Malkia Amanirenas: Shujaa wa kiafrika aliyeishinda dola ya Kirumi

Malkia Amanirenas: Shujaa wa kiafrika aliyeishinda dola ya Kirumi

zitto junior

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2013
Posts
20,537
Reaction score
31,729
Kwa ufupi tu Malkia Candace Amanirenas ama KENDAKE alikuwa malkia wa ethiopia ya kale yaani KUSH EMPIRE ambayo kwa kipindi hicho utawala wa meroe ulikuwa Sudan ya sasa.

Alitawala kuanzia 40 BC mpaka 10 BC. Alijizolea umaarufu mkubwa baada ya kuwa kiongozi imara mwanamke shujaa ambaye aliweza kuitawala dola kubwa bila mfalme hivyo kujijengea heshima kubwa.

Mwanamama huyu alikuwa na jicho moja tu baada ya jingine kuwa limetoboka wakati wa moja ya vita na warumi ila pamoja na hayo bado alikuwa na uwezo mkubwa sana kwenye uwanja wa vita na alipigana kishujaa bila uoga.

images (39).jpg


UMAARUFU WAKE

Alijizolea umaarufu baada ya kuiongoza KUSH kwenye vita iliyodumu kwa miaka 5 yaani 27-22 BC dhidi ya Roman empire waliokuwa wameitawala dunia ya wakati huo na kwa muda huo walikuwa wameitawala misri.

Baada ya vita kali wazungu hao walipigwa na kufurushwa kutoka misri ya kusini kwa kuteka miji muhimu ya Syrene, Philae, na Elephantina, ila baadae warumi wakajipanga na wakarudi vitani na walipoona vita inawadhoofu mwishoni wakaamua kuheshimu mipaka ya wakush hao na wakasaini mkataba wa amani hivyo ushindi huu uliodhihirisha nguvu ya mtu mweusi kupinga ubeberu na ubabe wa wazungu.

Ni tukio la kishujaa sana na limemzolea mwanamama huyu umaarufu mkubwa ukizingatia Dola ya Rumi ilikuwa ndio yenye nguvu na kuogopeka sana wakati huo ni sawa na Marekani ya sasa.

HITIMISHO
Ingawa historia za namna hii hazifundushwi mashuleni tunaishia kufundishwa tu kuhusu ukoloni na jinsi tulivyopigwa kwenye majimaji resistance!!!

Ni wakati umefika sasa historia za namna hii zitunzwe na kuelezwa ili waafrika tuache kuwa na inferiority complex kwa wazungu na kuaminishwa hakuna tunaloweza wakati miaka ya nyuma tuliwahi kuwa na falme zetu zenye dola kamili inayojiendesha kwa mifumo thabiti bila kuomba misaada kwa wazungu.

AFRIKA TUAMKE

Wenye kujua zaidi kuhusu malkia huyu wa shoka mtiririke tuzidi kujifunza

13184376.png
 
Last edited by a moderator:
Historia nzuri sana mkuu, nitarudi ngoja nikusanye nondo, maana huyu simuoni kwenye kile kitabu changu pendwa.
Sorry mkuu zitto junior huyu Malkia Candace au Kandake ametajwa kwenye kitabu changu pendwa Biblia, MATENDO 8:27. Nitarudi kudadavua kwa undani kidogo.
 
Last edited:
Historia nzuri sana mkuu, nitarudi ngoja nikusanye nondo, maana huyu simuoni kwenye kile kitabu changu pendwa.
Sawa mkuu ila ingawa biblia haijamtaja kandake amanirenas moja kwa moja ila naona jina lake halikuachwa nyuma.

Matendo 8:27
27 Naye akaondoka, akaenda; mara akamwona mtu wa Kushi, towashi, mwenye mamlaka chini ya Kandake malkia wa Kushi, aliyewekwa juu ya hazina yake yote; naye alikuwa amekwenda Yerusalemu kuabudu
 
Du mkuu, mm nikisikia habari iliyotokea BC huwa anaishiwa nguvu kabisa...na nilivyokuwa sipendi somo la historia hata sijamaliza kusoma story yote. Anyway, hongera zake malkia kwa ujasiri mkubwa.
 
