Malezi...Step Parenting.


...mara nyingi wanaume kama hao hudhani eti kwa kufanya hivyo anamkomoa Ex wife wake. Ujinga mtupu!



..nawasifu kina mama katika hili, ni mahodari sana kusamehe kila kilichomo ili wabakie na mtoto/watoto wao.



...dahh, mkuu Tulizo pole sana kwa kupitia hayo, wala hujaenda off topik...haya ndio tunayoyazungumzia hapa.
Inauma sana kwakweli.



...naaam, ndivyo ilivyo. Naamini kwa ushirikiano utaopewa na mama/baba mzazi wa huyo mtoto unaweza mlea vizuri sana mtoto kwani mzazi ndiye anayejua mengi tangu huko walikotokea. Tatizo ni pale mzazi asipokupa ushirikiano kwenye malezi ya mwanae,...yaani sawa na yule anayekwambia achana nae huyu ana mama yake!...wanaume wengi wana kaujinga hako kwa kudhani anampendezesha mkewe kumbe anapenyeza mianya ya mtoto kuteseka.



...japo inauma hiyo scenario, lakini je? Vipi iwapo mama mtoto huyo alifariki wakati wakujifungua? au alimtelekeza mtoto mlangoni kwa baba yake akatoweka? ...najua kuna ugumu sana wa ulezi huo lakini bado nataka kuamini unao moyo wa huruma kwa huyo malaika asiye na kosa maskini.
 
Mbu nakubaliana na wewe wanawake wengi wako tayari kusucrifice kila kitu wahakikishe kuwa watoto wao wanabakia na malezi na maisha mema. Na wengi wako tayari waache kila kitu katika mikono ya waliotengana nao ila tuu wahakikishiwe usalama wa watoto wao kuliko kung'ang'ania mali
 
....wamama kama hao ndio wnatufanya wa mama walezi tuchukuliwe kama vile tuna mateso/manyanyaso kwa hawa watoto wetu wa kufikia......

Ni kweli sio kina mama wote wana tabia mbaya..lakini pia wale wachache wanaharibu sifa na heshima ya mama.

Lakini kwa upande wa pili..tusiwalaumu moja kwa moja kina mama na kuwaacha kina baba. Kwani kabla hujategemea kupata yule Mama kambo ambaye ana roho ya upendo toka kuzaliwa basi jaribu kulazimisha na kuweka wazi unategemea nini toka kwenye mahusiano ili kama mama mgeni hawezi kulea basi aachie ngazi na kazi ya kutafuta mwingine iendelee.. na kama atajifanya anaweza halafu baadaye anabadilika..basi ajue mlango uko wazi..Yaani ukipenda boga unapenda na ua lake.. Naamini Baba ukiwa na msimamo..hivi vitu vitapungua..
 
Hilo la kukataa kulea watoto wa kuwazaa na kwenda kulea watoto wa kufikia ni tabia ya mababa wengi. Ndio maana kuna siku nilisema mapenzi ya wababa wengi kwa watoto ni very conditional; wengi wakimchukia mama yao basi wanachukia na watoto pia; si wote lakini.

Kuna mama mmoja mtu mzima ni rafiki yangu alinisimulia story ya maisha yake iliniuma sana. Mme wake aliamia kwa shangingi la mujini na kumtelekeza yeye na watoto wake wanne. Mume alikuwa na pesa kweli kweli lakini hakuwa anasomesha watoto wake bali alipeleka watoto wawili wa hilo shangingi nje kusoma na siyo wake. Huyu mama alinambia NK nachoshukuru mume wangu hakuuza majumba yetu wala hakunifukuza ndani; aliama yeye, sisi maisha yaliendelea kama kawa.

Mama alijipinda na ndugu zake huyu mama wana uwezo sana hivyo walikuwa wanampa support na kazi yake haikuwa mbaya; watoto wake wote wamesoma sasa wengine ni medical doctors, last born yuko versity kawasomesha mwenyewe.

Baba alirudi home anapiga magoti after so many years akiwa mgonjwa hoi. Mke alimsamehe kwa kuwa hakuolewa alinambia yeye alishakuwa mtu mzima hakuona sababu ya kuolewa aliamua kulea watoto wake. Kwa kifupi baba keshakufa. Huyu mama anasema nilimsamehe sababu ya watoto ila mahusiano ya ngono hakukubali kama mjuavyo tena.

