albert_daud
Member
- Aug 26, 2015
- 21
- 26
Tanzania ni moja ya nchi ambazo huduma za kununua na kulipia ving'amuzi zinafanyika kwa kasi sana, hasa baada ya ushindani kuongezeka miaka kadhaa nyuma kutoka kampuni moja ambayo ilitawala soko kupata ushindani kutoka kwenye kampuni mpya zilizoanzishwa hasa moja ambayo ukuaji wake umechangiwa kwa kiasi kikubwa na kuonyesha na mpira wa ndani na tamthilia na nyingine kutokana na gharama zake kuwa nafuu na kuenea maeneo mengi ya nchi.
Wote tutakubaliana kwamba ushindani uliopo kwa namna fulani umeleta nafuu kwenye gharama za kulipia visimbuzi vyetu ukiachana na gharama za awali kabla ya ushindani sasa tumekua tukishuhudia ofa mbalimbali makampuni yakishindana yote kuonyesha wapi wanahuduma nzuri na zinapatikana kwa bei rahisi.
Turudi kwenye Hoja yangu ya msingi "MALIPO YA VING'AMUZI YAWE KWA NAMNA MTUMIAJI ANAVYOTUMIA"
tumekua tukipata huduma kwa kulipia visimbuzi vyetu kwa muda fulani "wengi kila mwezi" lakini tumekua tukipata changamoto kwamba kama umelipia kifurushi cha mwezi basi haijalishi kama kwa mwezi huo umetumia mara ngapi.
Mfano: Unaweza lipia kifurushi leo lakini bahati mbaya umepata safari mwezi mzima au hata masiku kadhaa hauko nyumbani au hata kutumia kifurushi chako kwa njia simu au kifaa chochote, lakini ukifika ule muda wa kifurushi kuisha basi kinaisha unalazimika kununua tena.
Kwanini usiwepo utaratibu wa malipo ya vifurushi yatokane na muda ambao mtumiaji kalipia, kama kalipia kifurushi cha mwezi basi isiwe kwa maana ya kuhesabu tarehe bali iwe kwa maana ya matumizi yake.
Teknolojia sasa imekua naimani inawezekana kabisa kila king'amuzi kuonyesha kimekua wazi kwa matumizi kwa muda gani.
Kwa maana inaweza kuwa king'amuzi kiuzwe kwa mfumo wa masaa na masaa hayo yanahesabika pale tu king'amuzi kinapokuwa kimewasha au kama mfumo huu huu wa week au mwezi basi kuhesabu matumizi yake iwe ni pale ambapo ambapo mteja anatumia.
Kwa maana nyingine iwe kama ambavyo sasa inafanyika kwenye umeme uniti za umeme zinatumia pale tu ambapo umeruhusu matumizi ya umeme, kama umeondoka hujaacha kifaa cha umeme kinafanya kazi basi ukirudi uniti zako unazikuta kama zilivyo unaendelea na matumizi.
Nawasilisha
Asanteni.