Malezi ya sasa bado siyaelewi

Kasie Matata[emoji91][emoji91][emoji91][emoji736]
 
Afadhali wewe umekutana na mfano halisi. Niliposoma uzi, nilipata wazo la mama kutamani mtoto wa kike wakati aliye naye ni wa kiume, ila skuwa na mfano hai.
 
Hapo labda wa kulaumiwa ni huyo mkufunzi wa Dodoma aliyekuwa na ndoto za kupata mtoto wa kike, asimpate, na inavyoonekana anajaribu kumchukulia wa kiume kama wa kike.
Ila hao wengine, watoto wameshakuwa wakubwa, wanafanya maamuzi yao, kama wazazi, wafanye nini?
Na nyie mnaojiona rijali wa kuingiza wasichana, muwe tayari kulea watoto kama familia na mtakaowapa mimba, la sivyo mtaishia kuwaumba watu wapya wenye tabia unazozipinga.
 
Kinacho nisumbua ni kwanini kizazi hichi kimeshindwa kutoa malezi yaliyo sahihi kwa jinsia sahihi?

Mkuu shida ni utandawazi,,,malezi ya kimagharibi..

Siku hzi malezi ya kimagharibi yametapakaa sana na jamii imeamini ndio malezi sahihi,,, hakuna viboko,, mtoto wa mwenzako siku hizi sio wako kama zamani( ulezi shirikishi,,,umefanya kosa na mtoto wa jirani...mnaadhibiwa wote hukohuko kwa jirani),,,,siku hizi ubinafsi umekuwa mkubwa sana,,, namna ya kulea watoto tunapangiwa n.k.

Single maza wa kitambo wengi unakuta wana misingi ya kiafrika,,,so walivaa uhusika wa Mama na Baba....

Single Maza wa siku hizi wanafikiri kulipa hela na mahitaji pekee ndio majukumu ya Baba.... wamekuwa wa hovyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…