Malkia Amanirenas: Shujaa wa kiafrika aliyeishinda dola ya Kirumi

Malkia Amanirenas: Shujaa wa kiafrika aliyeishinda dola ya Kirumi

Mkuu kuhusu imani kupotoshwa na Mungu kuruhusu nafkiri alishatuasa kwenye biblia kuhusu kuja kwa manabii wa uongo ambao watapotosha misingi ya imani na kweli na watatupeleka katika kuamini imani zisizo sahihi hivyo ni kazi kwetu sisi tunaofuata imani hizi kutambua ipi ipo kwenye msingi wa imani na ipi imekengeuka ili tusije kujikuta tunaongozwa na makanisa ya manabii wa uongo waliokuja kupotosha imani yetu huo ndio mtazamo wangu

Cc Son of Gamba
Zitto junior, Ipi imani iliyo sahihi, na ipi haiko sahihi hebu nisaidie hapo
 
Zitto junior, Ipi imani iliyo sahihi, na ipi haiko sahihi hebu nisaidie hapo
Imani sahihi ni kumuabudu Mungu wa kweli if at all unaamini Mungu yupo kama mimi ila hizi dini ingawa zina nia moja ila procedure zao ndio zinatofautiana na ndio zimetuletea matatizo makubwa sisi wanadamu hadi kutufikisha hapa tulipo hadi wengine kuitumia kutugawa na kututawala
 
Sawa mkuu ila ingawa biblia haijamtaja kandake amanirenas moja kwa moja ila naona jina lake halikuachwa nyuma.

Matendo 8:27
27 Naye akaondoka, akaenda; mara akamwona mtu wa Kushi, towashi, mwenye mamlaka chini ya Kandake malkia wa Kushi, aliyewekwa juu ya hazina yake yote; naye alikuwa amekwenda Yerusalemu kuabudu
mkuu hizi ndondo nimezikubali sana. ila timing za utawala wa huyu mama kwa mujibu wa bandiko lako, na mwaka wa huyu mkushi anabatizwa ilikuwa ni ACE 33+ , ila umenifungua akili sana maana ni wiki hii tu tulikuwa tunajifunza kuhusu huyo jamaa lakini Kandake sikuwahi kudhani ni kitu chenye kuchukua umakini na chenye kina kikubwa kiasi hicho.
Hongera sana mkuu. binafsi nimebarikiwa na hii kitu.
 
Last edited:
Mkuu zitto junior kwenye hii vita Amanirenas alipigana na Wagiriki siyo Warumi.
Alipigana na Mfalme Alexander mkuu wa Makedonia baada ya kuvamia Egypt (Kemet) karne ya 332 BC.
Prof John Henrik Clarke ndiyo aliyeandika vizuri hili tukio na kusema kwenye vita Amanirenas alitolewa jicho moja.
Kwenye mkataba wa Amani aliwatishia wajumbe wa Alexander kwamba akirudi tena atamkata kichwa na kukutundika juu.

Jambo jingine muhimu kukumbuka ni kwamba huyu siyo wa kwanza kupigana na mataifa makubwa.
Wakushi wa zamani/Wasudan/Waethiopia/Wasomali wa leo walivamiwa na mfalme Cambyses (Mtoto wa Koreshi Mkuu) wa Umedi na Uajemi lakini wao pia walimshinda. Waajemi walikuwa hawana utaalamu wa kupigana vita kwenye jangwa na mlimani, sasa ukisoma vizuri historia wanakwambia Wakushi ndiyo walikuwa wataalamu wa kupiga mishele. Wakushi walijificha kwenye mchanga wa jangwa na waajemi walivyochoka walianza kuwapiga mishale. Wenyewe wanasema walikuwa na shabaha wakawa wanalenga kichwani na machoni tu. Waajemi baada ya kuzidiwa wakaamua kukimbia.

Baada ya hii vita Wafalme wa Misri na Uajemi walikuwa wanakuja kuwakodi wapiga mishale kutoka kwenye Kush kwenda kupigana vita zao. Mfalme Dario na Ahasuero (Artaxerxes) walikuwa wanafanya hivi sana......

Soma hapa:Cambyses - Encyclopedia
ubarikiwe mkuu.
 
Mekeda au Bilkis alitawala kipindi ambacho ufalme wa Sheba ulikuwa ndiyo unatawala hadi ufalme wa Misri.
Ndiyo maana alivyoenda kwa Suleimani alitambulishwa kama Malkia wa Misri na Sheba. Mekeda alienda kumjaribu Mfalme Suleimani kwasababu kipindi hicho kabla ya Suleimani kuwa mfalme, yeye ndiyo alikuwa anasifika kwa Utajiri na Akili nyingi hapa duniani. Kwenda kule alichokiona kilimfanya abaki mdomo wazi tu na kwasababu alikuwa hana mwanaume akaona ni vyema kabisa azae na Suleimani ndiyo wakamzaa Mfalme Menelik I au David II.

