Malezi ya sasa bado siyaelewi

Huyo ana Ulimbukeni na ujinga anadhania mtoto ni mdoli unaweza chezea unavyotaka.

Eenh kwaiyo baada ya kumwambia ikaweje?
 
Suala hapa nafikiri ni namna pande zote mbili zinavyoweza kushiriki vyema kwenye kulea na kutunza watoto....

Lakini kwasasa, nguvu inayotumika kuiaminisha jamii kuwa wanawake wanaweza kutekeleza majukumu yote, hii si sawa na ndio mwiba na chanzo cha uharibifu unaoanza kukita mizizi taratibu
 
Zaman hata ukilelewa na mama tu,wajomba na baba wadogo na wakubwa wanakuwa wapo karibu na wew tena wengine walikuwa wanawaomba wanaenda kuishi kwa mjomba au baba mdogo

Ila maisha ya siku hz kila mtu anapambana kivyake,
Tatizo jingine ni kuwa ata wajombo na baba wadogo na wakubwa wa siku hizo hawaaminiki
 
Nilichokifanya nilimkemea kwa ukali kuhusu kitendo husika kwasababu alinidanganya kuwa mtoto alipakwa rangi na watoto wenzie angali ni yeye kafanya hivyo....
Kitendo cha yeye kukudanganya kua mtoto alipakwa rangi na watoto wenzie kina ashiria kua alikua anatambua kua lile ni kosa ila alifanya kwa utashi wake tu.
 
Kwa hiyo mkuu kutoleta mademu geto ni dalili ya ushoga? toa ufafanuzi.

Maana hata mm huwa naona ukakasi sana kupeleka mademu kwenye geto langu tangu niibiwe huwa namalizana nao kitaani huko huko.

Kipindi cha nyuma nilisha vusha demu mmoja usiku tukafanya yetu asubuhi akasepa na mm nikaenda mishe.

Kurudi mida ya saa 2 za usiku sikuamini nilicho kikuta geto lilikuwa limevunjwa na kukomba kila kitu.
Kuja kupeleleza kumbe yule demu ni mafia ana kundi la wahuni.

Na ndio tabia yake kwenda kwenye mageto ya watu kusoma ramani na vitu vilivyomo geto alafu anaenda kukuchoma kwa wahuni wana kuja kukufanyizia.
Yaan yule demu siku nikija kumkamata ama zangu ama zake jinga sana.
 
Malezi malezi malezi....

Umri wa mimba ni miezi 9

Mtoto akizaliwa anajaliwa sana na jamii anafurahiwa kwa kuletewa zawadi na kuangaliwa kwa makini asipate magonjwa. Akishatimiza miaka 2 kama si mwaka 1, sio mama, baba wala jamii wenye muda na mtoto. Wengi wa watoto kuanzia hapo hata mlo wao hauzingatiwi tena, wanalishwa mlo kama wa wakubwa wali harage ugali nyama mchicha.

Hiyo inaendelea hadi mtoto anapoanza shule wazazi/walezi wanaachia mahausigeli/ walimu/bodaboda ndo walee watoto huku wazazi wanajua wanachokifanya.

Jana nilikuwa nyumba ya ibada, mhubiri alofundisha kuhusu familia....
Kwamba uharibifu wote wa wanadamu tunaouona kwenye jamii unaanzia kwenye familia.

Wezi, mashoga, wasagaji, wala rushwa, matapeli n.k. Wote wanaanzia kwenye ngazi ya familia.

Kama alivyosema mtoa mada, malezi ya mtoto ni jukumu la baba na mama, iwapo mmoja wa wazazi ametwaliwa basi aliyebaki anasaidiana na ndugu wa upande wa baba na mama kulea mtoto hadi awe raia mwema mwenye kujitambua na kufata miiko ya dini, jamii na familia kwa ujumla.

Kulea sio kazi ndogo, waswahili walisema kuzaa si kazi kazi kulea mwana.....

Wengi wa wazazi sikuhizi ni wavivu

Hawafanyi majukumu yao ipasavyo

Kwa ambao hamjazaa bado, usizae kama hauko tayari kutumika kwa ajili ya mtoto wako, iwe mwanamke au mwanaume. Malezi yanahitaji muda na kujitoa, uwepo wa mzazi kwa mtoto unahitajika kwa asilimia 100 bila kukabidhi majukumu hayo kwa mtu mwingine.

Kumbuka kuzaa unashiriki uumbaji wa Mungu.

Na mzazi ni kioo cha kwanza cha mtoto namna anaona natakiwa niishi, vile unataka mtoto wako awe, ishi maisha hayo.

Huwezi kiwa unataka mwanao awe anawahi kurudi nyumbani mara moja atokapo shule wakati wewe ukitoka kazini una konakona kibao unapita kabla hujafika nyumbani, mtoto atakuiga tuu.

Iwapo wewe si mkweli kwenye maneno au ahadi unazozitoa, mtoto wako nae atakuiga tuu kutoa ahadi za uongo.

Huendi/hushiriki nyumba za ibada, mwanao nae hatoshiriki.

Hutembelei ndugu au husaidii wasiojiweza mwanao nae atapita mulemule unakopita...

Kubwa kuliko....

Unaingiza milupo nyumbani kwako ukijua mkeo/mumeo hajui ila mwanao anaona ..... its Karma, atakuja kuyaishi hayo unayoyaishi nyumbani mwako.

Kulala na house girl/house boy au kutembea na mke/mume wa jirani.... mwanao anaona na yeye atakuja fanya hayo unayofanya ukifikiri haoni au hajui...


