Malkia Amanirenas: Shujaa wa kiafrika aliyeishinda dola ya Kirumi

Malkia Amanirenas: Shujaa wa kiafrika aliyeishinda dola ya Kirumi

Hivi unajua alieficha hii historia ya watu weusi kwa kiasi kikibwa ni Kanisa Katoliki chini ya Papa Julius wa Pili ???
Alimtuma Michael Angelo achore upya michoro ya Yesu mzungu na mama yake, na siyo kutumia ile michoro ya zamani al maarufu kama The Black Madonna. Akawadanganya waumini wake kwamba sanamu la Black Madonna lilikuwa jeupe lakini kuna nyota ilishuka karne ya 16 na kubadilisha sanamu kuwa jeusi. Haya ni maneno ya Dr Yosef ben Jochannan

Hata hivyo naomba nikuulize swali lifuatalo:
Hivi kwanini Wakatoliki mnamwabudu Yesu Mzungu ??? Ndugu Kudo na zitto junior naomba mtusaidie hapa.

NB: Hili ni siyo swali la kidini bali la kihistoria, sawa na kusema Mtume Muhammad S.A.W alikuwa na wake wangapi.
Aseee hili swali zito sana ngoja nisubiri kwanza mkatoliki pure Da'Vinci na SALA NA KAZI walijibu kwanza
 
historia ya kinjeketile ngwale huijui, unatuletea za watu wa nje
Shida ya historia za ndani hazitunzwi hata ukitaka kuisoma hujui unaipatia wapi wala unaanzia wapi ila wenzetu wana maktaba kubwa za mitandaoni zenye historia za mashujaa wao ndio maana ni rahisi kupata hizi historia..... Changamoto ndio hiyo
 
Sijui ni lini ngozi nyeusi tutarudi kuwa na nguvu hivi maana rasilimali zote tunazo na nguvu kazi tunazo ila kuna eneo tulipwaya hadi kuacha mwanya kwa hawa wazungu kutuburuza mpaka leo ila naamini ni jambo la wakati tu tukijitambua na kurudi katika misingi yetu ya asili bila ya kuendeshwa na western mentality and leadership style pamoja na kuungana tutarudi tunapotakiwa kuwa

Unapozungumzia matatizo ya mtu mweusi huwezi kabisa kuacha madhara ya dini za Wazungu na Waarabu.
Waislamu na Wakristo ni moja ya sababu kubwa sana kwenye matatizo ya Afrika lakini huwa tunawaacha nje na kukazania Biashara ya Utumwa na Ukoloni pekee. Ili kuelewa vizuri historia ni lazima uweka kila kitu mezani na uanze kuchambua kitu kimoja baada ya kingine. Waislamu wenye asili ya Kiarabu walivamia Afrika mnamo karne ya saba (7) na kuanza kueneza dini kwa makali ya upanga; watu weusi wengi walikufa kwa makali ya upanga na tamaduni za Kiafrika nyingi sana zilipotea. Leo hii ukienda nchi za Maghreb unakuta waarabu tu na wengine wanajitanabaisha kwamba wao ndiyo waliojenga mapiramidi ya Misri na kuiletea dunia yetu mbinu za Kilimo na umwagiliaji , Ujenzi, Utabibu, Hesabu, Utengenezaji wa meli na Ubaharia. Mwanahistoria wa Kigiriki Herodotus anasema kwamba Mafarao walikuwa wanajua sana kufanya safari za baharini kwa namna ambayo hajawahi kuona.

Wengine ni Wakristo wa Ulaya.
Ambao wao waliona njia nyepesi kabisa ya kutawaala mtu ni kutumia imani. Maana baada ya dola la mrumi kuanguka mnao karne ya nne: Dunia nzima ilishuhudia ulaya ikiingia katika kipindi cha The Dark Age, ambapo kulikuwa hakuna maendeleo makubwa sana na Kanisa ndiyo lilikuwa limeshika hatamu. Mpaka kuifikia Mkatabwa wa Westphalia 1648 hadi karne ya 18 hadi 19 (The Renaissance) watu waliopanza kutumia akili zao kufikiria na kuanza kujitenga na uongo wa kidini ndipo Ulaya ikapiga hatua kubwa sana kwenye viwanda na mwishowe kutawala dunia nzima. Wazungu walikuja na mbinu zilezile zilizotumiwa na Kanisa Katoliki kutawala Ulaya kipindi chote cha The Dark Ages, wakaleta dini kwa nguvu kwa mwafrika. Wakasema majina na tamaduni zenu ni za kishenzi , wakaleta hadi na sala maalumu kwa ajili ya washenzi wote wa Afrika. Sasa lile giza la Ulaya la kutokea Karne ya 4 hadi 18 likahamia Afrika na ndiyo Bara letu likaitwa The DARK CONTINENT.