Huyu mama ni mchesi sana na nampenda kwani ana ushauri mzuri sana wa maisha ya ndoa. Uvumilivu ni mzuri sana. Na yeye kama si kunisimulia nisingejua kama aliwahi pata shida maishani; ni kati ya wale wamama ambao hata vijana wanamuuliza ulipokuwa kijana ulikuwaje mama maana ni mtu wa fashion balaa. Raha anajipa mwenyewe.


 
Mbu....hapo bado nashikilia mcmamo wangu kwamba hapana, nilienae ananitosha au kama kulikuwaga na mkubwa wake au mdogo wake kabla ya wangu nitampokea kwa mikono miwili, huyo chini ya umri wa mwanangu babake amfanyie malezi yake anayoyajua, kujua kuwa mtoto mahali haitanijalisha sana lakini sio azae huko aniletee nimlee...big no!
 
Mkuu unajua mambo mengi yanafanyika wababa wakiwa wako either kazini au kwenye mizunguko.
Inawezekana baba akiwepo home mama anawatreat watoto wote sawa ila akigeuza tuu mgongo mama anaanza vibweka vyake.
So ni mara chache sana unamkuta baba anamtesa mtoto ambaye sio wake.
 


nikifikiaga hapo huwa nasema kwa Mungu mtu ackose mama jamani......nina kijana wa mama yangu mdogo, mamake alifariki akiwa form 4, ni tabu tupu, baba hajali, japo ni kijana huyo 1 tu lakini yupo radhi akeshe bar but ameshindwa kumuendeleza mtoto wake kimasomo, imebidi tuingie jukumu la kumsomesha, wakati wa uhai wa mama yake kijana alikuwa anapata kila kila atakacho kwamba ni huyo mmoja bac aliwekeza kwake kwa kila kitu, leo baba anavuruga kila kitu...kweli mtoto ackose mama jamani.
 
Tulizo kuna watu wana theory kuwa ukioa/olewa na binti/kaka aliyetoka broken home/family kuna chance kubwa ndoa yenu isidumu. Mimi nina wazo tofauti. Watu wengi waliopitia malezi ya single parent au wazazi wa kambo huwa na bidii sana kustawisha familia zao kwani wanajua through experience madhara ya broken home. Yani kuna watu wanasema kabisa mimi nimelelewa na mama/baba kambo kwa mateso sitakubali kamwe wanangu wapitie shida nilizopata.

Afu mababa wengi huwa hawajuhi what their kids are going through maana kama tujuavyo wengi kurudi ni usiku mwingi, na watoto wengi wanaogopa kukaa na baba zao kuwaambia shida zao. Tuombe Mungu jamani kuna binadamu wana roho za kikatili si wote lakini.
 
Mwenye roho nzuri na mbaya unadhani ni rahisi kumjua kabla hajaingia ndani?? Watu wana mitihani. Unakuta baba anajua kabisa wife anatesa wanangu ila anachanganyikiwa kwani si rahisi kumwacha kwa kuwa labda tayari wameshazaa. Atamwacha aoe mwingine mambo yawe yale yale. Kuna watu wana majaribu duniani. Wengi wanaanza kutesa watoto wa kambo baada ya kuzaa wao. Wangeanza mateso mapema mbona wangeachika issue utamwacha naye watoto wake waingie kwenye chain ile ile.
 

...inasikitisha sana lakini ndivyo ilivyo. Malipo mengine ni hapa hapa duniani.
Hata wale watoto ambao waliteseka sana kwa wa mama wa Kambo ndio hao hao wanaokuja
kuwasitiri mama zao hao wa Kambo, au step bros/sisters wao....it's a KARMA..(What goes around comes around!)

Hatusomi, hatujifunzi wala kuyaelewa haya mpaka yatufike. Kwanini?


...lol, haya. Nadhani Bwana Mkubwa anajua wapi anasimamia katika hili, madhali anajua wapi pa kupeleka majeruhi wa ajali hiyo ikitokea yote salama. Mw'Mungu ayapitishilie mbali kwakweli.