Kama wazazi mlikuwa hamjui, ukishakuwa na mtoto, hauko huru tena, yakupasa uishi maisha ya mfano hasa kwa mtoto wako ili awe wa kujielewa na kujitambua.

Swala jingine dogo tuu, huwezi kutaka mwanao awe anazingatia muda wakati wewe kila mahala unachelewa na anaona...

Kanisani mnachelewa, hospitali mnachelewa, kazini unachelewa, kwenye vikao vya familia unachelewa, kwenye sherehe unachelewa... nakwambia mtoto wako atapita mulemule.


Na kama haitoshi, ukisema bwana eeeh mo nshazaa acha akue atajijua mwenyewe maisha yake mie mwenyewe sikulelewa kwa maadili, atakuja kukutana na mke/mume ambae nae maadili mabovu kila siku kesi....

There’s no free lunch, kika kitu kizuri kinagharamiwa.

Wekeza muda kwa mtoto wako, badili mienendo yako ili mtoto wako nae aenende kama wewe, mentor wa kwanza wa mtoto ni mzazi/mlezi.

Ukiona hivyo vyote ni ngumu, unapofanya ngono kumbuka kumwaga nje, ngonoka siku ambazo si za hatari, tumia condom, acha kuendekeza nyege saa nyingine zipuuzie ili uishi maisha unayoyataka bila kubugudhiwa kuishi namna ya maisha kwa ajili ya mtoto wako.

NB: ITS EASLY SAID THAN DONE...👍🏼

Kasinde Mahaba.
 
Wewe unabeba mademu wa mtaani ambao huwajui lazima wawe vibaka. Mimi nasema kwa sisi wanachuo mademu tani kama ngapi unasoma nao alafu mwanaume mwenye afya na mkamilifu unakosa kuwa dhaifu walau mara moja moja?

Mtu pekee ninayeweza kuamini anajiepusha na hili ni mtumishi sana au sheikh mshika dini ila sisi wengine lazima tu uwe na mtu. Sasa huyo jamaa sio tu hana demu, bali hata haongei nao. Hata ukute anaongea mambo ya siri kwa kujificha utasikia tone na maneno anayotumia sio ya kuongea na mwanamke.

Ukishaona una mwanao au mdogo wako yuko chuo na hana dalili zozote za girlfriend kuwa makini nae
 
Mkuu uliyoyasema ni kweli ila nilicho pingana na wewe ni kuhusu kupeleka mademu geto.
Wengine hawapeleki mademu geto kwa sababu zao na si kwasababu si wanaume kamili naama magesti yamejaa mitaa.

Wenda huyo mshikaji alisha umizwa na mapenzi na ndio maana akaamua kuwa potezea mademu kwa muda.

Kigezo cha kumjua huyo demu hakiwezi kuwa hakikisho ya kwamba hawezi kukuibia maana yeye haji kuvunja bali wavunja wengine kabisa ambao hata kuwajua huwajui, yeye kazi yake ni kuja kusoma ramani tu.

Yule demu nyumbani kwao napajua na kabla ya kumtonza na kumla tulikuwa na mazoea ya kawaida ilikuwa ni ngumu sana kufikilia ya kwamba demu ni mafia la hatari.

Mm mwenyewe ilinichukua mwezi kugundua ya kwamba yule demu ndio aliye nichoma.

Nilikuja kugundua baada ya kukamatwa vibaka wakivunja geto la msela mwingine walipo banwa sana ndipo waka mtaja huyo demu,ya kwamba kazi ya yule demu nikwenda kwenye mageto ya masela anasoma ramani alafu ana kuja kuwaambia vitu vilivyomo geto kama geto lina vitu vya kiaina hiyo geto wanaipotezea lakini kama kuna vitu vya thamani basi huna bahati.

Na mpaka anakuja kugundulika alikuwa amesha chomesha mageto mengi.

Tulipo enda nyumbani kwao kumkamata tukaambiwa amesafiri kwenda mkoa mwingine ila nahisi wazazi walimficha, mwaka wa tatu sija wahi kumuona.

Ila siku nikimkamata naahidi ntamfanya kitu mbaya sana maana vitu nilivyo ibiwa nikikumbuka mwili huwa una sisimka kwa hasira.
 

Umesema sawa mkuu

wanawake wanawezeshwa ila hakuna anaewawezesha watoto wa kiume ili waweze kuendana na hao wanawake waliowezeshwa. Mwisho wa siku tunakuwa na wanawake wa kisasa na wanaume wanaotaka wanawake traditional kama mama au bibi zao. Hapa lazma misuguano itokee

Wanaoumia sana sana ni watoto maana tunakuwa na kinamama wanaohisi wanaweza kulea pasipo wanaume na kinababa wasioona umuhimu wa mwanamke katika malezi ya watoto which is wrong

Baba anawafundisha watoto uhalisia wa maisha na jinsi ya kupambana nayo in a hard way. Anawapa financial security pamoja na ulinzi juu ya watu wabaya

Mama pia anawapa watoto emotional security and stability. Mama ndio anawafundisha watoto upendo na kujali

Hivi vyote ni muhimu kwa mtoto, kikikosekana kimoja itabidi mzazi anaebakia atafute namna ya kufit, kitu kwa maisha ya sasa ni ngumu sana
 
ukisikia kesi za ulawiti ni wajomba, baba wadogo mara babu. Mbaya zaidi yanamalizika kifamilia huku hawa watu wakiendelea na uharibifu wao
Yan hapa napo inatakiwa paangaliwe kwa umakin sana
 
Umesema ukwel kabsa kumuwesha mtoto wa kike wakamsahau mtoto wa kiume kuna effects nyingi sana sio kwenye malezi tu bali had kwenye ngazi ya familia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…