Malezi...Step Parenting.


...lol...astaghafirullah,....hhhahhahaa, hebu nikalale mie, wewe ushaanza hadithi zitazoniletea ndoto mbaya leo.
Baba mkubwa na u step dada wapi na wapi? ha hahhahah...haya bana.
Hiyo kesi hata kwenye malezi ni utata mtupu!
 

lol...haya mambo yanastahiki busara kubwa sana...tatizo kizazi cha sasa utasikia mingong'ono ya kumsuta mzee wa watu hapo hapo harusini mpaka wakwe wanatambua kulikoni. Ni aibu sana. Ndio maana nasisitiza mambo haya ni bora yakaanzia kusimamiwa tangu vijana wadogo kabisa, ili kuja epuka aibu huko mbele ya safari.
 
Mbu, Ahsante sana kwa mada hii inayogusa maisha halisi ambayo wengi wetu tumepitia au ndio tunapitia kwa sasa. Nimependa sana michango iliyotolewa hapo juu.

Kwa mtazamo wangu. Wazazi tuna sehemu kubwa na ya pekee katika maisha ya Step-children. Sisi ndio tunaweza kujenga au kubomoa maisha ya watoto hao. Msingi wa yote unaanza pale (a) tunapoweza au kushindwa kuainisha na ku – document makubaliano ya kuvunja mahusiano na pia (b) Ni kwa jinsi gani au kwa mapenzi gani tunaingia katika mahusiano mapya yaani upeo wa mapenzi mapya unaishia kwa mama au unafika hadi kwa mtoto?

Kama tuta – assume wazazi wa zamani wamefuata taratibu zote za kisheria na kuweka bayana mipaka, haki na uwajibikaji (responsibilities za malezi) basi maisha mapya ya mtoto yatategemea wigo wa mapenzi ya baba au Mama mpya. Yaani kama Step-parent utakuwa na upendo wa kweli na sio unafiki basi malezi ya mtoto yatakuwa sawa na mtoto wako wa kibailojia. Kuna wazazi wengi waliofanikiwa kwa hili na kuna wale walioshindwa hasa kutokana na msukumo mbaya wa jamii eti " mtoto wa kambo si damu yako" hii ni dhana potofu na ya kizandiki kwani jamii inashindwa kujua hata yule unayefikiria kuwa ni mtoto wako wa kibailojia anaweza kuwa si wa kwako bali ni wa jirani yako.

Malezi ya mtoto yanategemea na mambo mengi. Umri wa mtoto unaweza kuchangia, mtoto mdogo chini ya miaka 3 akili yake ni rahisi kukubali yeyote kuwa mzazi. Kati ya miaka 4 hadi 7 atauliza kidogo then atakubaliana na lolote. Miaka 8 hadi 14 itabidi mzazi ueleze sababu za mabadiliko. Zaidi ya miaka 14 wazazi inabidi wamwage sera za nguvu. Lakini kumbuka kikubwa ni kukubalika kwako kama mzazi (step-parent) kunatokana na kujitoa kwako muhanga na kuwa kama mzazi asilia wa mtoto kwa 110% ukiweza hili mtoto hatoweza kukusahau hadi kufa na ukishindwa hili, mtoto atakusahau muda mfupi tu akiweza kujitegemea.

Nafasi ya biological parents: Hapa tun- assume active parent yaani yule mwenye uchungu wa kweli na makuzi ya mtoto na sio yule ambaye anajifanya kumpenda mtoto ili kumsumbua Ex parent mwenzake. Nafasi ya biological parent inategemeana na masuala na haki za kisheria. Kwa wenzetu waliondelea wanaweka bayana mambo kisheria na kuhakikisha mtoto anakuwa kwa amani. Huku kwetu uswazi tunaachana tu bila hata kuandikishana motekeo yake ni usumbufu ambao unaingilia hadi maisha ya mtoto.

Athari za dini, kipato, mila na desturi zinaingia kwa yale niyosema hapo juu. Kama umejitoa muhanga na kwa vitendo kujali na ku-care maisha ya step child basi mzazi mwenza atakupenda na atakuheshimu kwa hilo; mtaweka mipango na makubaliano ya familia nzima; mzazi mwenza atakubali ufukara wako na juhudi zako za kutaka maendeleo ya mtoto ndani ya uwezo wako. Lakini usisahau issue za dini na mila Dini zinaweza kutegemea makubaliano ya kisheria na Biological-parent lakini mtoto anaweza ku-veto akiwa mkubwa.

