sauti mkuu huku mtaani zimekua pipi kwenye mabegi ya mabinti zetu
Binti anaanza kuliwa akiwa na miaka 14 halafu anakuja kuolewa akiwa na miaka 25, miaka yote 11 anabutuliwa tu na wahuni kitaani, amemeza p2 za kutosha. Hivi binti wa hivi anastahili kweli kutolewa hata hiyo mahari?

Tumezaliwa wakati mbaya sana[emoji852]
 
Kama sikosei hii mada ya P2 itakuwa imerudi tena hapa jamvini hata mwezi haujaisha. Hivi siku hizi wataalamu/ wanataaluma wamepungua sana hapa jamvini au wameamua kupotezea hili jukwaa? Hili suala ni "sensitive " sana lakini tokea lilipokuja mara ya kwanza mpaka sasa sijaona hoja za kitaalamu kutoka kwa wenye fani yao. Jamani wenye fani yenu mje msaidie huku kwani kuna tetesi mitaani huko kuwa hivi vidonge vinatumika vibaya na mabinti na vikitumika muda mrefu vinasababisha watoto kupatikana kwa shida.
 
Back
Top Bottom