Ukitaka kumuua NYANI usimtazame USONI.Umofia Kwenu Wana JF,
Kampuni ya Yono Kupitia TRA yamekamata majumba matatu ya Lugumi yaliyoko Ndege Beach Mbweni kwa kudaiwa kodi ya zaidi ya Bilioni 14.
Nawasilisha kutoka MINJINGU.
=======
Kampuni ya udalali ya Yono, imefanikiwa kukamata mali za wafanyabiashara wanaodaiwa kodi ya serikali inayofikia zaidi ya Sh bilioni 68.1. Operesheni ya kukamata mali hizo kwenye maeneo mbalimbali ndani na nje ya Jiji la Dar es Salaam imefanywa ndani ya wiki moja.
Katika operesheni hizo maofisa wa Yono wamekuwa wakishirikiana na maofisa wa Mamlaka ya Mapato(TRA), ambayo ndiyo imeipa kampuni hiyo kazi ya kukusanya kodi kwenye maeneo mbalimbali nchini.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Yono, Scholastica Kevela, Yono imepewa kazi na TRA kukusanya madeni yake ya kodi kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Pwani Njombe, Mbeya, Iringa na Zanzibar.
Aliwataka watanzania kuunga mkono jitihada za Rais John Magufuli za kuleta maendeleo kwa kulipa kodi bila shuruti ili zipatikane fedha za kujenga miundombinu kama barabara, reli, shule, madaraja, hospitali na zahanati.
Kuhusu taarifa zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii kwamba hata baadhi ya mali za Kampuni ya Lugumi zimeshikiliwa, Mkurugenzi huyo alithibitisha kuwa habari hizo ni za kweli ambapo wanashikilia nyumba za kifahari za mfanyabiashara huyo.
“Mmeniuliza kwamba mmesikia nyumba za Lugumi zimefungiwa ni kweli, amefungiwa nyumba zake za kifahari na anadaiwa Sh bilioni 14, yupo mtu anaitwa Gm Dewji naye anadaiwa Sh bilioni 1.8, Kampuni ya ujenzi ya Mutluhan Construction anadaiwa Sh bilioni 45,”alisema.
Alisema wanaodaiwa wanapaswa kulipa madeni yao TRA ndani ya siku 14 na kwamba muda huo ukipita watapewa maelekezo na serikali kama ni kuuza mali hizo ili kufidia madeni yao.
Ofisa Mwandamizi wa TRA, ambaye hakupenda jina lake litajwe alithibitisha kwamba nyumba ya Lugumi iliyoko Upanga mtaa wa Mazengo inashikiliwa na mamlaka hiyo na ghorofa la kifahari lililoko Mbweni JKT, Dar es Salaam.
“Hakuna siri maana mkienda kwenye hizo nyumba mtakuta alama ambazo huwa Yono wanaweka kwa nyumba inayoshikiliwa, nendeni Upanga na kule Mbweni JKT mtakuta hizo nyumba tunazoshikilia,” alisema
Chanzo: HabariLeo
Hivi kulalamika kwetu kunazuia nini serikali kufanya kazi zake? Pili, mbona Tanzania hakuna walalamikaji! Hivi kuna wananchi wanaolalamika kama wamarekani na waingereza? Lakini nchi hizo zinasong mbele!JPM ana mapungufu mengi kama Kiongozi na kama binadamu. Lakini tujitahidi kuona hata yale mazuri kidogo anayoyafanya. Otherwise..tutakuwa tunalalamika tuu for the next ten years! and at the end of the day...we will have achieved one thing only. NOTHING!.
Habari wadau!
Nimesoma vichwa vya habari kwenye magazeti kuwa mali za Lugunm zakamatwa akidaiwa kodi ya zaidi ya bil 14 na TRA.
Mie naona tunapiga sarakasi huku tukiwa tumevaa taulo.
Nijuavyo mimi anapoomba tenda kaiwaida lazima awe na tax clearence toka TRA ndo upewe tenda kuashiria hudaiwi kodi ili usije tumie pesa ya mradi kulupia madeni hasa kodi na tozo mbalimbali.
Iweje leo ndani ya miaka 3 awe anadaiwa zaidi ya bilioni 14 kwa biashara ipi anayofanya huyu Lugumi.
Kumshitaki kwa kosa la ufidlsadi inaonekana kuna watu serikalini wataguswa hasa toka chama kileeee. Ili ionekane anakufa nayo kama Lugumi wamekuja na njia nyingine kuwapumbaza wananchi
Hili jipu naona liko kwenye paji la uso inamaana mtumbuaji halioni? Au kwakuwa ni kampuni toka kanda maalum
Wanadamu hatuna jema. Ni humu humu JF tumemkosoa Mkulu kwa kutowachukulia hatua akina Lugumi. Now, the man is trying and here we come....eti ni maigizo.
Aise mtu akikuchukia hata ufanye nini wallah! Mbele yake utakuwa ni ziro tuu.
Tanzania imevamiwa na kizazi cha hovyo sanaWanadamu hatuna jema. Ni humu humu JF tumemkosoa Mkulu kwa kutowachukulia hatua akina Lugumi. Now, the man is trying and here we come....eti ni maigizo.
Aise mtu akikuchukia hata ufanye nini wallah! Mbele yake utakuwa ni ziro tuu.
Hahaha Haa watu Hata mungu anakazi aisee!!hata akishitakiwa mtasema anaonewa ....nyumbu kwa kugeuka geuka ni hatari sana.
Watakuja tena kudai wanapinga juhudi za mh Rais jamani tuelewa mada vizuri mkuu umeelezea vyemawatu wanaona maigizo kwasababu haieleweki hiyo kodi ya bilion 14 ni kwa biashara ipi hasa,ndo maana watu wanaona kuna usanii hapa,
afterall lugumi scandal yake haikuwa kukwepa kodi unless labda kama serikali ilimlipa yale mabilion halafu wakasahau kumdai kodi,na kama wanamdai kodi sasa ina maana yale malipo aliyolipwa kwa tenda ya fingerprint machine yalikuwa malipo halali
Mitandao ya kijamii inaonyesha baadhi ya Watanzania hata hawajui watakalo.Wanadamu hatuna jema. Ni humu humu JF tumemkosoa Mkulu kwa kutowachukulia hatua akina Lugumi. Now, the man is trying and here we come....eti ni maigizo.
Aise mtu akikuchukia hata ufanye nini wallah! Mbele yake utakuwa ni ziro tuu.
Kama na wee hujui kuwa anafanya biashara gani ýa kudaiwa ela hiyo basivnaee pia huna haja ya kulaumu basiHabari wadau!