Ila akiwa young MJ1 you are a bit safe... tegemea na the guy you get.... Unajua kaka/baba zetu wa ajabu saana, hivi hujagundua mara nyingi kua mwanaume akikupenda kwa dhati, anapenda the whole package, sometimes hata hajali kua una watoto hata kumi! lol... As long you are his... yeye ndo furaha yake, na siku moja moja hata atataka aspend time na wanao kidogo (yaani wala sio kwa kujifanisha bali kutaka...)
-Strange-
Umeiweka vyema AshaDii, nashukuru.
Katika picha za hapo juu, nadhani wachache watakuwa wamegundua hiyo ya Barack Obama na wazazi wake. Indonesian Dad, American Mum, na dadake. Nitafanya jitihada kutafuta na kusoma kitabu kinachoelezea maisha yake bwana huyu. Yeye ni mfano mzuri wa hii mada, unajua kwanini?
Namfikiria huyu bwana Kuanzia Baba Muafrika, mama Mmarekani Mkristo, dada Indonesian American, amekulia Hawaii, Indonesia, na sasa ni American 1st Black president. Kuna kitu kilichompa 'uti wa mgongo' wa achievements zake. Kuna kitu kilimzuia na kuondoa prejudices maishani mwake.
Tofauti na sisi tulio sensitive hata kwa kuambiwa wewe mweusi...wewe dini fulani, nk...
However kwa wale ambao wanaoana dini tofauti athari ya malezi kwa mtoto naona sio mbaya saana but sometimes yaweza kua hata for the better Yule mtoto anakua exposed to two sides of the religion i.e. Islam vs Christianity.. IMO naona kama mtoto anakua na exposure nzuri, na pia humuwekea busara Fulani ambayo imetokana na ile tolerance ya wazazi ya dini ya mtu mwingine na the like .
Tukirudi kwenye mada. Kwa mtazamo wangu, namini malezi ya "mtoto wa mke wangu" yatahitaji ushirikishwaji wa baba yake haswa kwenye maamuzi ya msingi kabisa ambayo najua yanaweza kuathiri maisha ya mtoto mbele ya safari hata kama mama mtu atapinga. Mnakubaliana na hili au mnanishauri tofauti?
Umeiweka vyema AshaDii, nashukuru.
Katika picha za hapo juu, nadhani wachache watakuwa wamegundua hiyo ya Barack Obama na wazazi wake. Indonesian Dad, American Mum, na dadake. Nitafanya jitihada kutafuta na kusoma kitabu kinachoelezea maisha yake bwana huyu. Yeye ni mfano mzuri wa hii mada, unajua kwanini?
Namfikiria huyu bwana Kuanzia Baba Muafrika, mama Mmarekani Mkristo, dada Indonesian American, amekulia Hawaii, Indonesia, na sasa ni American 1st Black president. Kuna kitu kilichompa 'uti wa mgongo' wa achievements zake. Kuna kitu kilimzuia na kuondoa prejudices maishani mwake.
Tofauti na sisi tulio sensitive hata kwa kuambiwa wewe mweusi...wewe dini fulani, nk...
Tukirudi kwenye mada. Kwa mtazamo wangu, namini malezi ya "mtoto wa mke wangu" yatahitaji ushirikishwaji wa baba yake haswa kwenye maamuzi ya msingi kabisa ambayo najua yanaweza kuathiri maisha ya mtoto mbele ya safari hata kama mama mtu atapinga. Mnakubaliana na hili au mnanishauri tofauti?
...hapo sasa, halafu eti baba mzazi anamkurupua ex-wife wake kwanini mtoto kaenda outing na 'uncle' wake!
Mke/mtoto ana kosa gani kuendelea na maisha yao?
