Malezi malezi malezi....
Umri wa mimba ni miezi 9
Mtoto akizaliwa anajaliwa sana na jamii anafurahiwa kwa kuletewa zawadi na kuangaliwa kwa makini asipate magonjwa. Akishatimiza miaka 2 kama si mwaka 1, sio mama, baba wala jamii wenye muda na mtoto. Wengi wa watoto kuanzia hapo hata mlo wao hauzingatiwi tena, wanalishwa mlo kama wa wakubwa wali harage ugali nyama mchicha.
Hiyo inaendelea hadi mtoto anapoanza shule wazazi/walezi wanaachia mahausigeli/ walimu/bodaboda ndo walee watoto huku wazazi wanajua wanachokifanya.
Jana nilikuwa nyumba ya ibada, mhubiri alofundisha kuhusu familia....
Kwamba uharibifu wote wa wanadamu tunaouona kwenye jamii unaanzia kwenye familia.
Wezi, mashoga, wasagaji, wala rushwa, matapeli n.k. Wote wanaanzia kwenye ngazi ya familia.
Kama alivyosema mtoa mada, malezi ya mtoto ni jukumu la baba na mama, iwapo mmoja wa wazazi ametwaliwa basi aliyebaki anasaidiana na ndugu wa upande wa baba na mama kulea mtoto hadi awe raia mwema mwenye kujitambua na kufata miiko ya dini, jamii na familia kwa ujumla.
Kulea sio kazi ndogo, waswahili walisema kuzaa si kazi kazi kulea mwana.....
Wengi wa wazazi sikuhizi ni wavivu
Hawafanyi majukumu yao ipasavyo
Kwa ambao hamjazaa bado, usizae kama hauko tayari kutumika kwa ajili ya mtoto wako, iwe mwanamke au mwanaume. Malezi yanahitaji muda na kujitoa, uwepo wa mzazi kwa mtoto unahitajika kwa asilimia 100 bila kukabidhi majukumu hayo kwa mtu mwingine.
Kumbuka kuzaa unashiriki uumbaji wa Mungu.
Na mzazi ni kioo cha kwanza cha mtoto namna anaona natakiwa niishi, vile unataka mtoto wako awe, ishi maisha hayo.
Huwezi kiwa unataka mwanao awe anawahi kurudi nyumbani mara moja atokapo shule wakati wewe ukitoka kazini una konakona kibao unapita kabla hujafika nyumbani, mtoto atakuiga tuu.
Iwapo wewe si mkweli kwenye maneno au ahadi unazozitoa, mtoto wako nae atakuiga tuu kutoa ahadi za uongo.
Huendi/hushiriki nyumba za ibada, mwanao nae hatoshiriki.
Hutembelei ndugu au husaidii wasiojiweza mwanao nae atapita mulemule unakopita...
Kubwa kuliko....
Unaingiza milupo nyumbani kwako ukijua mkeo/mumeo hajui ila mwanao anaona ..... its Karma, atakuja kuyaishi hayo unayoyaishi nyumbani mwako.
Kulala na house girl/house boy au kutembea na mke/mume wa jirani.... mwanao anaona na yeye atakuja fanya hayo unayofanya ukifikiri haoni au hajui...
Kama wazazi mlikuwa hamjui, ukishakuwa na mtoto, hauko huru tena, yakupasa uishi maisha ya mfano hasa kwa mtoto wako ili awe wa kujielewa na kujitambua.
Swala jingine dogo tuu, huwezi kutaka mwanao awe anazingatia muda wakati wewe kila mahala unachelewa na anaona...
Kanisani mnachelewa, hospitali mnachelewa, kazini unachelewa, kwenye vikao vya familia unachelewa, kwenye sherehe unachelewa... nakwambia mtoto wako atapita mulemule.
Na kama haitoshi, ukisema bwana eeeh mo nshazaa acha akue atajijua mwenyewe maisha yake mie mwenyewe sikulelewa kwa maadili, atakuja kukutana na mke/mume ambae nae maadili mabovu kila siku kesi....
There’s no free lunch, kika kitu kizuri kinagharamiwa.
Wekeza muda kwa mtoto wako, badili mienendo yako ili mtoto wako nae aenende kama wewe, mentor wa kwanza wa mtoto ni mzazi/mlezi.
Ukiona hivyo vyote ni ngumu, unapofanya ngono kumbuka kumwaga nje, ngonoka siku ambazo si za hatari, tumia condom, acha kuendekeza nyege saa nyingine zipuuzie ili uishi maisha unayoyataka bila kubugudhiwa kuishi namna ya maisha kwa ajili ya mtoto wako.
NB: ITS EASLY SAID THAN DONE...👍🏼
Kasinde Mahaba.