Malezi ya sasa bado siyaelewi

Malezi ya sasa bado siyaelewi

Malezi malezi malezi....

Umri wa mimba ni miezi 9

Mtoto akizaliwa anajaliwa sana na jamii anafurahiwa kwa kuletewa zawadi na kuangaliwa kwa makini asipate magonjwa. Akishatimiza miaka 2 kama si mwaka 1, sio mama, baba wala jamii wenye muda na mtoto. Wengi wa watoto kuanzia hapo hata mlo wao hauzingatiwi tena, wanalishwa mlo kama wa wakubwa wali harage ugali nyama mchicha.

Hiyo inaendelea hadi mtoto anapoanza shule wazazi/walezi wanaachia mahausigeli/ walimu/bodaboda ndo walee watoto huku wazazi wanajua wanachokifanya.

Jana nilikuwa nyumba ya ibada, mhubiri alofundisha kuhusu familia....
Kwamba uharibifu wote wa wanadamu tunaouona kwenye jamii unaanzia kwenye familia.

Wezi, mashoga, wasagaji, wala rushwa, matapeli n.k. Wote wanaanzia kwenye ngazi ya familia.

Kama alivyosema mtoa mada, malezi ya mtoto ni jukumu la baba na mama, iwapo mmoja wa wazazi ametwaliwa basi aliyebaki anasaidiana na ndugu wa upande wa baba na mama kulea mtoto hadi awe raia mwema mwenye kujitambua na kufata miiko ya dini, jamii na familia kwa ujumla.

Kulea sio kazi ndogo, waswahili walisema kuzaa si kazi kazi kulea mwana.....

Wengi wa wazazi sikuhizi ni wavivu

Hawafanyi majukumu yao ipasavyo

Kwa ambao hamjazaa bado, usizae kama hauko tayari kutumika kwa ajili ya mtoto wako, iwe mwanamke au mwanaume. Malezi yanahitaji muda na kujitoa, uwepo wa mzazi kwa mtoto unahitajika kwa asilimia 100 bila kukabidhi majukumu hayo kwa mtu mwingine.

Kumbuka kuzaa unashiriki uumbaji wa Mungu.

Na mzazi ni kioo cha kwanza cha mtoto namna anaona natakiwa niishi, vile unataka mtoto wako awe, ishi maisha hayo.

Huwezi kiwa unataka mwanao awe anawahi kurudi nyumbani mara moja atokapo shule wakati wewe ukitoka kazini una konakona kibao unapita kabla hujafika nyumbani, mtoto atakuiga tuu.

Iwapo wewe si mkweli kwenye maneno au ahadi unazozitoa, mtoto wako nae atakuiga tuu kutoa ahadi za uongo.

Huendi/hushiriki nyumba za ibada, mwanao nae hatoshiriki.

Hutembelei ndugu au husaidii wasiojiweza mwanao nae atapita mulemule unakopita...

Kubwa kuliko....

Unaingiza milupo nyumbani kwako ukijua mkeo/mumeo hajui ila mwanao anaona ..... its Karma, atakuja kuyaishi hayo unayoyaishi nyumbani mwako.

Kulala na house girl/house boy au kutembea na mke/mume wa jirani.... mwanao anaona na yeye atakuja fanya hayo unayofanya ukifikiri haoni au hajui...


Kama wazazi mlikuwa hamjui, ukishakuwa na mtoto, hauko huru tena, yakupasa uishi maisha ya mfano hasa kwa mtoto wako ili awe wa kujielewa na kujitambua.

Swala jingine dogo tuu, huwezi kutaka mwanao awe anazingatia muda wakati wewe kila mahala unachelewa na anaona...

Kanisani mnachelewa, hospitali mnachelewa, kazini unachelewa, kwenye vikao vya familia unachelewa, kwenye sherehe unachelewa... nakwambia mtoto wako atapita mulemule.


Na kama haitoshi, ukisema bwana eeeh mo nshazaa acha akue atajijua mwenyewe maisha yake mie mwenyewe sikulelewa kwa maadili, atakuja kukutana na mke/mume ambae nae maadili mabovu kila siku kesi....

There’s no free lunch, kika kitu kizuri kinagharamiwa.

Wekeza muda kwa mtoto wako, badili mienendo yako ili mtoto wako nae aenende kama wewe, mentor wa kwanza wa mtoto ni mzazi/mlezi.

Ukiona hivyo vyote ni ngumu, unapofanya ngono kumbuka kumwaga nje, ngonoka siku ambazo si za hatari, tumia condom, acha kuendekeza nyege saa nyingine zipuuzie ili uishi maisha unayoyataka bila kubugudhiwa kuishi namna ya maisha kwa ajili ya mtoto wako.

