Kwenye falsafa ya Ujerumani hata kabla ya Hitler kuwepo kuna kitu wanakiita The Volk-Geist wakimaaisha Volk kama People na Geist ni Spirit/Ghost. Hii falsafa inadai kwamba ili mtu ailewa Ujerumani ni lazima awe ni mtu wa jamii hiyo. Wakina Von Savigny ndiyo waliipigia sana debe hii kitu.
Falsafa hii ndiyo ilitumiwa kusema kwamba the Germany command of good art is Ruined by the Jewish art. Na haikuishia hapo tu, hadi kwenye sheria wakaleta kitu kinatwa Historical Jurisprudence na mambo mengine mengi tu.
Baada ya vita ya pili ya dunia hii falsafa ilipigwa marufuku kwasababu ndiyo iliwafundisha wajerumani ubaguzi na kujenga mazingira ya kuwepo watu kama Adolf Hitler.
NB: Bahati mbaya sanaa, mimi nilifundishwa hii kitu darasani na nikafanyia kabisa mtihani. Siyo ya kutisha sana lakini inajenga dhana kwamba jamii moja haitakiwi kabisa kuingiliana na nyingine.