Mali inakuwa ya umma pale umma unapomiliki hisa

Mali inakuwa ya umma pale umma unapomiliki hisa

GwaB

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2014
Posts
4,291
Reaction score
5,786
Kwa muda mrefu sasa tumekuwa tukihamasishwa kulinda mali zinazoitwa za umma na kutahadhalishwa kuwa atakaechezea mali ya umma atawajibishwa. Imekuwa hivyo kwa miongo kadhaa na imezoeleka hivyo pamoja na kwamba ni ulaghai tu.

Kwenye mjadala huu pamoja na upana wake ningependa kuwaalika wadau tijaribu kudadisi hapo kwa uchache mali za umma zilizopo na zijazo kwa kujiuliza maswali haya:

: Mali za umma ni zipi? Mali za umma ziko wapi?
:Mali za umma zinamilikiwa na nani na kwa utaratibu upi?
:Mali za umma zinasimamiwa na nani? :Mali za umma zinaendeshwa na nani
: Mali za umma zina mgawanyo upi?
: Faida na hasara inabebwa na nani?
: Mikataba inaingiwaje? Maslahi yapi?

Hapo juu ni baadhi ya maswali ya kujiuliza ingawa yako mengi, tutafakari haya mengine yanaweza kuongezeka.

Tanzania tangu kupata uhuru imekuwa na mashirika na makampuni mengi tu ambayo tunaweza kuyaita ya Serikali na mengi yalifilisika na mengine kubinafsishwa. Hivi sasa kuna mwelekeo wa kufufua baadhi ya mashirika kwa mtindo ule ule wa awali ambao utakuja kuyafilisi.

Kama kweli kuna nia njema ya Serikali kuwainua wananchi kiuchumi ni vema sasa Serikali ikatenga asilimia 20-40 ya hisa zake inazomiliki kwenye makampuni, mashirika na taasisi, ziuzwe kwa mwananchi mmoja mmoja au makampuni binafsi kama njia moja ya uwekezaji.

Kuna azimio liliwahi kutolewa na kujadiliwa Bungeni likihimiza makampuni na mashirika yote yaorodheshwe kwenye soko la hisa, hili halijatekelezwa hadi leo kwa sababu likifanyika litagusa maslahi ya viongozi wachache wakiwemo wabunge wenyewe, lakini pia kuogopa mashirika kuendeshwa kwa uwazi zaidi pale wananchi wengi watakapokuwa na uwezo wa kuwasimamia kupitia hisa wanazomiliki.

Manufaa ya kuwashirikisha wananchi kumiliki hisa za mashirika kupitia soko la hisa, na faida kubwa itokanayo na kuorodheshwa kwenye soko la hisa, ni kupata mtaji wenye gharama nafuu utakaowezesha mashirika na makampuni kama ATCL, TRC, Bandari, Posta, Simu, na mengineyo kuweza kujiendesha na kulipa madeni. Naamini wananchi wengi tu wakielimishwa vyema watapenda kushiriki kwenye uchumi wa nchi hii na kupitia hisa zao kwenye mashirika na makampuni haya na hivyo kuleta maana halisi ya mashirika au makampuni ya umma.

Kwa utaratibu wa mali hizi kuwa chini ya umiliki wa Serikali, maana yake ni kukabidhi mali ya walio wengi kwa watu wachache kwa jina la SU. Naamini tumejifunza kuwa mali zilichezewa huko nyuma kwa msemo wa hovyo kuwa 'Mali ya Umma haina mwenyewe' tusiendeleze mtazamo huu.

Tubadilike!
 
Hata hizo hisa zikiuzwa matapeli ya CCM yatauziana
Hapana mkuu, kampuni ikiishaorodheshwa kwenye soko la hisa uuzwaji wa hisa zake uko wazi kabisa, kinachoamua ni pesa yako tu. Matapeli unaowasema hawana ubavu wa kununua hisa zote peke yao.
 
Hapana mkuu, kampuni ikiishaorodheshwa kwenye soko la hisa uuzwaji wa hisa zake uko wazi kabisa, kinachoamua ni pesa yako tu. Matapeli unaowasema hawana ubavu wa kununua hisa zote peke yao.
Mhhhh Rostam, Lowassa, MO, Shabibi, Makonda, Bakheresa, Manji yote yapo kule wewe utaenda kununua nini?
 
Hakuna mtu toka CCM atakubali jambo hili kumbuka ya Escrow wabunge wale wale wakina Simba walisema ni mali za watu binafsi na sio za Umma
 
Serikali inapomiliki mali hufanya hivyo kwa niaba ya wanachi, na hapo ndipo dhana ya mali za umma huanzia. Na kwa kufanya hivyo ndipo huduma mbalimbali huweza kutolewa kwa wananchi kupitia kodi na maduhuli mbalimbali yanayolipwa serikalini na wananchi wenyewe.

Serikali huitwa ni ya umma kwa sababu wananchi wenyewe ndio huigharamia ili iweze kuendesha shughuli za kila siku. Kwa hiyo si sahihi kusema wananchi pale wanapomiliki hisa katika mashirika na taasisi za kiserikali ndipo hutambulika kuwa wamiliki wake.
 
Back
Top Bottom