Malkia Amanirenas: Shujaa wa kiafrika aliyeishinda dola ya Kirumi

Malkia Amanirenas: Shujaa wa kiafrika aliyeishinda dola ya Kirumi

Kwa ufupi tu Malkia Candace Amanirenas ama KENDAKE alikuwa malkia wa ethiopia ya kale yaani KUSH EMPIRE ambayo kwa kipindi hicho utawala wa meroe ulikuwa Sudan ya sasa.

Alitawala kuanzia 40 BC mpaka 10 BC. Alijizolea umaarufu mkubwa baada ya kuwa kiongozi imara mwanamke shujaa ambaye aliweza kuitawala dola kubwa bila mfalme hivyo kujijengea heshima kubwa.

Mwanamama huyu alikuwa na jicho moja tu baada ya jingine kuwa limetoboka wakati wa moja ya vita na warumi ila pamoja na hayo bado alikuwa na uwezo mkubwa sana kwenye uwanja wa vita na alipigana kishujaa bila uoga.

View attachment 819834

UMAARUFU WAKE

Alijizolea umaarufu baada ya kuiongoza KUSH kwenye vita iliyodumu kwa miaka 5 yaani 27-22 BC dhidi ya Roman empire waliokuwa wameitawala dunia ya wakati huo na kwa muda huo walikuwa wameitawala misri.

Baada ya vita kali wazungu hao walipigwa na kufurushwa kutoka misri ya kusini kwa kuteka miji muhimu ya Syrene, Philae, na Elephantina, ila baadae warumi wakajipanga na wakarudi vitani na walipoona vita inawadhoofu mwishoni wakaamua kuheshimu mipaka ya wakush hao na wakasaini mkataba wa amani hivyo ushindi huu uliodhihirisha nguvu ya mtu mweusi kupinga ubeberu na ubabe wa wazungu.

Ni tukio la kishujaa sana na limemzolea mwanamama huyu umaarufu mkubwa ukizingatia Dola ya Rumi ilikuwa ndio yenye nguvu na kuogopeka sana wakati huo ni sawa na Marekani ya sasa.

HITIMISHO
Ingawa historia za namna hii hazifundushwi mashuleni tunaishia kufundishwa tu kuhusu ukoloni na jinsi tulivyopigwa kwenye majimaji resistance!!!

Ni wakati umefika sasa historia za namna hii zitunzwe na kuelezwa ili waafrika tuache kuwa na inferiority complex kwa wazungu na kuaminishwa hakuna tunaloweza wakati miaka ya nyuma tuliwahi kuwa na falme zetu zenye dola kamili inayojiendesha kwa mifumo thabiti bila kuomba misaada kwa wazungu.

AFRIKA TUAMKE

Wenye kujua zaidi kuhusu malkia huyu wa shoka mtiririke tuzidi kujifunza

Asante umenikumbusha mbali kwa nini Ethiopia ni moja ya nchi Africa ambayo haikutawaliwa
 
Kushi ni sudan au ethiopia?
Kush ni jamii ya wethiopia wa kale waliwahi tawala mashariki ya kati na baadae misri na sudan na mwishoni wakasettle ethiopia ya sasa hivyo wakush ni jamii ya ki-hamiti yaani ethiopia djibouti Eritrea somalia n.k ila kwa kipindi hiki cha Amanirenas walikuwa bado wanaitawala sudan (Nubia) na misri ya enzi hizo kupitia 25th dynasty ambayo ilitoa mafarao weusi wa kicush

Sijui nmejibu swali lako
 
Africa ya sasa wamama mashujaa ni too scarce, ila wakitokea wanakuwa vzr sana refer Elen Johnson Sallif
 
Kwa ufupi tu Malkia Candace Amanirenas ama KENDAKE alikuwa malkia wa ethiopia ya kale yaani KUSH EMPIRE ambayo kwa kipindi hicho utawala wa meroe ulikuwa Sudan ya sasa.

Alitawala kuanzia 40 BC mpaka 10 BC. Alijizolea umaarufu mkubwa baada ya kuwa kiongozi imara mwanamke shujaa ambaye aliweza kuitawala dola kubwa bila mfalme hivyo kujijengea heshima kubwa.

Mwanamama huyu alikuwa na jicho moja tu baada ya jingine kuwa limetoboka wakati wa moja ya vita na warumi ila pamoja na hayo bado alikuwa na uwezo mkubwa sana kwenye uwanja wa vita na alipigana kishujaa bila uoga.

View attachment 819834

UMAARUFU WAKE

Alijizolea umaarufu baada ya kuiongoza KUSH kwenye vita iliyodumu kwa miaka 5 yaani 27-22 BC dhidi ya Roman empire waliokuwa wameitawala dunia ya wakati huo na kwa muda huo walikuwa wameitawala misri.

Baada ya vita kali wazungu hao walipigwa na kufurushwa kutoka misri ya kusini kwa kuteka miji muhimu ya Syrene, Philae, na Elephantina, ila baadae warumi wakajipanga na wakarudi vitani na walipoona vita inawadhoofu mwishoni wakaamua kuheshimu mipaka ya wakush hao na wakasaini mkataba wa amani hivyo ushindi huu uliodhihirisha nguvu ya mtu mweusi kupinga ubeberu na ubabe wa wazungu.

Ni tukio la kishujaa sana na limemzolea mwanamama huyu umaarufu mkubwa ukizingatia Dola ya Rumi ilikuwa ndio yenye nguvu na kuogopeka sana wakati huo ni sawa na Marekani ya sasa.

HITIMISHO
Ingawa historia za namna hii hazifundushwi mashuleni tunaishia kufundishwa tu kuhusu ukoloni na jinsi tulivyopigwa kwenye majimaji resistance!!!