Kuna mzee mmoja yeye alipokumbwa na ajali kama hii, na kwakuwa mama mazazi alifariki wakati wa kujifungua...akaamua 'kufunika kombe' na kumtelekeza mtoto huko kijijini kwa mama wa mzazi mwenziwe (marehemu) Akaendelea maisha yake na mkewe na wanawe raha mustarehe na biashara zake.

Kijana hakubahatika kusoma vizuri, aliishia la saba...akaishia kutumikishwa kazi za kulima, ufugaji kwa ujira mdogo huko kijijini. Kimbembe kimekuja siku mzee wa watu amefariki...kijana kaletwa msibani kutoa last repects na wanandugu wamjue. Msiba ukageuka kipindi cha "mikingamo!"



...Upendo ni kitu muhimu sana. Utapokuwa na upendo na wanao kiasi cha kuwa wawazi, haijalishi utakuwa nyumbani au la watakuambia yale yaliyo na kero kwao. Muhimu ni ile trust unaowajengea tangu wakiwa wadogo kuweza ku share kinachoendelea maishani mwao. Nadhani hiyo Bond hata aje mama/baba wa kambo wa aina gani hawezi kuivunja.
 

Umesema kweli..tena ungeendelea mbele na kusema..chanzo cha misekule (refer Thread ya Mbu 'Msekule' ) ya kujitakia ni mambo kama haya.. yaani una watoto watatu kwenye ndoa.. lakini wewe binafsi umelelewa kwenye dhiki ya wazazi wa kambo..halafu ndani ya ndoa yako kuna rabsha ndogo ndogo. Basi unakaa na ukifikiri kama ukiondoka watoto wako watapata shida kama ile uliyopata..hivyo una amua na kuona ni heri wewe mzazi uendelee kuwa msekule ili watoto wasionje yale maisha uliyoishi..Just an example.
 
This post umeeandika imenigusa! Imeniumiza! for najua ni kweli, nimeshuhudia.... nimeona.... na bado haya mambo yanaendelea...


The above ni kweli sio woote, but ni majority... hili suala kaka/baba zetu inabidi waliangalie na kulitafakari kwa ukaribu.... Inasikitisha mno!! Sijui inakuwaje kwa kweli kutelekeza watoto... inauma... inauma saana hasa ukizingatia ana uwezo wa kulea na kusomesha watoto na kuwajengea maisha bora na ya kisasa, bora hata kama hana uwezo waweza sema kashindwa....


Hio experience umetoa hapo juu... inasikitisha mno, but kutoa the reality ya jinsi wanawake wanavo pata majaribu toka kwa waume zao... Ni ajabu saana hata kwanini baadhi ya wanaume wanadharau wanawake na kuwaona viumbe dhaifu, hali huweza simama in most straining and complicated experiences... hilo hapo juu fanya wewe mwanamke alafu ujifanye unataka kurudi kwa huyo mumeo wa zamani.... unaweza fukuzwa kama mbwa!!

Hata hivo saizi wanawake weengi wa kizazi cha sasa wamebadilika na huo ujinga hawa condone... labda huko vijijini lakini sio dada wa mjini (thou kuna exceptions) kwamba umtelekeze alafu urudi kuuguzwa ili ufe in dignity within your family?? She wont give you hio nafasi... however mimi ni mwanamke but one thing is for sure... I know we are the most complicated beings on earth... waweza kuta mwanamke roho mbaya no mfano, but sometimes she does something even you as a woman would not understand..... Dah! Maisha haya....
 
Sijui kwanini watu huwa wazito kulea watoto wa kambo. Wengine kuonesha chuki za wazi wazi.
Ila tunaweza kulaumu wazazi wa kambo kumbe na watoto wenyewe hasa wale wanaojitambua ndio chanzo cha chuki kwa wazazi wao wa kufikia.
Tofauti za mila na desturi zina athari hasa kwa watoto ambao bado hawajajitambua kwa wale wanaojitambua ni rahisi kujua upande upi ni sahihi kwao na kuamua kushikilia hapo hapo.
 
Reactions: Mbu
mbu mwanao mzuri sana tayarisha mbwa

I wish!!!...