Vile wazungu wanaizungumzia Africa na Waafrica huwezi amini kuna vitu kama hivi viliwahi tokea kwenye hili bara na vinatajika!


MALAIKA ANAONGEA NA FILIPO (mstari 26-26)


“Ondoka ukaende upande

wa kusini njia ile itelemkayo toka Yerusalemu kwenda Gaza; ambako ni jangwa”
naye Filipo alitii

haraka sana na haukuwa muda mrefu alielewa ni kwanini Mungu alimtuma huko. Mtu maarufu kutoka

Ethiopia alisafiri njiani. Huyu alikuwa ni towashi aliyekuwa afisa na mkuu wa hazina ya Kandake

Malkia wa Kushi. Ingawa mwethiopia huyu alimwamini BWANA Mungu wa Israeli na alikuwa

Yerusalemu kuabudu na alipokuwa akirejea nyumbani akiwa ameketi garini, alikuwa akisoma chuo

cha nabii Isaya. Mungu akamwambia Filipo “Sogea karibu na gari hili ukashikamane nalo”.
 
Vile wazungu wanaizungumzia Africa na Waafrica huwezi amini kuna vitu kama hivi viliwahi tokea kwenye hili bara na vinatajika!


MALAIKA ANAONGEA NA FILIPO (mstari 26-26)


“Ondoka ukaende upande

wa kusini njia ile itelemkayo toka Yerusalemu kwenda Gaza; ambako ni jangwa” naye Filipo alitii

haraka sana na haukuwa muda mrefu alielewa ni kwanini Mungu alimtuma huko. Mtu maarufu kutoka

Ethiopia alisafiri njiani. Huyu alikuwa ni towashi aliyekuwa afisa na mkuu wa hazina ya Kandake

Malkia wa Kushi. Ingawa mwethiopia huyu alimwamini BWANA Mungu wa Israeli na alikuwa

Yerusalemu kuabudu na alipokuwa akirejea nyumbani akiwa ameketi garini, alikuwa akisoma chuo

cha nabii Isaya. Mungu akamwambia Filipo “Sogea karibu na gari hili ukashikamane nalo”.

Corrections,
Kandake lilikuwa siyo jina la mtu.
Bali ni cheo cha malkia wa nchini Kushi/Sheba/Meroe ni sawa na kusema Farao tu.
 
Last edited:
Mkuu zitto junior kwenye hii vita Amanirenas alipigana na Wagiriki siyo Warumi.
Alipigana na Mfalme Alexander mkuu wa Makedonia baada ya kuvamia Egypt (Kemet) karne ya 332 BC.
Prof John Henrik Clarke ndiyo aliyeandika vizuri hili tukio na kusema kwenye vita Amanirenas alitolewa jicho moja.
Kwenye mkataba wa Amani aliwatishia wajumbe wa Alexander kwamba akirudi tena atamkata kichwa na kukutundika juu.

Jambo jingine muhimu kukumbuka ni kwamba huyu siyo wa kwanza kupigana na mataifa makubwa.
Wakushi wa zamani/Wasudan/Waethiopia/Wasomali wa leo walivamiwa na mfalme Cambyses (Mtoto wa Koreshi Mkuu) wa Umedi na Uajemi lakini wao pia walimshinda. Waajemi walikuwa hawana utaalamu wa kupigana vita kwenye jangwa na mlimani, sasa ukisoma vizuri historia wanakwambia Wakushi ndiyo walikuwa wataalamu wa kupiga mishele. Wakushi walijificha kwenye mchanga wa jangwa na waajemi walivyochoka walianza kuwapiga mishale. Wenyewe wanasema walikuwa na shabaha wakawa wanalenga kichwani na machoni tu. Waajemi baada ya kuzidiwa wakaamua kukimbia.

Baada ya hii vita Wafalme wa Misri na Uajemi walikuwa wanakuja kuwakodi wapiga mishale kutoka kwenye Kush kwenda kupigana vita zao. Mfalme Dario na Ahasuero (Artaxerxes) walikuwa wanafanya hivi sana......

Soma hapa:Cambyses - Encyclopedia
 
Last edited:
Back
Top Bottom