Malezi ya wazazi wa siku hizi na dosari zake!

Malezi ya wazazi wa siku hizi na dosari zake!

Tunaita maendeleo. Tunawapenda watoto kama property sio kama wanadamu

Fahari ya mzazi wa zamani ilikua ni kumuona mwanae anaishi kwenye jamii kama mtu aliyelelewa katika maadili

Fahari ya wazazi wa siku hizi ni kuona watoto wao wakiwa tofauti ki muonekano wa mavazi, elimu na hata maadili

Kwao wao akimpa mtoto mahitaji ya kimwili kama nguo na vitu vya kuchezea vya thamani na shule nzuri baaasi, imetosha maadili sio priority tena
Tunakoelekea huko sijui kwakwel
 
Naitaji kuelewa kitu:
Ni umri gani mtoto anakua muelewa unapo muambia akuskiye?? Mana watoto wengine unakua unaona bado hajajua zuri wala baya una amua kupotezeaa!!!
Jumapili iliyopita nilihudhuria kwenye msiba wa ndugu wa rafiki yangu, Miongoni mwa waombolezaji alikua dada mmoja mwenye miaka kama 26-30, alikuwa na mwanae wa kama miaka minne hivi

Sijui ilikuaje lakini mara yule dogo akaanza kulia na kisha kumvurumishia ngumi na mateke mama yake. Mama mtu akabakia kusema tu " Brian stooop banaa". Mpaka mama mmoja alipokuja akamwambia hiyo ni aibu mwanao hata kama ni mdogo unamuachia akupige hivyo hebu ingieni kule chumbani mkabembelezane

Watoto wote wadogo sio ajabu kuwa na utundu lakini utundu mwingine nahisi kama ni wa kukosa adabu na unaendekezwa na wazazi hasa wakike.

Nimewahi kushuhudia mtoto wa chini ya miaka mitano akiipasua simu ya mama yake kwa makusudi kwa kuibamiza chini na mama mtu anasema "mmmh leo sijui kakasirika nini huyu!" halafu akaanza kumbembeleza!

Kuna mtoto wa shangazi yangu aliwahi kumtupia usoni mfuko wa chips mama yake baada ya kugundua alicholetewa sio alichomuagiza wakati anaenda kazini!

Hapo kwenye msiba baada ya tukio la huyo mama na mtoto watu walisema mengi sana kuhusu dosari za kimalezi za wazazi wa kike wa siku hizi. Kuna mzee mmoja akawa anasema dunia inavokwenda huko baadae hayo mapenzi ya mama na mwana yanaweza kufikia hatua ya aibu zaidi hata mama "kumuonjesha" mwanae atakapo balehe

Sina hakika kama haya mambo ya kudekeza watoto kiasi hiki yalikuwepo zamani ila nahisi mengine ni kuwapotosha watoto kwa kuwapa malezi yasiyofaa.
 
Naitaji kuelewa kitu:
Ni umri gani mtoto anakua muelewa unapo muambia akuskiye?? Mana watoto wengine unakua unaona bado hajajua zuri wala baya una amua kupotezeaa!!!
Kawaida watoto wote ni wadadisi na watundu kwani hawana wajualo

Katika makuzi yao kuanzia miezi 9 hadi miaka kumi watoto hua wanataka kujifunza na kujaribu kila kitu

Ni kipindi hicho ndio unatakiwa akiwa anafanya jambo ambalo ni kinyume na maadili au lolote baya unamuonyesha hata kwa ishara au kwa maneno kua halifai na unampa moyo pale anapofanya jambo zuri

Hapa wala haihusiani na kumchapa kwani maneno yenye maelekezo na makatazo yakiwa kwa msisitizo watoto wanaelewa

Ndiyo maana hata kwenye uchezeaji wa simu utakuta simu za kina baba hua hazichezewi sana na watoto na wala sio kama wakichezea wanachapwa bali watoto hujifunza kua baba hataki simu yake ichezewe

Kwahiyo ndugu yangu umri wote wa kuanzia miezi tisa hadi miaka kumi ni umri tete na muhimu sana kwa mafunzo na maelekezo ya watoto
 
Asante saana Mungu akubariki [emoji120][emoji120]

Ila huu uzi umenikumbusha katoto ka Dada angu ..kale katoto kamelelewa ovyo kabisa..lilitokea tukio kama ilo la msiba tuko msibani katoto kanamwambia mama ake waondoke..mama ake anakaambia subiri tuzike tutaondoka mtoto acha acharuke anamvuta mama ake nguo yani ili mradi amkere wanyanyuke waondoke..yule dada baada ya kuona kero zimezidi akampiga kale katoto kofi .

Kakaanza kujiliza kanabembelezwa kanazidisha sauti mama ake akawa kama anamnon'goneza katoto si kakaropoka "toka hapa ndio maana baba anakupigaga"

Aibu niliona mimi
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom