Mali hutengeneza mali; Hakuna cha miujiza, mafuta ya upako, bahati, nyota, kibali, visomo, uganga, majini wala meditation

Mali hutengeneza mali; Hakuna cha miujiza, mafuta ya upako, bahati, nyota, kibali, visomo, uganga, majini wala meditation

EBO Mungu wa Israeli ameingiaje hapa? ? ?

Ukiona unamuwaza Mungu wa Israeli halafu unawaza hela, si Mungu wa Israeli huyo! ! ! Huyo ni mwinignie uliyeingizwa kingi na false prosperity preachers.

Sema nini, ana namna yake tu ya kuku bless when you least expect it, when it's the last thing you think about! ASIFIWE SANA MUNGU WA ISRAELI, MUUMBA WA MBINGU NA NCHI. OUR GOD IS AN AWSOME GOD!
Mungu wa waisrael hawa wanaoua watoto wa kipalestina ? Au unazungumzia waisraeli wapi?
 
Mungu wa waisrael hawa wanaoua watoto wa kipalestina ? Au unazungumzia waisraeli wapi?
Myahudi wa kweli, Muisraeli wa kweli ni yule aliyemkubali YESU.

"Kwa maana mtu si Myahudi kwa vile alivyo kwa nje, wala tohara ya kweli si kitu cha nje au cha kimwili.

Lakini mtu ni Myahudi alivyo ndani, nayo tohara ya kweli ni jambo la moyoni, ni la Roho wa Mungu, wala si la sheria iliyoandikwa. Mtu kama huyo hapokei sifa kutoka kwa wanadamu bali kwa Mungu
."
Waroma.2.28-29.NENO

Hawa Wayahudi wa leo ambao walimkataa YESU na bado wanamsubiri Masihi, wamefungwa ufahamu kwa muda mpaka dunia nzima isikie kuhusu YESU, kisha wao watakuwa wa mwisho, watafunguliwa macho na kumtambua na kutubu, lakini baada ya dhiki nyingi, and they will call upon him whom they pierced, then our Lord will set foot in Jerusalem.

"Ndugu zangu, ili msije mkajidai kuwa wenye hekima kuliko mlivyo, nataka mfahamu siri hii: Ugumu umewapata Israeli kwa sehemu hadi idadi ya watu wa Mataifa watakaoingia itimie."
Waroma.11.25.NENO

"Kwa maana nawaambia, hamtaniona tena tangu sasa hadi mtakaposema, ‘Amebarikiwa yeye ajaye kwa Jina la Bwana.’"
mathayo.23.39.NENO

"Ole! Kwa kuwa siku ile itakuwa ya kutisha. Hakutakuwa na nyingine kama hiyo. Utakuwa wakati wa dhiki kwa Yakobo, lakini ataokolewa kutoka dhiki hiyo."
jeremiah.30.7.NENO

"Nami nitawamwagia watu wa nyumba ya Daudi, na wenyeji wa Yerusalemu, roho ya neema na kuomba; nao watamtazama yeye ambaye walimchoma; nao watamwombolezea, kama vile mtu amwombolezeavyo mwanawe wa pekee; nao wataona uchungu kwa ajili yake, kama vile mtu aonavyo uchungu kwa ajili ya mzaliwa wake wa kwanza.'
zekaria.12.10.SUV

Waone wanajua kabisa wakati umefika, hawajui tu ni yule waliyemkataa ndie anarudi:

View: https://youtu.be/M2Po_MiAQS4?si=WWKNdq1dv5VkK2FI
 
Meditation usiikate: Matajiri bongo zao zinaenda nyumba na mbele, wanawaza na kuwazua, wanahama fikra kabisa, wanahitaji utulivu.Huwezi pata clarity na idea kama huwezi reconcile na kuruhusu kichwa kikatafuta chenyewe basing na experience,facts etc...
 
Meditation inakupa utulivu wa akili , na katika utulivu unaweza pangilia mambo yako yakaenda sawa.
 