NB: ITS EASLY SAID THAN DONE...[emoji1360]

Kasinde Mahaba.
Kasie Matata[emoji91][emoji91][emoji91][emoji736]
 
kuna mmoja alibeba ujauzito akitamani kupata mtoto wa kike, akaja jifungua wa kiume, basi akawa na mchezo wa kumvisha nguo za kike, anampaka wanja anamvalisha magauni siku naenda namkuta na hiyo hali nikamwambia tu unamfundisha mtoto kuikataa jinsia yake mapema sana, na hizo tabia za kishoga ndio hua zingine zinaanza kwa style hio shukuru hicho ulichoruzukiwa ndicho unacho stahiki
Afadhali wewe umekutana na mfano halisi. Niliposoma uzi, nilipata wazo la mama kutamani mtoto wa kike wakati aliye naye ni wa kiume, ila skuwa na mfano hai.
 
Kuna jamaa alipanga nyumba ninayopanga, pale tuko wanachuo tu kwahiyo tabia hazina tofauti sana. Yeye sasa miezi yake kama minne ya kukaa pale hajawahi kuleta demu, kuongea nae hata kwa simu, kuonesha dalili zozote za kuwa na encounter na mwanamke. Yani wengine tunavusha, usiku tunakaa nje tupunge upepo tuongeale nao, wanatutembelea, ukikaa kidogo unasikia huyu analalamika demu fulani kamfanyaje sijui.

Sasa huyo jamaa yuko busy na wanaume mara wako kwenye photoshoot ya kuvaa suti, mara wamevaa manguo ya kung'aa, nywele katia dawa za kulainisha kama Wahindi. Mimi nina wasiwasi nae na kwa sasa kahamia Sinza kwetu kahama.

Alafu wazazi wanashindwa vipi kuwatambua mbona dalili zinakuwepo. Kuna mmoja nilikuwa naye A level huyo anachonga nyusi na anapaka wanja, ana yale mafuta ya kulainisha na kung'arisha lips. Sasa huyu mzazi wake haoni?

Kuna dogo mwingine O level yeye alikuwa anakaa na wadada pekee. Anajilainisha kwenye kuongea na movements alafu ni "designer" na anapamba mademu wakijiandaa na zile sherehe za shule. Yani asipokuwepo wanalalamika wanaona hawatopendeza wakati dogo mwenyewe alikuwa form 2. Huyu anageuzwa tangu darasa la sita alikosomea uko shule maarufu Mwanza. Sasa wazazi wake hawakuona hobbies za mtoto na lifestyle yake?

Kuna lecturer flani Dodoma nilimsaidia kitu kwenye kuongea nae akanambia nafanana na mwanae. Akanambia ana watoto wanne wote wa kiume, huyo wa mwisho ninaefanana nae walijua ni wa kike wakampa na jina kabla. Akazaliwa wa kiume ila "bahati nzuri lile jina linatumika hata kwa mtoto wa kiume". Alafu akanambia anacheka eti ana tabia chache za kike.

Mzazi unamuita mtoto wa kiume Gift na wahuni wanamuita "Gee"
Hapo labda wa kulaumiwa ni huyo mkufunzi wa Dodoma aliyekuwa na ndoto za kupata mtoto wa kike, asimpate, na inavyoonekana anajaribu kumchukulia wa kiume kama wa kike.
Ila hao wengine, watoto wameshakuwa wakubwa, wanafanya maamuzi yao, kama wazazi, wafanye nini?
Na nyie mnaojiona rijali wa kuingiza wasichana, muwe tayari kulea watoto kama familia na mtakaowapa mimba, la sivyo mtaishia kuwaumba watu wapya wenye tabia unazozipinga.
 
Kinacho nisumbua ni kwanini kizazi hichi kimeshindwa kutoa malezi yaliyo sahihi kwa jinsia sahihi?

Mkuu shida ni utandawazi,,,malezi ya kimagharibi..

Siku hzi malezi ya kimagharibi yametapakaa sana na jamii imeamini ndio malezi sahihi,,, hakuna viboko,, mtoto wa mwenzako siku hizi sio wako kama zamani( ulezi shirikishi,,,umefanya kosa na mtoto wa jirani...mnaadhibiwa wote hukohuko kwa jirani),,,,siku hizi ubinafsi umekuwa mkubwa sana,,, namna ya kulea watoto tunapangiwa n.k.

Single maza wa kitambo wengi unakuta wana misingi ya kiafrika,,,so walivaa uhusika wa Mama na Baba....

Single Maza wa siku hizi wanafikiri kulipa hela na mahitaji pekee ndio majukumu ya Baba.... wamekuwa wa hovyo
 
Back
Top Bottom