...hukumbuki 'sredi' yangu ya kutafuta mtoto wa kike? ...panapo majaaliwa!
Tayari na Boys from my previous marriage,....Soulmate naye ana ka Prince
ka nguvu.

Tumo mbioni kukamilisha mambo halafu tuanze mchakato wa kutafuta Princess
[I'm sure atakuwa mzuri kama mama'ke] kwa hisani ya Doctor Shafiq...

...unless kuna wajuzi humu mtoto wa kike anapatikanaje! Otherwise,
maisha yan'kwenda vizuri mpaka sasa, ALHAMDULILLAH.
 
Mbu hebu fafanua vizuri hapo nimeacha njia panda sielewi au lugha ngumu hapo sijui
 

Mbu hongera sana.........kuna mdada mmoja jamani nilikutana naye some kama nakumbuka vizuri mwezi June mwishoni. She said kuwa anatoa njia ya namna ya kupata mtoto umtakaye na hiyo formula yake ilishatestiwa KCMC kama sikosei na ikaprove 98%. Alinipaga namba yake nafikiri.
 

Husninyo yaani inashangaza sana kusema ukweli. Ila mie nilipataga experience ya ajabu sana but nadhani baadae nilikuja kuelewa kuwa inawezekana inatokana na uwoga ulioathiriwa na hizi hisia. My Ex had a baby way long , na hata tulipokutana alikuwa anaogopa kusema but after knowning ikaanza safari ndefu ya kumshawishi amchukue (she was living na bibiake mzaa mama kijijii since her mum was married na anaishi nje ya nchi)....It wasnt easy kumconvince so mwisho tukakubaliana ampeleke Boarding........... uamuzi ambao nlikujaujutia. But am glad kwa mchango nlotoa.
 

Ni kweli Mr. Rocky yaani katika mbinu watumiazo wanawake wanaowanyanyasa watoto wa kufikia ni hii......yaani baba akiwepo nyumbani utashangaa mama anawakumbatia kabisa watoto wa kambo wakati akiwa hayupo hata kukaa nao sebuleni au meza moja hawezi!! Ukimpata mwanamke mwenye roho mbaya utajuta.

Kuna mmama mmoja yeye hakuwa na watoto wa kambo but akitembelewa na watoto wa mawifi/shemeji unaona kabisa anawaweka kundi moja na mfanyakazi wake wa ndani- yaani ni marufuku kula chochote bila idhini yake. Mmatunda mpaka yanaozea kwenye fridge, mkitengeneza juice kila akirudi anaikagua kisha anasema mmekunywa mkaongezea maji!! nyama anakata anahesabu, ikifika wakati wa kula kama hayupo mnakula na mchuzi vipande vyenu mtavipata kesho asubuhi na chai!! (Well iikuwa ni utaratibu wa nyumbani kwake - alikuwa na haki) But mtu kama huyo najaribu kufikiria umpeleke mtoto wa kambo hapo!!

Cha muhimu tu ni kuwa baba awe karibu na wanae/hata kama anaamini kuwa mkewe wa sasa ni malaika kwa roho nzuri; at least kwa siku za mwanzo ni vema akawa makini angalau kuwajengea hao wanae confidence ya kuweza kumwambia chochote kile hata kama wanaonewa. Maana watoto wengine hujikuta njia panda baada ya kuona na baba yao naye amewasaliti.

Kwa wale wababa ambao watoto wao wanaishi na Ex- wao wasiwe confortable kuwa ni mama yao then atawatreat vizuri kumbukeni bado kuna wamama ambao wako tayari kutesa watoto wao kwa penzi jipya........msishangae!!
 
Tatizo wewe hunywi pombe, ungekuwa mnywaji simple tu hahahaaa, nasikia mtoto wa kike unafanya mapenzi siku moja kabla ya siku za denja, ili yale ya kiume yafe zibaki zile mbegu za kike tu, coz za kiume huwa zinakufa faster na za kike huwa zinaweza kaa hata 72 hrs, sasa kwa shafiq inabidi ujichue then aziweke kwa soulmate, kwa hiyo na yeye atakuwa ameshiriki kwenye tendo la ndoa hahahaaaaa mnakuwa mababa wawili, yaani wewe na shafiq, teheeee just joking mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…