Mbu mh kuna scenerio nyingine ni ngumu kidogo kwa Current spouse kuingilia bana........Mfano mie najua Ex-wangu hatoi matunzo lakini kila kukicha aja na visharti vya kumpeleka mtoto shule zenye majina na accounts ambazo mwisho wa siku jukumu lote linaangukia kwangu, afu we uje useme ni haki ya mtoto au ya Ex kwa kuwa analazimik kuingia katika maisha yangu by default......hapana
Mbu mh kuna scenerio nyingine ni ngumu kidogo kwa Current spouse kuingilia bana........Mfano mie najua Ex-wangu hatoi matunzo lakini kila kukicha aja na visharti vya kumpeleka mtoto shule zenye majina na accounts ambazo mwisho wa siku jukumu lote linaangukia kwangu, afu we uje useme ni haki ya mtoto au ya Ex kwa kuwa analazimik kuingia katika maisha yangu by default......hapana
Mzazi ambae yupo genuine hawezi chukia mtoto wake akienda na uncle wake (hasa kama imehalalishwa) for ataelewa kua mtoto needs some balance na breathing space ya hio divorce amepitia, na pia kua mtoto hatakiwi kabisa ku smell any hint of hate between the parents and step parent... Yaani wivu tu ndo yaweza fanya hayo ulosema yatokee...
Akhsante....
...kuhalalishwa vipi tena naye keshamuacha mke bana?...'asokuwapo na lake halipo!'
yaani mimi leo wanangu waende Outing na Boyfriend/fiancee wa mama yao basi nihamaki? Busara gani hiyo...lol!
.
dahhh,...akhsante ya nini sasa na wewe..lol...yani umeona maneno ya Mwj1 kamili 100%?
Topik ya Msukule mshaisahau nyie,...hawa Ex-Spouses wanakausumbufu sana kwenye masuala ya mtoto/watoto
inabidi kwenda nao hivyo hivyo...'unauma huku unapuliza!'
Mbu hicho kitu cha kuangalia saana sema tu wazazi wengi hupuuzia...
Haipendezi kabisa kuonesha wanao your boyfriend/lover kama you are
not yet sure about the relationship... believe me you.... mpaka pale you
know you have a future then the kids can be involved - for waweza ishia
kua in a few years ume wa introduce to more than four of your lovers...
Not healthy for the child(ren), na hata ile heshima kwa watoto plus morals...
solution usioe mtu aliyezaa tayari.
Akhsante....
...kwenye hoja ya msingi niligusia mila na tamaduni zinavyoweza leta athari pia kwenye jambo hili.
Hapa sitazungumzia ukabila, mfano binti wa kizaramo kalelewa na baba wa kambo huko Usukumani
kiasi cha binti kwa kiwango kikubwa kachukua mila na tamaduni za huko.
Linapokuja suala la binti anataka kuchumbiwa, JE? zile taratibu zetu za kupeleka posa sijui ndio kifunga uchumba,
mahari nakadhalika, Je?....hapa napo pakoje? Watafutwe ili washirikishwe ndugu na jamaa wa mke, au haya mambo yeshapitwa na wakati? Sidhani kama ni jambo la ajabu kuona siku ya harusi hata mama mlezi anapewa tuza zake kwa kumlea vyema mtoto japo mzazi wake yupo!
Umeona AshaDii! Kuna vitu vingine bana mtu wa nje hawezivielewa kivile kwa kuwa si yeye alokivaa kiatu kile...kunamaudhi mengine hukufanya mpaka sometimes u'mnunie' hata spouse wako kisa unaona anamtetea Ex lol!!
Kuna mdada mmoja yeye ameolewa akiwa na watoto wawili wa Ex- ni baada ya kuteswa na kupigika ipasavyo na Ex akamhakikishia kabisa kuwa hakuna atakae'mpenda'........akapendwa yeye na wanae.......Ex kagoma kutoa matunzo anadai akitaka awalipie wanae ada basi agaiwe na mbuchuchu kwanza!!............Mdada current spouse yuko njema na hana shida kabisa juu ya watoto hawa na watoto wanampenda kuliko! but sometimes mtu unajisikia tu vibaya maana unaona kama unamtwisha mzee wa watu mzigo uso na lazima.