Anyway, kikubwa wazazi wakati wanaachana inabidi wafikirie malezi ya baadaye ya watoto. Watoto wadogo hawajui sheria, watoto watamkubali yeyote ambaye atakuwa mlinzi na msimamizi wao awe biological parent au step parent...

Jamani kabla ya kuachana tusikimbilie kugombania nguo, magari, na viwanja. Tugombanie hati za kisheria, haki na mipango ya malezi ya mtoto. Tupoteze muda kwa kukimbizana na wanasheria..hayo yatalipa huko mbele

Nawasilisha..
 

Linapokuja suala la binti anataka kuchumbiwa, JE? zile taratibu zetu za kupeleka posa sijui ndio kifunga uchumba,
mahari nakadhalika, Je?....hapa napo pakoje?
!

IMO... Linapokuja swala la binti kutaka kuchumbiwa ni bara biological parent (hata kama hayupo katika maisha yenu) ahusishwe kwa kuambiwa exactly what is happenning kuhusu huyo binti yake na yeye aamua kama anataka kuplay part (kwa kushirikishwa tu!) katika the whole process au lah! For at the end of the day hata kama unamchukia ex wako kwa chuki ya level yoyote ile; haifai kumhusisha mtoto hiyo chuki, na ni muhimu daima yule mtoto in question ajenge katika kichwa chake kua ingawa huyo mzazi ni dhaifu.... s/he is responsible kwa kuzaliwa kwake - thus owes him/her one...


Watafutwe ili washirikishwe ndugu na jamaa wa mke, au haya mambo yeshapitwa na wakati? Sidhani kama ni jambo la ajabu kuona siku ya harusi hata mama mlezi anapewa tuza zake kwa kumlea vyema mtoto japo mzazi wake yupo!


Mbu in your own coloured words kweli sio ajabu kabisa!! But haipendezi for sometimes busara katika maamuzi kama haya ni muhimu mno... for unapoonesha dharau za wazi za mzazi mwenzako mpaka mtoto akajua hilo na kuishia ku stick upande wa mzazi mmoja.... sio kwamba unamkomoa yule mzazi mwenzio.... bali unamjengea msingi wa mtoto wako kua na dharau iso kithiri... for kama aweza mdharau alo mzaa... nini kitamzuia kumdharau mwanadamu wa kawaida?? haipendezi... inatakiwa mtoto ajenge dharau ya mzazi alomtelekeza using his/her own judgement tokana na matendo ya huyo mzazi - but still ni marufuku kudharau!! Mfano; mimi na ex haviivi kabisa... but mwanangu haruhusiwi kudharau madhaifu ya babake for once i loved that man.... he is not completely inhuman, na wala mwanangu hayamhusu!!

In green katika mila na desturi zetu wazazi wawepo wasiwepo lazima wanandugu wanahusishwa... in most cases...
 
Reactions: Mbu



Hapo mimi ndio hushangaa hawa wanaume... kakuacha wewe anaacha na wanae... cha ajabu anaenda oa mwanamke mwingine mwenye watoto na kuanza kulea watoto sio wake (which is not bad kama he is doing the same to his kids..); wapi na wapi tusha talakiana anataka kuja maliza gunge zake kwako ndo atimize majukumu ya wanawe?? Khaaa!! Hata kama una hamu vipi yayeyuka....
 
Reactions: Mbu


Tulizo... i love the whole post na insight umetoa... i wish i had more time to get into it (but will be back) and i wish kila mzazi angeweza soma hapa.... hasa hizo words in red.... Zaonekana kama simple na yooote yako black and white... but bana zile shades in grey huweza haribu mtiriko woote wa future ya mtoto...

BTW was used to your prev avatar... sasa inabidi niget used to this... kidogo nikusahau...lol.. but your post and name did the trick!
 
I wish Tulizo angekuja kwenye huu ulimwengu tuliopo kabla ya kuongea hilo.
Watu wnapotengana sidhani kama kuna anayewaza mustakabali wa wale watoto watatunzwaje na wataishi vipi. Na je huko wanakoenda wana maisha gani. Na je in case yule mama akaolewa au yule baba ambaye amebaki na watoto akaoa je maisha ya wale watoto na matunzo yao yakoje.
Watu wanawaza mengine kabisa ya mali na mgawanyo wake bila kufikiria wale watoto. Ni wazazi wachache sana wanaoenda kuomba custody ya mtoto au kuwaombea watoto maisha. (Niko off topic ila nayo ni katika kufikiria watoto ambao wanajikuta wazazi wao wametengana na wanaingia kwenye maisha mapya)
 
Reactions: Mbu
I wish Tulizo angekuja kwenye huu ulimwengu tuliopo kabla ya kuongea hilo.

