Mali, Pesa na Nyumba. Vya (Baba & Mama/ Mke)

Tman900

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2017
Posts
589
Reaction score
1,897
Mi nimezaliwa Dar na Nimekua Dar, nimejipambania kutafuta kile Mungu amenijalia kilicho kidogo changu, Ila nafsini mwangu mi sitaki chochote Cha urithi iwe kwa Familia yangu niliozaliwa yaani kwa baba na Mama Yangu.
Ingawa sijawaeleza ndugu zangu.Kua sihitaji chochote.

Ikitokea wazazi wetu wamefariki nitawaeleza ndugu zangu.
Kuhusu mke pia vivyo hivyo, mke nilienae sihitaji Mali yake kwa chochote, ikitokea mke ametangulia mbele ya haki kilichopo nitawapa Familia yake Mali zote. Isipokua watoto tu ndo nitaomba nibaki nao.

Mali yoyote ambayo inahusisha kurithi Wala nafasi Yangu aivutiwi kua na hiyo Mali.

Baba Mama na Mke, Ni watu muhimu Ila nafsi Yangu tu haipendi vitu vya urithi.
 
Kwahiyo sisi tufanyaje..tungewafahamu hao ndugu zako tungekusaidia kuwafahamisha.
Ila wewe Mali zako watarithi.
 
Mi nimezaliwa Dar na Nimekua Dar, nimejipambania kutafuta kile Mungu amenijalia kilicho kidogo changu, Ila nafsi mwangu mi sitaki chochote Cha urithi iwe kwa Familia yangu niliozaliwa yaani kwa baba na Mama Yangu.
Ingawa sijawaeleza ndugu zangu.Kua sihitaji chochote.

Ikitokea wazazi wetu wamefariki nitawaeleza ndugu zangu.
Kuhusu mke pia vivyo hivyo, mke nilienae sihitaji Mali yake kwa chochote, ikitokea mke ametangulia mbele ya haki kilichopo nitawapa Familia yake Mali zote. Isipokua watoto tu ndo nitaomba nibaki nao.

Mali yoyote ambayo inahusisha kurithi Wala nafasi Yangu aivutiwi kua na hiyo Mali.

Baba Mama na Mke, Ni watu muhimu Ila nafsi Yangu tu haipendi vitu vya urithi.
Inategemea huo urithi uko wapi. Kama uko huko bush bush aaah hata mm sina haja nao. Ila assume uko pale kariakoo eneo unasikia likiuzwa ni bills 4 nani asitake mgao
 
Kujitafutia chako ni jambo jema tu.Lakini,ikitokea wazazi/ndugu kwa upendo na utaratibu halali wa jamii yako,wakaamua kukurithisha kitu ni vema uchukue.Matumizi utapanga mwenyewe au kuhifadhi kadiri ya mrithishaji na wosia wake.
 
Maisha yanabadirika Bora ukae nalo moyoni usilitamke waziwazi Mambo yakiwa ndivyo sivyo umelazwa Mwaisela hujitambui watahoji "Si alituambia hataki chochote huyu atatumia vya kwake?"
Pole ndugu..
 
Pole ndugu.. mi sijasema tuko sawa ndugu wote.
Haina maana kwamba utakua ulivyo siku ZOTE kuna siku utaomba watu wakusaidie kukutembezea bakuri usaidiwe chochote, sasa ukiongea maneno ya nyodo mapema hivyo km una guarantee na uhai wako au ufahari ulionao kwamba hautowahi kufirisika au hautowahi kushuka chini, siku yakikufika Jamaa wanachofanya ni kufanya reference tu alishasema hivi na hivi, mchezo umeishia hapo
 
Sawa Ndugu kwa ushauri. Nimeufanyia kazi.
 
Inategemea huo urithi uko wapi. Kama uko huko bush bush aaah hata mm sina haja nao. Ila assume uko pale kariakoo eneo unasikia likiuzwa ni bills 4 nani asitake mgao
Ukiwa na akili za namna hii inaashiria uko tayari hata ku plan kumuondoa uhai mwenye mali ili upate urithi, ni suala la muda tu.
 
Mi nimezaliwa Dar na Nimekua Dar, nimejipambania kutafuta kile Mungu amenijalia kilicho kidogo changu, Ila nafsini mwangu mi sitaki chochote Cha urithi iwe kwa Familia yangu niliozaliwa yaani kwa baba na Mama Yangu.
Ingawa sijawaeleza ndugu zangu.Kua sihitaji chochote.

Ikitokea wazazi wetu wamefariki nitawaeleza ndugu zangu.
Kuhusu mke pia vivyo hivyo, mke nilienae sihitaji Mali yake kwa chochote, ikitokea mke ametangulia mbele ya haki kilichopo nitawapa Familia yake Mali zote. Isipokua watoto tu ndo nitaomba nibaki nao.

Mali yoyote ambayo inahusisha kurithi Wala nafasi Yangu aivutiwi kua na hiyo Mali.

Baba Mama na Mke, Ni watu muhimu Ila nafsi Yangu tu haipendi vitu vya urithi.
Mali za urithi huwa zina nongwa sana
 
Kuhusu mali au pesa usije ukatamka kuwa hautaki hata Kama unazo mali nyingi na pesa nyingi.

Kurithi mali na pesa sio udhaifu.

