Malezi ya wazazi wa siku hizi na dosari zake!

Tunakoelekea huko sijui kwakwel
 
Naitaji kuelewa kitu:
Ni umri gani mtoto anakua muelewa unapo muambia akuskiye?? Mana watoto wengine unakua unaona bado hajajua zuri wala baya una amua kupotezeaa!!!
 
Naitaji kuelewa kitu:
Ni umri gani mtoto anakua muelewa unapo muambia akuskiye?? Mana watoto wengine unakua unaona bado hajajua zuri wala baya una amua kupotezeaa!!!
Kawaida watoto wote ni wadadisi na watundu kwani hawana wajualo

Katika makuzi yao kuanzia miezi 9 hadi miaka kumi watoto hua wanataka kujifunza na kujaribu kila kitu

Ni kipindi hicho ndio unatakiwa akiwa anafanya jambo ambalo ni kinyume na maadili au lolote baya unamuonyesha hata kwa ishara au kwa maneno kua halifai na unampa moyo pale anapofanya jambo zuri

Hapa wala haihusiani na kumchapa kwani maneno yenye maelekezo na makatazo yakiwa kwa msisitizo watoto wanaelewa

Ndiyo maana hata kwenye uchezeaji wa simu utakuta simu za kina baba hua hazichezewi sana na watoto na wala sio kama wakichezea wanachapwa bali watoto hujifunza kua baba hataki simu yake ichezewe

Kwahiyo ndugu yangu umri wote wa kuanzia miezi tisa hadi miaka kumi ni umri tete na muhimu sana kwa mafunzo na maelekezo ya watoto
 
Asante saana Mungu akubariki [emoji120][emoji120]
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…