Mkuu, Tulizo haitaji kuja kwenye huo ulimwengu kwani amekulia kwenye huo ulimwengu.

Binafsi, Kuna mengi mabaya ambayo nayakumbuka hadi sasa, nami nimeapa kuwa nitafanya kila lililo ndani ya uwezo wangu kuepusha watoto wangu kuingia kwenye maisha kama haya ya wazazi wa kambo wasio thamini viumbe wengine ..Hebu fikiri unalelewa na mzazi wa kambo ambaye yuko tayari kuzima Jiko la kupikia, kumnunulia chips mtoto wake na kuacha watoto wengine wakiangalia kwa uchungu au kusubiri kurushiwa vipande vya mabaki na mdogo wao kama mbwa uliza kisa ...baba yao kasahau kuacha hela ya chakula na Mama wa kambo ingawa anayo hela lakini hawezi kuchezea hela yake kulisha watoto wa mtu mwingine.

Picha kama hii inaweza kukaa akilini hadi unakufa.. na inarudi kila unaposoma thread kama hizi..

My apologies..a bit out of topic..
 
Tulizo nakupata mkuu na inauma na hilo ndio tatizo la watoto wengi wanaojikuta katika mazingira hayo na wakikutana na wale wamama au wababa ambao wanatumia lile jina kuwa ni wa kambo.

Mshukuru Mungu na muombe sana kuishi kuona watoto wako wanaishi the way unavyotaka wasije kuishia ambako watakuwa wa kambo
 

asante BAK.... mie mwanzoni nilikuwa najiuliza naanzia wapi malezi na huyu binti yangu, ictoshe alikuwa ametoka kwenye malezi ya mama yake mzazi sasa naanzia wapi, hapo bado nilikuwa cna mtoto, nilikuwa namlea kwa hofu kweli ndugu wa mama yake walisema mengi, nitawezaje wakati mie bado cjui uchungu wa mtoto cjui nn na nn, lakini nilifanikiwa kwa msaada wa msukuma, ndio mana nasemaga binti yangu wa kwanza, huwezi kujua kabisa kama sio wangu, tunaenda sawa sana mpaka raha......
 

hapo ndio kuna ule usemi wa kiswahili ukipenda boga.....mie niliemkuta kama ninaemlea sasa cna shaka but kwa sasa aniletee mtoto chini wa umri wa mwanangu wa mwisho hiyo atanisamehe, sioni sababu ya mwanamke kukataa mtoto wa mume wake aliemkuta, hapo hakuna upendo kabisa kabisa.
 

kwenye malezi kama haya kuna wakati mnatakiwa muweke tofauti zenu kando, ndio kama hapo! hayo ni mambo ya kushirikiana kati ya baba na mama mzazi, kwa upande wangu japo binti yangu mama yake alifariki lakini tukifikia huko nitaomba muongoza wa mama zake wakubwa/wadogo......
 
Reactions: Mbu

Mbu....sio wote wametelekezwa/wamenyang'anywa watoto, kuna wale waliofanya makubaliano japo wametangana na kuamua mtoto akae na mama/baba yake, kwenye hili kwann asishirikishwe mama/baba mzazi wa mtoto? kwangu haipendezi kukaa high table natambulishwa kaka mama wakati mama mzazi wa mtoto yupo ukumbini kama mgeni mwalikwa, kumtunza nimemtunza but mama mzazi pia ana haki juu ya mwanae.
 
Reactions: Mbu
MJ1....leo unanimwagia vimbwanga nachoka mwenyewe, imeniacha hoi ya namsaka baba yangu...maisha haya jamani.
 
Reactions: Mbu

Tulizo pole sana, wamama kama hao ndio wnatufanya wa mama walezi tuchukuliwe kama vile tuna mateso/manyanyaso kwa hawa watoto wetu wa kufikia, huwa naogopa sana kumtendea huyu mtoto baya, kuna leo na kesho na kameshakuwa kabinti kakubwa kataniangalizia wadogo zake kwa moyo kama mie ninavyomlea kwa moyo, imagine mama mwenye kujua uchungu kweli wa mtoto unafanya hivyo? Mungu anisaiodie kwa kweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…