Lakini leo hii wasomi wa Afrika walioko kwenye dini haya hawayaoni na wanarusha makombora kwa mzungu tu na kuacha dini zao pembeni. Trans-Atlantic Slave Trade ilifanywa na Waarabu wa Wafalme wa Kiislamu waliokuwa wanavamia jamii za kishenzi (Makafiri) na kuanza kuwauza kwa wazungu hasahasa Wafanyabiashara kutoka Uholanzi. Afrika ilipoteza nguvu kazi kubwa sana na rasilimali nyingi na mwishowe ikavaa tamaduni zisizokuwa za kwake. Hili ni tatizo kubwa sana kwa Afrika, leo hii mwafrika akiishi kama Muitalia, Marekani, Myahudi au Muarabu anasema ndiyo anafuata dini.

Kuna mambo mengi sana ambayo tunayafuata kwenye dini lakini kiukweli siyo mafundisho ya Kiroho bali ni tamaduni za Waitalia au Waarabu. Kama kuvaa kanzu kulikuwepo hata kabla Mtume hajazaliwa, hivyo siyo dini bali ni sehemu ya tamaduni ambayo imevaana na dini. Makanisa ya Kiafrika kuanzia yale ya waorthodoksi wa Abyssinia yalikuwa tofauti kabisa na makanisa ya kiroho ya leo hii ambayo yana masharti lukuki ambayo mimi sijawahi kuyaelewa hata siku moja.

NB: Mtu mweusi asipojifunza kutenga uongo wa mapokeo ya kidini na ukweli wake binafsi, ataishi miaka yake yote akiamini kwamba Wayahudi, Wazungu na Waarabu wako bora kuliko yeye na ndivyo maulana alivyoumba hii dunia. Ataridhika na kubweteka na kuamini tamaduni zake ni ushenzi kama ilivyo hii leo. Ndiyo maana Uchina na Korea baada ya vita ya pili ya dunia mwaka 1945 waliamua kuchoma moto kila aina ya upuuzi wa kijapan na wazungu na kupiga marufuku kabisa mafundisho ya kipuuzi ambayo yanahubiri kwamba kuna jamii fulani ni bora kuliko nyingine.

Tuna safari ndefu sana kufika tunakotakiwa kwasababu mpaka sana sisi hatujui hata tunakoenda.....
Ila hizi Dini za Mzungu na Mwarabu zimechangia sana kudumaa akili mtu mweusi......
 
Last edited:
historia ya kinjeketile ngwale huijui, unatuletea za watu wa nje
Hivi kuna maandiko mangapi yaliyotukuka ambayo wanazuoni wa kitanzania wamendika kuhusu Ngwale ???
Wametingwa sana kuandika historia za CCM na TANU, Sultani wa Zanzibar, Wazee wa Dar es Salaam na nani jinsi gani Nyerere aliwafanyia dhulma waislamu waliopigani uhuru wa Tanganyika. Tena wengine wanaenda mbali sana kuleta upumbavu wa kudiriki kusema kwamba Kabla ya Sultani Seyyid said Zanzibari kulikuwa hakuna ustaarabu na kwamba Waarabu wa kiislamu ndiyo wameleta ustaarabu pwani ya Afrika Mashariki. AU kwa lugha rahisi Zanzibar ndiyo kitovu cha ustaarabu hapa Mashariki ya Afrika. Hivi hawa wanaosema hivi wana tofauti gani na wale wapumbavu waliosema kwamba mzungu ndiye aliyegundua Mlima Kilimanjaro ??? utafikiri wakati huo wachagga walikuwa hawaishi pale (Stupid, really stupid)

NB: Haya hebu taja vitabu nondo 10 vya kitanzania ambavyo vinamzungumzia vilivyo mzalendo kinjekitile Ngwale.
 
