Kusema ukweli mambo ni mengi sana ambayo tunapaswa kuyajua lakini bahati isio kua njema hatuyajui.
Shukrani kwako mleta mada kila siku nakupa saluti kwa mchango wako hapa JF haswa Jamii intelligence.
Lakini pia shukrani za kipekee kwa wadau kwa michango ambayo inaipa mada husika thamani.
Kwa habari ya huyu mwana mama ni moa kati ya wanawake wachache waliofanya kitu chakipekee tofauti na na wengine na kuondoa ile dhana ya mwanamke ni kuzaa na kulea tuu, japokua jukumu hilo kamwe kwa mwanamke halimkwepi.
Lakini pia tunazidi kujua africa si kama vile tulioamniashwa kwenye vitabu vya historia. Nadhani sasa ni wakati wa africa kuamka pale tulipo angukia na kuendelea japo tumebaki nyuma sana lakini haitalingana na kuendelea kubakia hapa tulipo.
Mkuu
Malcom Lumumba kuhusu post yako #45 imeniacha njia panda japo imenitafakarisha sana kuhusu dini. Lakini sina la kusema maana mimi nimeamini na katka imani ninatumaini. Sasa inapokuja changamoto kama hii kuhusu dini maswali yakua kua mengi yasio na majibu.
Kama ndio hivyo ulivyosema je Mungu nafasi yake katika kuzuia hilo iko wapi? au ndio kusema ni idhini yake iwe hivyo? kwa sisi africa tudanganywe kuhusu yeye? Na mwisho wa huu uwongo utakua ni lini?
Nipende kuwatakieni kila jema na wepesi katika mambo yote. Tusichoke kuhabarishana chochote tukipatacho bila kuchoka huwenda siku moja haitakua hivi ilivyo leo.