commitment muhimu sana kaka. Kuna time kinywaji kimekolea inabidi uache urudi home mapema ujue mtoto amekula, na ule nae. Huwezi lala kabla mtoto hajalala. Asubuhi inabidi uamke mapema uhakikishe anaenda shule yuko smart. Inabidi ujenge urafiki nae ili awe huru kufunguka kwako, hapo utajua yanayomkuta shule, watu anaokutana nao, marafiki zake wakoje, fikra na mitazamo yake ikoje ili umshape. Needs a high commitment!
Nidhamu na kujiota kwa wazazi katika kulea watoto ni muhimu sana. Mara zote wazazi wengi wamewaacha watoto wakae na walezi wao kuliko wao. Kama kuna kitu watoto hawapendi katika maisha yao ni kuona wazazi hawana nidhamu, kila wanachoongea kinakinzana na kile wanachowafanyiwa watoto. Wazazi hawaongei ukweli kwa watoto na kuwapelekea watoto kuishi bila kujua misingi ya familia inaelekea wapi.
Adhabu wanazopewa watoto haziilingani na kosa alilofanya mtoto (never displine a child in anger)
Watoto wanahitaji malezi ya usawa, hasa wale tunaolea watoto wa ndugu zetu na wetu, ni vizuri mzazi ukatengeneza usawa. Kama unaleta zawadi, basi leta zawadi zinazofanana.
Usiruhusu watoto wako kwenda kinyume na yale maelekezo uliyowapa au kubalidili maelekezo bila kuwashirikisha na kuhakikisha waelewe kwa nini umebadili.
Mtoto aheshimiwe, usipende sana kumkaripia mtoto au kumpiga mbele ya rafiki zake au kadamnasi, unamjengea hofu.
Watengenezee ratiba watoto wafanye nini na kwa wakati gani, hakikisha watoto wanaangalia au kusoma vitu vinavyowatengenezea ubongo wao kukua katika maadili.
Wazazi, tengenezeni ratiba za watoto wenu pamoja, elewaneni, ikitokea mtoto kakosea, asipate sababu ya kukimbia jukumu lake.
Watoto wanaumie sana wanapoona wazazi mnagombana kila kukicha, hakuna siku hamrushiani maneno ya hovyo mbele ya watoto wenu bila kufikiria ni kiasi gani mnaawathiri.
Watengenezee watoto wenu muda wa kukaa pamoja, watengenezee muda wa kuwapa kalamu na karatasi waandike yale wanayohisi yanahitaji kufanyiwa marekebisho, acha watoto wakutathimini utendaji wako, usiwaburuze ukahisi hawaelewi au hawana cha kukwambia. wanaogopa.
Zingatia kuwafundisha watoto siyo kuwaadhibu.