Last edited:
Sina uhakika sana kama alikuwa na mme kwa alivyokuwa mwanamke wa shoka kama alikuwa na mme basi "alipata tabu sana" 😀😛
HAKUNA WANAWAWAKE WALAINI KAMA WANAWAKE WANOONEKANA NA WANAUME WENGINE KUWA NI WAGUMU!
chukua hiyo na usiiiache !
huyo akifika kwa jamaa yake hakiiiiii hutaamini alivyo meek and mesmerized!
 
Mekeda au Bilkis alitawala kipindi ambacho ufalme wa Sheba ulikuwa ndiyo unatawala hadi ufalme wa Misri.
Ndiyo maana alivyoenda kwa Suleimani alitambulishwa kama Malkia wa Misri na Sheba. Mekeda alienda kumjaribu Mfalme Suleimani kwasababu kipindi hicho kabla ya Suleimani kuwa mfalme, yeye ndiyo alikuwa anasifika kwa Utajiri na Akili nyingi hapa duniani. Kwenda kule alichokiona kilimfanya abaki mdomo wazi tu na kwasababu alikuwa hana mwanaume akaona ni vyema kabisa azae na Suleimani ndiyo wakamzaa Mfalme Menelik I au David II.

Ikumbukwe mfalme Suleimani mbali na kuwa na mali nyingi sana.
Sehemu kubwa ya utajiri wake ilikuwa ni Urithi kutoka kwa baba yake Mfalme Daudi. Lile hekalu na kasri lake la kifalme vilikuwa ni utajiri ulioachwa na Daudi. Mfano mzuri tu Daudi alianga madini ya thamani kwa ajili ya kujengea hekalu ambapo katika kiwango cha leo gharama yake ilikuwa ni 20 Billion USD ambazo ni sawa na Trillion 40 na ushee (Bajeti ya nchi kwa miaka 2 hivi). Sasa Malkia wa Sheba kuona haya akawa mpole tu. Nebukadrezza na Farau walivyovamia Israel walipata utajiri mwingi sanaaa.

Huyo Cleopatra huwa simhesabii sana kama Malkia wa Afrika kwasababu alikuwa ni Mgiriki.
Baada ya Alexander kufa na ufalme wake kugawanyika vipande vinne, jemedari wa Alexander aitwaye Ptolemy ndiyo alipewa Misri (Kemet) atawale. Sasa Cleopatra ni mzao wa Ptolemy ndiyo maana mimi huwa sipendi kumchukulia kama mmisri asilia. Japo hata hivyo zaidi ya kutumia ngono kuwalaghai wanaume wa Kirumi alikuwa hana cha ziada kama hawa wakina Mekeda na Amanirenas.
mkuu hizi jamii zilikuwa ni nyeusi au walionekanaje.Malcolm lumumba.
 
mkuu hizi jamii zilikuwa ni nyeusi au walionekanaje.Malcolm lumumba.
Waethiopia na Wamisri walikuwa ni weusi.
Lakini kuna wasomi wanadiriki kudanganya na kusema kwamba "Egyptians were not white, but were neither black"
Sasa unabaki unashangaa tu, hivi hawa watu wana akili mbovu kiasi gani. Sijui watu weusi tuliwakosea nini hawa wazungu na waarabu. Maana zamani majina ya nchi yalikuwa yanaelezea vizuri sifa za eneo au watu: Mfano mzuri kabisa jina la Misri ya zamani lilikuwa ni Kemet likimaanisha mchanga mweusi uliongua au nchi ya watu waliongua mikuu.

Neno Egypt limekuja baadae kabisa kwasababu wagiriki walikuwa wanachanganya jina la mji moja ya miji mikubwa ya kibiashara iliyokuwepo huko Kemeti. Sasa huo mji ulikuwa unaitwa Aigyptos na wagiriki likawakaa neno Aigyptos ndiyo Egypt likatokea.
Lakini kiarabu maana ya neno Egypt ni Misr ambalo linatokana na jina la mjukuu wa Nuhu aliyekuwa anaitwa Mizrahimu. Mizrahimu alikuwa ni mtoto wa Ham (Baba wa weusi) na ndugu yao na wakina Kush na Put.