Sema wewe kuna hatua umeifikia huwa inaitwa satisfaction au complacent - hii ni hataua ya kuridhika na kuona ulipo panatosha hivyo utakaa katika eneo huitwa Comfort zone.

Unabidi uendelee kuhitaji pesa na mali haijalishi umerithi au za baba mkwe muhimu usimuibie MTU .
 
Mila zinataka urithi hata koti la suti ukakae nalo kwako.

Anyway ni jambo zuri,umasikini na utegemezi wa mali za ulithi ni chanzo cha uhasama sehemu nyingi.na sijajua kashetani gani huwa kanawaingia watu!!!
 
Ukiwa na akili za namna hii inaashiria uko tayari hata ku plan kumuondoa uhai mwenye mali ili upate urithi, ni suala la muda tu.
Tunaongelea urithi sio kumwondoa mwenye mali. Hakuna ambaye atakataa kuwa kwenye urithi wa eneo kama hilo. Mimi nimerithishwa mali nyingi ziko huko bush nyumba, mashamba ya miti, mashamba mengi. Nyumba za maana mbili mzee kajenga huko lakini kwangu ni mzigo maana nalipa watu kukaa. Yani huwezi zipangisha hakuna wa kupanga, siwez ziuza pia. Mtu anaishi na bado unamlipa hadi luku unamnunulia.
Hakuna ambaye hataki urithi wa maeneo potential kama kariakoo
 
Kuhusu mali au pesa usije ukatamka kuwa hautaki hata Kama unazo mali nyingi na pesa nyingi.

Kurithi mali na pesa sio udhaifu.

Sema wewe kuna hatua umeifikia huwa inaitwa satisfaction au complacent - hii ni hataua ya kuridhika na kuona ulipo panatosha hivyo utakaa katika eneo huitwa Comfort zone.

Unabidi uendelee kuhitaji pesa na mali haijalishi umerithi au za baba mkwe muhimu usimuibie MTU .
Asante kwa ushauri, nitajifunza na kuendelea na upambanaji wa kujitafutia kipato.
 
Tunaongelea urithi sio kumwondoa mwenye mali. Hakuna ambaye atakataa kuwa kwenye urithi wa eneo kama hilo. Mimi nimerithishwa mali nyingi ziko huko bush nyumba, mashamba ya miti, mashamba mengi. Nyumba za maana mbili mzee kajenga huko lakini kwangu ni mzigo maana nalipa watu kukaa. Yani huwezi zipangisha hakuna wa kupanga, siwez ziuza pia. Mtu anaishi na bado unamlipa hadi luku unamnunulia.
Hakuna ambaye hataki urithi wa maeneo potential kama kariakoo
Duuh Kweli tunatofautiana, mimi binafsi mali ya urithi nilishaiondoa kwenye akili zangu, Baba yangu wa kambo aliniweka kwenye urithi wa moja kati ya mali zake lakini nilikataa, sio kwamba tuna migogoro ya kifamilia au matatizo yoyote ila nilikataa tu, kwa sababu huwa naamini urithi pekee nilio nao ni akili yangu tu, na inanitosha kupata nachohitaji maishani.
 
Nmerithi mali na hakuna hata mali moja niliyouza na wala kuitegemea. Mimi naishi kwa pesa na juhudi zangu. Nimerithi mashamba ya miti, sijawahi kukata hata mti mmoja. Ni mwaka wa tatu nimeyamwachia ndugu yetu aliyekywa anazitunza kwa niaba ya mzee aendelee kkuitunza na kuvuna kama kawaida kwa maslahi yake mwenyewe kama ilivyokuwa kabla ya mzee kufariki. Nmerithi nyumba mbili standard sema siko vijijini huko. Badala ya kufaidika nazo mimi natumia ela kulipa watu waziangalie maana siwez kuziuza wala kupata wapangaji. Zitakaa tu nami nitawarithisha wanangu wajue chimbujo letu.
My point is...
Kuna urithi mwingine ni mzigo au unakuwa wa kawaida. Ila kuna urithi mwingine kila mtu atatamani apate mgao. Nikakupa mfano imagine mzee wako ana eneo kariakoo thamani yake ni bils kama 4. Mko watoto 4 tu, utakataa huo urithi?
Kuna vitu ni so tempting to say no.
 
Urithi ni haki ya kila mtoto ila sasa sio busara kudai au kukataa urithi. Ni sawa na kumsusia marehemu na mali zake.

Mtu halaimishwi kurithi mali ila sisi ni jamii tayari kuna kanuni zipo sio lazima kuzifuata ila ni muhimu kuzitambua.

Hapa unaweza ukawa na wazo a kutokuhitajisehemu ya urithi wako, ia kuna mazingra unaweza jikuta wewe ndio mtu unayeweza kusimamia na kuendeleza mali za marehemu, hapo ukikataa kurithi sio busara kabisa.

Fikiria wewe hapo sasa hiv mtoto wako anakuambia hahitaji mali yako yoyote, aise utafadhaika sana hasa ikiwa ni mtu ulikuwa unaamini ataendeleza ulichokianzisha.

Wahenga walisema, busara ni kukaa kimya. Usije ukasema hicho hadharani. Ikitokea watu wakagombea mali za marehemu sasa hapo wewe kaa kando n uwaambie umejivua lawama na mabalaa yajayo, na hili wajue na kufahamu.
 
Back
Top Bottom