Malisa GJ: Mchanganuo wa Fedha za Simba na Yanga una utata

Malisa GJ: Mchanganuo wa Fedha za Simba na Yanga una utata

Nahisi hii hoja imeibuliwa kimkakati sasa hivi kuwavuruga viongozi na mashabiki wa Simba kuelekea gemu la Wydad.

Nina yangu ya kusema kuhusu hili ila nikiyasema nitaingia kwenye mtego kama wengine mlivyoingia.
 
Nahisi hii hoja imeibuliwa kimkakati sasa hivi kuwavuruga viongozi na mashabiki wa Simba kuelekea gemu la Wydad.

Nina yangu ya kusema kuhusu hili ila nikiyasema nitaingia kwenye mtego kama wengine mlivyoingia.
Kichwa ukikijaza Usimba na Yanga hata ajadiliwe Mwakinyo utahisi wanaijadili timu yako.
 
Mwaka 2013 au 2014 kama sikosei nilikuwa kiongozi wa Timu moja pale Mpanda Katavi inaitwa Katavi Worriors. Timu ilikuwa mshindi wa Mkoa ikawa inacheza Ligi ya Mabingwa Kanda. Kwa kuwa timu ni ya mtaani tulikuwa tunqombq misaada mtaani kwenda kucheza Mikoa Mingine.

Nakumbuka tulienda kucheza mechi na Ujenzi Rukwa kule kwao. Tulipotoka kule tukaja Cheza Mpanda kwenye ule uwanja wa Kashauriri. Uwanja ule ulikuwa na uzio Upande mmoja, tukahamasisha Mashabiki pamoja na sisi viongozi tukaenda kukata miti, tukatafuta maturubai huko mitaani then tukazungushia maturubai ili mashabiki watoe viingilio nasi tupate fedha za kuendeshea timu. Wakati tunahangaika, tuliwashirikisha viongozi wa chama cha soko Mkoa wa Katavi na Wilaya ya Mpanda watusaidie wakasema hawana msaada tuangalie namna gani tutafanya.

Eehhh bwana, tumefanikiwa kuzungusha maturubai, siku ya mechi tunaambiwa Chama cha Soko Wilaya ya Mpanda ndio kitasimamia ulinzi na kuchukua viingilio mlangoni. Tukawa kimya maana tulijipanga tuweke watu wengi wasimamie viingilio mlangoni.

Baada ya mechi tukaitwa viongozi na tukaambiwa viingilio vimepatikana 1,980,000/=. Wakaanza makato na migao pale. Huyu Karia kipindi hiko alikuwa Mkurugenzi wa Mahindano Nyanda za juu kusini. Hahaaaaaa, jamaa wakatuambia viongozi tusaini 13,500 ndio mapato tunayostahili. Nilimtukana sana yule Bwege na nilikataa kusaini hizo pesa nikamwambia kamnunulie mkeo ch.....i. hadi sasa ukiniambia uongozi wa Mpira Tz nakutukana. Jamaa wanachowaza ni matumbo yao na familia zao kwa jasho la wengine. Si unaona sasa alivyo na litumbo likubwa. Pumbavu kabisa yule msomali.

Malisa yupo sahihi kabisa kwa hili. Bila kujali gharama za kuendesha timu, wao wanachoangalia wanapata nini ili usiku wakahonge au kunywea bia. Nchi hii ni ngumu sana asikwambie mtu.
 
Kichwa ukikijaza Usimba na Yanga hata ajadiliwe Mwakinyo utahisi wanaijadili timu yako.
Wewe amini unachoamini. Inawezekana hauielewi nchi hii vizuri. Ngoja uone taarifa hizi zitakavyoathiri idadi ya mashabiki hapo kesho pamoja na kwamba ni sikukuu ndiyo utanielewa.
 
Karia na wapambe wake, ni wapigaji tu pale TFF. Hilo halina ubishi.

Ila inasikitisha pia kuona miaka nenda timu kubwa na kongwe kabisa nchini za Yanga na simba kukosa viwanja vyao binafsi. Yaani timu za juzi tu kama Azam Fc, Ihefu Fc, Namungo Fc, Mtibwa Fc, JKT Tanzania, nk. Vina viwanja vyao

Lakini ukija kwa hivi vilabu vikuu na vikongwe nchini! Kila siku viongozi wao wanaleta tu porojo. Viwanja kama hivyo vya Taifa, Huru, nk. Vilitakiwa kutumika kwenye timu za Taifa, nk.

Kama Yanga na simba wangekuwa wanamiliki viwanja vyao vya michezo, huo wizi na hayo makato yasiyo na kichwa wala miguu; yasingekuwepo.
Hata kama watakuwa na uwanja wao makato yatakayo pungua hapo ni gharama za uwanja tu.
 
Back
Top Bottom