Ethiopia ni neno linaoleezea sifa za watu lakini mwanzoni kabisa Ethiopia ilikuwa ni ufalme wa Abyssinia.
Neno Ethiopia linatokana na meneno ya Kigiriki Aitho kumaanisha aliyeungua na Ops likiminaanisha uso. Hivyo neno Ethiopia maana yake ni mtu aliyeaungua uso (Mweusi). Herodotus alisema aliwakuta Ethiopians hadi barani Ulaya sehemu za vilima vya Caucasus.

Majina ya zamani yalikuwa yanatumika kuelezea sifa za eneo.
Mfano Yerusalem maana yake mji wa amani "Yeru" inasimama kwa Maji na Salem/Salam ni Amani.
Dar es Salama nayo inaelezea sifa za eneo kuwa ni bandari salama kama waarabu walivyoiita.
Sasa sijui mnataka ushahidi upi ili muachane na hizi nadhari za "Baada ya Mungu ni Mzungu"
 
Last edited:
Waethiopia na Wamisri walikuwa ni weusi.
Lakini kuna wasomi wanadiriki kudanganya na kusema kwamba "Egyptians were not white, but were neither black"
Sasa unabaki unashangaa tu, hivi hawa watu wana akili mbovu kiasi gani. Sijui watu weusi tuliwakosea nini hawa wazungu na waarabu. Maana zamani majina ya nchi yalikuwa yanaelezea vizuri sifa za eneo au watu: Mfano mzuri kabisa jina la Misri ya zamani lilikuwa ni Kemet likimaanisha mchanga mweusi uliongua au nchi ya watu waliongua mikuu.

Neno Egypt limekuja baadae kabisa kwasababu wagiriki walikuwa wanachanganya jina la mji moja wa kibiashara wa
watu wanahangaika kutafuta shetani misikitini na makanisani bila kujua waliozianzisha hizo nyumba za ibada ndio mashetani wenyewe.
 
Hakuwa na mme
Historia inaonesha kuwa alikuwa na Mumewe aliyeitwa Mfalme Teriteqas, na anaonekana kuwa mchungaji wa malkia mpaka kufa kwake. Pia walikuwa na mtoto wao wa kiume akiitwa Mwana mfalme Akinidad mkuu wa taji (crown prince)

Inaaminika kuwa mara baada ya kufariki kwa Teriteqas mwanzoni mwa vita inasemekana ndipo Amanirenas na Akinidad walifanikiwa kurithi na kukaa kwenye kiti cha enzi.
 
Last edited:
watu wanahangaika kutafuta shetani misikitini na makanisani bila kujua waliozianzisha hizo nyumba za ibada ndio mashetani wenyewe.
Mzee Jomo Kenyatta (R.I.P) aliwahi kusema hivi:
"When the white-men came, we had the land and they had a Bible. They said close your eyes and lets pray.
When we opened up our eyes they had the land and we had the Bible" Shetani anaishi kwenye nyumba za ibada tangu kipindi Yesu aliposema "Nyumba ya baba yangu haitakuwa ni pango la wanyang'anyi" Washika dini ndiyo wanaongoza kwa kurudisha bara letu nyuma kimaendeleo kwa mafundisho yao potofu. Hili ushahidi wake ni mkubwa sana na haihitaji kuwa na PhD ili kuyaona
 
Last edited:
Hivi unajua alieficha hii historia ya watu weusi kwa kiasi kikibwa ni Kanisa Katoliki chini ya Papa Julius wa Pili ???
Hapana sifahamu, ilikuaje? Kwanini alificha aisili ya watu weusi? Naomba maelezo mkuu
Hivi kwanini Wakatoliki mnamwabudu Yesu Mzungu ??? Ndugu [alikuwa na wake wangapi.
Mkuu kwani kwa mujibu wa historia Yesu alikua Race gani? Na wa taifa lipi?
Hatumuabudu Yesu mzungu, Tunamuabudu Yesu Kristo mkuu
 
Duuuh hii jf mpyaa nashindwa kukata Quote. Msaada please
 
Back
Top Bottom