Asa huyu Ex- kama si ubahau nn...... mbwai!! ah
Hapa Mbu kusema ukweli mie nitakuwa mshamba tu ila ninavyoelewa mie haijalishi mmeachanaje linapofikia swala kama hili ni vema kushirikishwa mzazi halisi i.e. biological parent.......tena kwa mie kaka ndo step nitajiweka kando kabisaaa nikisubiri tu nipewe kibwebwe cha kuandaa shughuli but maamuzi ya kila itakavyokuwa yafanywe na wazai wake halisi......nitaingilia tu pale nitakapoombwa kufanya hivyo otherwise mie nitabakia mtekelezaji
Na siku ya sherehe, Ukumbini nitaomba niwe naserve 'High Table' huku Mr na Ex wake wawe wamekaa pale pa wazazi........Unless niitwe kutambulishwa LOL.
lol....hhahhahhaha....asalaaale, Mwj1 nimekuelewa mahbouba,...lol...
eti whaaaat? agawiwe nanihii ndio atoe ada ya wanawe? huyo kadata|!
Well, kwa issue hii sasa akili inaniingia nifuate muongozo wa Spouse jinsi anavyo deal na Ex-wake,
maana kujitia 'kichwa cha nyumba' hapa naweza jikuta naharibu kuliko kurekebisha nyufa,
Lohhh,...nakushukuru Mwj1 kwa darasa hili...
...Enheee, hapa ndio napataka.
Iweje wewe mama mzazi uliyemlea binti mfano ana 2-3 years, ukahangaika nae kwa uzima na ugonjwa, mpaka binti kavunja ungo, kamaliza madarasa na leo anaolewa halafu eti shughuli ya kuozesha isiwe yako? Huyo mama/baba mzazi aliyemtelekeza/kunyang'anywa mtoto ananafasi gani kwenye shughuli hiyo kama sio 'mgeni mwalikwa' tu kwasababu za ki itifaki? Nishayashuhudia haya, msinibishie.
Kwa upande wa kijana wa kiume ni hivyo hivyo, mama mlezi kwenye scenario ya hapo juu inaingiliana vile vile.
Hapana, naamini mama na baba mlezi wana nafasi kubwa kwenye kuamua shughuli nzito kama hiyo, hata panapotokea msiba.
Haya mambo kiukweli si ya kupuuzwa, maana kila siku ya mwenyezi mungu kuna jipya linalozuka kugombea uhalali wa mtoto.
Kuna watu walifikia hata kugombea maiti!
.........Hapo sasa Mbu mzazi ni mzazi, mie nilishuhudia dadangu alipoolewa, mamake alikuwa Mgeni rasmi haswaaa tena mgeni rasmi asiyecheka wala kutabasamu!! nilimwelewa kwani nafsi ilikuwa inamsuta maana yeye alimkimbia (wakimia maana walikuwa watatu) akenda kwa mwenye pesa (ndivyo tulivyoambiwaga). But kuna ile ya mmama amenyang'anywa watoto wakingali wachanga...huyo ukisema umzuie kushiriki kwenye shughuli ya mtoto wake utakuwa unamuonea kupita kiasi! Maana sometimes bana inabidi mtu uchunguze authenticity ya 'stori' ulopewa.
Kuna mkaka mmoja alilelewa na Baba wa Kambo!! iakaambiwa kuwa Babake alikwendaoa mzungu akamtelekeza mama mtu huko Unyakyusani. Wakati wa arusi kijana kakomaa anamtaka babake aje arusini, watu wakamwambia ni haki yake, wakaafiki.........ikaanza saka baba yangu, saka baba yangu, Mbeya hayupo, Dar hayupo.........akaenda Arusha akampata!, kumbe ni Babake Mkubwa!! Yaani Mama alizaa na shemeji mkubwa na ndo ikawa chanzo cha talaka!