Malipo ya ving'amuzi yawe kwa namna mtumiaji anavyotumia

Kwa hio huko Nigeria ,South pia Ile huduma ya PPV( PAY PER VIEW )NI KUBWA?Ni sera tu ya nchi ikiwekwa Sawa linawezekana wenzetu wameanza mda sana na ni huduma nzuri na sio chonganishi ,mfano Jana game ya man u tu kupitia mfumo huo wenzio wamelipia na game ilipoisha ka kifurushi nako kakaisha,Je mkuu kama ulijilipua compact (nusu laki ongeza buku nne) target ikiwa man u Jana Leo unapambana na huba au unaicheki marudio.
 
Zimbabwe si Azam TV ipo?

Kifurushi cha juu cha Azam ni bei ya chini sna uki compare na Tanzania
 
Hii ni realistic? Huna familia? Huna watoto? Wageni wakija...so imagine at least kila siku, siku nzima (Masaa 6 kwa siku) unalipa pay per view
 
Hujamwelewa jamaa. Rudia kusoma tena maana kwa spidi hiyo usije jikwaa ukatuangukia humu.
 
Mkuu mawazo yako kinzani na yangu nayaheshimu sana hatuwezi wote kuwaza jambo moja au kuona kwa jicho moja jambo fulani
Wala haionyeshi ujinga wa mtu kuhoji tofauti na mitazamo ya wengine
 
Hii ni realistic? Huna familia? Huna watoto? Wageni wakija...so imagine at least kila siku, siku nzima (Masaa 6 kwa siku) unalipa pay per view
Na ndio mana ya kuwekwa Kwa option zote kwamba wewe wa familia ubaki na normal package wazee wa kuonekana usiku tutalipia chetu hiko
 
Umesema vyema Mkuu
Sera ya nchi ndo itayomnyonya mtumia au ndo itayomtetea mtumiaji
 
Kwa Tanzania bado Sana mkuu
Ni sera tu Mkuu mwaka mmoja au miezi kadhaa ni mingi sana kwa teknolojia kikubwa sera tu
Mfano sisi bado tv ya 4k tunavimba wakati kuna simu ina 8k au tayari kuna simu za 6g zinatoka.
Sera tu Mkuu linawezekana
 
Mimi ningeonelea nako kuwe na Bufee kama ya TTCL unajipimia idadi ya channel unataka. Na bei yako
Na ilipiwe kwa kuzingatia watch time.

Different bundles
 
Tukitaka tuwalipe kwa muda tunaoangalia tuu ..hasara tutapata sisi coz wanaweza ongeza option ya kulipia channel moja moja ...tofauti na sasa ambavyo ukilipia kwa mwez unapata channel zote ambazo ziko kwenye package husika

Kumbuka kadri unavozidi kumpa condition service provider ndivo anavozidi kuweka limit kwa kila service atakayokua anaitoa

Mfano kuna ile umechoka kutazama channel moja unahama channel nyingine ..hapa pia wanaweza kutumia hii kibiashara kwamba kwa kila channel utakayotaka kubadilisha kuna parcent flan itabidi ulipie kwanza ndo channel husika ifunguke.

Haiwezekani mtu alipie muda atakaokua anaangalia tuu afu awe free kubadili badili channel lazima kungekua na additional charges kwa kila unaposhika remote ya king'amuzi kutaka either kubadili channel ,au kuna wale wanataka kurecord vipind ili kuangalia baadaye ( kwa watumiaji wa DSTV Explorer) hapa pia ingekua lazima ulipie

Kuna channel ambazo zinapendwa sana hizi pia wangeweza kuongeza charges mfano Maisha magic bongo , channel za mpira, Movies n.k

Kuna swala la quality hapa pia wangeweza kuifanya kibiashara swala La HD bei yake na normal bei yake

Ukija swala la Advertisiment hapa ndo wangetunyoosha hatari yan wangehakikisha Matangazo yanakua mengi, ie yanachukua muda mwingi kuliko vipindi ili tuu muda wa mtu kutazama vipindi uongezeke , Mfano hzi Tamthilia zetu wangepunguza muda wa kuzionyesha kwa kuongeza matangazo so utajikuta unatumia muda mwingi kutazama kipind kimoja

Ukija kwenye muda wa kuangalia Tv wanafaham kuwa watu wengi wanapenda kutazama tv usiku na siku za weekend hapa pia ni fursa kwao package ya kuangalia tv usiku na siku za weekend ingekua kubwa kuliko package ya kuangalia tv asubuh au mchana ambao watu weng asilimia kubwa hawako nyumbani

Mpangilio wa vipindi
Hapa wangehakikisha vipindi vizuri wanaweka muda ambao wanaju wako majumbani lakini bei ingekua tofauti na vipind vya kawaida

Mfano channel za mpira wangeweza kuongeza bei ya channel husika ..let say game ni kali afu wako half time wanaweza wakaweka option ya kulipia additional charges ili uone kipindi cha pili
Swala la uchambuzi wangeweza litenga kulipia bei yake ,

Ingekua mimi ndo service provider afu nipewe masharti magumu katika utoaji wangu wa huduma ...ningeset a very complicated limit kwa kila service ambayo naitoa
 
Ni sera tu Mkuu mwaka mmoja au miezi kadhaa ni mingi sana kwa teknolojia kikubwa sera tu
Mfano sisi bado tv ya 4k tunavimba wakati kuna simu ina 8k au tayari kuna simu za 6g zinatoka.
Sera tu Mkuu linawezekana
Duh mkuu simu ina 8k ma hiyo 6G mkuu embu acha uongo mzee hiyo teknolojoa hata testing haijafanyika kwani uongo unakusaidia nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…