Historia za jamii zilizo na legacy ya utajiri au mafaniko makubwa ya kifedha na mali zisizohamishika imetokana na wao kuwa aggressive katika kushinda ushindani, kuchukua kwa nguvu kwa wale walio wadhaifu, kuchakata fikra ya kushinda uzalishaji duni, kuwahi rasilimali ambazo hazijafanikiwa kufikiwa, kunyonya wale ambao bado hawashtuka na kurithisha ulivyopata kwa wale watakaomfata.

Kwa hio rasilmali hutengeneza mali, mali hutengeneza pesa, pesa hutengeneza utajiri.

Tofauti na hapo utamlaumu Mungu sana kwa nini hajibu maombi yako.

Utajichukia kwa kujiita mwenye mikosi.

Utaumia kwa kuchukia walio kuzidi.

Utawehuka ukitafuta elimu za giza za kufikirika

WEALTH CREATES WEALTH
Kuna watu bado wana amini katika kuroga ndio wafanye biashara
 
Meditation inakupa utulivu wa akili , na katika utulivu unaweza pangilia mambo yako yakaenda sawa.
Na kweli kabisa bila mental clarity hutoboi wengi wao utasikia aliwikawika akapotea pesa alikuwa nayo ni nyingi kuzalisha ,connection ya maana bila hata yeye kuingiza pesa yake advance anapata faida credibility usiseme anakuja angushwa na vitu vidogo mental clarity ni muhimu watu hawaelewi tu.....
 
Na kweli kabisa bila mental clarity hutoboi wengi wao utasikia aliwikawika akapotea pesa alikuwa nayo ni nyingi kuzalisha ,connection ya maana bila hata yeye kuingiza pesa yake advance anapata faida Ila sasa mental clarity ni muhimu watu hawaelewi tu
Kabisa , na vijana wengi wana matatizo ya akili , kutokana na ukali wa maisha , na mitindo ya maisha hasa ya mitandao ya kijamii, hivyo meditation ilipaswa iwe soma la msingi tokea vidudu kabisa , now kuna taka taka nyingi zinazolipua kichwa.
 
Kabisa afya ya akili ndo ugonjwa unaosumbua wengi wetu Ila sababu hata viongozi bado hawajajali mstakabali wa taifa tunawaza kuvuruga vijana akili kwa kuwa tablet kwanzia utotoni tukiona ni fahari kumbe tunazidi wakoroga mchawi ni kitu kidogo tu tahajudi bila kuona haya tutaendelea kuwa wakutangatanga na kuonewa badala ya kuona
 
Ushaona mfanyabiashara tajiri anaeleza hatua kwa hatua jinsi alivyoanza biashara hadi kutajirika katika maelezo yenye kueleweka kwa hapa afrika?
Mi ninaamini ukitaka kuwa na Tajiri mkubwa you have to bend some laws ila hapo kwenye uchawi bado sijajua mechanism yake inakuaje, wakati naanza biashara nilipata sana suggestions za waganga kila anaekuja anasema lake na mimi nikakaza tu nione itakuaje kumbe uchawi ni management tu
 
Watu ni juhudi zao zinawabeba ila kwa kuwa alienda kwa mganga atajua ni uchawi umemkomboa.
 
Mi ninaamini ukitaka kuwa na Tajiri mkubwa you have to bend some laws ila hapo kwenye uchawi bado sijajua mechanism yake inakuaje, wakati naanza biashara nilipata sana suggestions za waganga kila anaekuja anasema lake na mimi nikakaza tu nione itakuaje kumbe uchawi ni management tu
Ni suala la kila mtu anavyoamini kwa sababu kwenye haya masuala watu wanapitia experience tofauti hakuna formula moja, unakuta njia aliyopita A na hadi kufanikiwa B alipita na hakufanikiwa ila alipofanikiwa B huko C hakuweza kufanikiwa.

Binafsi nimejifunza binaadamu hatupo sawa unaweza ukamuona mtu yupo kawaida tu, kwenye biashara anafanikiwa vizuri sana na kweli hajihusishi na ndumba wala sio mtu wa kujihusisha na masuala ya Mungu basi ukadhani ukifanya kama anavyofanya yeye unaweza nawe ukafanikiwa ila unakuta haiwi hivyo.
 
Back
Top Bottom