Ikumbukwe mfalme Suleimani mbali na kuwa na mali nyingi sana.
Sehemu kubwa ya utajiri wake ilikuwa ni Urithi kutoka kwa baba yake Mfalme Daudi. Lile hekalu na kasri lake la kifalme vilikuwa ni utajiri ulioachwa na Daudi. Mfano mzuri tu Daudi alianga madini ya thamani kwa ajili ya kujengea hekalu ambapo katika kiwango cha leo gharama yake ilikuwa ni 20 Billion USD ambazo ni sawa na Trillion 40 na ushee (Bajeti ya nchi kwa miaka 2 hivi). Sasa Malkia wa Sheba kuona haya akawa mpole tu. Nebukadrezza na Farau walivyovamia Israel walipata utajiri mwingi sanaaa.

Huyo Cleopatra huwa simhesabii sana kama Malkia wa Afrika kwasababu alikuwa ni Mgiriki.
Baada ya Alexander kufa na ufalme wake kugawanyika vipande vinne, jemedari wa Alexander aitwaye Ptolemy ndiyo alipewa Misri (Kemet) atawale. Sasa Cleopatra ni mzao wa Ptolemy ndiyo maana mimi huwa sipendi kumchukulia kama mmisri asilia. Japo hata hivyo zaidi ya kutumia ngono kuwalaghai wanaume wa Kirumi alikuwa hana cha ziada kama hawa wakina Mekeda na Amanirenas.
Kweli mkuu
 
TUANSHUKURU SANA ILA NA NYIE WAALIMU NA WATU WA KWENYE SEKTA YA ELIMU, MNATAKIWA KULITAZAMA ILI JAMBO KWA JICHO LINGINE KAMA NILIVO GUSIA HAPO AWALI KUWA MATATIZO YA ELIMU HAYAPO KWA WATOTO ILA MITAALA YETU HAYA HUKU CHINI NI KUFUNDISHANANI UWOGA NA UDHAIFU(INFERIORITY) HUWEZI TENGENEZA MASHUJAAA WENYE UHURU WA AKILI NA KIMAWAZO KAMA MIZIZI YAKE HUJENGWA KWA HISTORIA DHAIFU INAYOMWONESHA KUWA YEYE KAMWE KATIKA DUNIA HII WATU WAKE HAWAJAWAI KUTHUBUTU WALA KUSHINDA KITU.........INASIKITISHA SANA NA TUTAPATA TABU SANA MPAKA HAO WAZEE WA ENZI WA UKOLONI NA WENYE MINDSET YA KARNE YA 19 NA 20 WATOKE WALIKO NA WAACHIE WATU WENYE MAWAZO MAPYA KAMA KAGAME/MAGU WALAU.
Hivi magu nae yupo!
 
Kwa historia hiyo ina maanisha africa tuliwahi kuwa super power
Yawezekana hii historia tuliyosoma shule ya msingi na secondary ni kanyaboya,kuna mambo mengi bado tumefichwa!
Sijui wazungu walitupigaje bao
Ila nacho elewa Baada ya kuletewa biashara ya utumwa hapo ndipo tukaaribikiwa

Ova
 
Mambo kama haya ilibidi wafundishe mashuleni!syo historia tuliyosoma sisi iliyojaa uongo kumtukuza mtu mweupe na mwarabu,sijui fulani ndiyo kagundua Milima Kilimanjaro wakati pale kulikuwa na watu wanaishi ......
Malcolm lumumba@nimekuelewa sana Asante kwa nondo

Ova
 
Hivi unajua alieficha hii historia ya watu weusi kwa kiasi kikibwa ni Kanisa Katoliki chini ya Papa Julius wa Pili ???
Alimtuma Michael Angelo achore upya michoro ya Yesu mzungu na mama yake, na siyo kutumia ile michoro ya zamani al maarufu kama The Black Madonna. Akawadanganya waumini wake kwamba sanamu la Black Madonna lilikuwa jeupe lakini kuna nyota ilishuka karne ya 16 na kubadilisha sanamu kuwa jeusi. Haya ni maneno ya Dr Yosef ben Jochannan

Hata hivyo naomba nikuulize swali lifuatalo:
Hivi kwanini Wakatoliki mnamwabudu Yesu Mzungu ??? Ndugu Kudo na zitto junior naomba mtusaidie hapa.

NB: Hili siyo swali la kidini bali la kihistoria, sawa na kusema Mtume Muhammad S.A.W alikuwa na wake wangapi.
Upo nje ya mada kabisa ianzishie uzi
 
Upo nje ya mada kabisa ianzishie uzi
Labda wewe ndiyo hujaelewa vizuri mada mkuu.
Mto maada amezungumzia mambo makubwa mawili hapa:
1. Malkia wa kushi na jinsi alivyomshinda Alexander Mkuu
2. Kufichwa kwa historia ya mtu mweusi kwa maslahi ya mtu mweupe (Papa Pius alikuwa mweupe)

NB: Utasemaje niko nje ya mada wakati nimezungumzia haya yote kwa pamoja???
 
Back
Top Bottom