Ni wakati umefika sasa historia za namna hii zitunzwe na kuelezwa ili waafrika tuache kuwa na inferiority complex kwa wazungu na kuaminishwa hakuna tunaloweza wakati miaka ya nyuma tuliwahi kuwa na falme zetu zenye dola kamili inayojiendesha kwa mifumo thabiti bila kuomba misaada kwa wazungu.

AFRIKA TUAMKE

Wenye kujua zaidi kuhusu malkia huyu wa shoka mtiririke tuzidi kujifunza

@zitto junior uko deep hadi unaboa, Congratulations to you.
 
Sawa mkuu ila ingawa biblia haijamtaja kandake amanirenas moja kwa moja ila naona jina lake halikuachwa nyuma.

Matendo 8:27
27 Naye akaondoka, akaenda; mara akamwona mtu wa Kushi, towashi, mwenye mamlaka chini ya Kandake malkia wa Kushi, aliyewekwa juu ya hazina yake yote; naye alikuwa amekwenda Yerusalemu kuabudu
Hao wanaotajwa hapo ni wanyiramba na wanyaturu sio waethiopia hao mnaowaona Leo.

OVER.
 
Vile wazungu wanaizungumzia Africa na Waafrica huwezi amini kuna vitu kama hivi viliwahi tokea kwenye hili bara na vinatajika!

MALAIKA ANAONGEA NA FILIPO (mstari 26-26)

“Ondoka ukaende upande

wa kusini njia ile itelemkayo toka Yerusalemu kwenda Gaza; ambako ni jangwa”
naye Filipo alitii

haraka sana na haukuwa muda mrefu alielewa ni kwanini Mungu alimtuma huko. Mtu maarufu kutoka

Ethiopia alisafiri njiani. Huyu alikuwa ni towashi aliyekuwa afisa na mkuu wa hazina ya Kandake

Malkia wa Kushi. Ingawa mwethiopia huyu alimwamini BWANA Mungu wa Israeli na alikuwa

Yerusalemu kuabudu na alipokuwa akirejea nyumbani akiwa ameketi garini, alikuwa akisoma chuo

cha nabii Isaya. Mungu akamwambia Filipo “Sogea karibu na gari hili ukashikamane nalo”.
Kumbe magari sio kitu kipya, babu alinambia kitu chochote chenye jina la lugha ya kiswahili au kibantu wazungu wamekikuta kwetu, magari tulikuwa nayo sisi,
 
Mekeda au Bilkis alitawala kipindi ambacho ufalme wa Sheba ulikuwa ndiyo unatawala hadi ufalme wa Misri.
Ndiyo maana alivyoenda kwa Suleimani alitambulishwa kama Malkia wa Misri na Sheba. Mekeda alienda kumjaribu Mfalme Suleimani kwasababu kipindi hicho kabla ya Suleimani kuwa mfalme, yeye ndiyo alikuwa anasifika kwa Utajiri na Akili nyingi hapa duniani. Kwenda kule alichokiona kilimfanya abaki mdomo wazi tu na kwasababu alikuwa hana mwanaume akaona ni vyema kabisa azae na Suleimani ndiyo wakamzaa Mfalme Menelik I au David II.

Ikumbukwe mfalme Suleimani mbali na kuwa na mali nyingi sana.
Sehemu kubwa ya utajiri wake ilikuwa ni Urithi kutoka kwa baba yake Mfalme Daudi. Lile hekalu na kasri lake la kifalme vilikuwa ni utajiri ulioachwa na Daudi. Mfano mzuri tu Daudi aliacha madini ya thamani kwa ajili ya kujengea hekalu ambapo katika kiwango cha leo gharama yake ilikuwa ni 20 Billion USD ambazo ni sawa na Trillion 40 na ushee (Bajeti ya nchi kwa miaka 2 hivi). Sasa Malkia wa Sheba kuona haya akawa mpole tu. Nebukadrezza na Farau walivyovamia Israel walipata utajiri mwingi sanaaa.

Huyo Cleopatra huwa simhesabii sana kama Malkia wa Afrika kwasababu alikuwa ni Mgiriki.
Baada ya Alexander kufa na ufalme wake kugawanyika vipande vinne, jemedari wa Alexander aitwaye Ptolemy ndiyo alipewa Misri (Kemet) atawale. Sasa Cleopatra ni mzao wa Ptolemy ndiyo maana mimi huwa sipendi kumchukulia kama mmisri asilia. Japo hata hivyo zaidi ya kutumia ngono kuwalaghai wanaume wa Kirumi alikuwa hana cha ziada kama hawa wakina Mekeda na Amanirenas.
USD 20 billions??? Wakati biblia inasema Selemani alikuwa na utajiri wa dhahabu zenye uzito wa tani 666.

Ikiwa na maana amekamilika, bado ng'ombe bado mbuzi na kondoo, ambapo kuna sherehe 1 tu alichinja Ng'ombe 20,000 na kondoo 120,000 huyu utajiri wake ni zaidi ya USD 1000bilions
 
Nimezungumzia mali alizoachiwa na Mfalme Daudi (baba yake) kwa ajili ya ujenzi wa hekalu.
 
Nimezungumzia mali alizoachiwa na Mfalme Daudi (baba yake) kwa ajili ya ujenzi wa hekalu.
Nimekuelewa haswaa, ila jamaa alikuwa tajiri sana. Na ninasikia alimgawia huyo mama sehemu ndogo Sana ya utajiri ndiyo maana Ethiopia ina nguvu toka zaman sana, pia ule utajiri Israel ilipovamiwa Warumi walibeba dhahabu na fedha yote wakaenda kununua plot pale Italy kwenye mji wa Roma na kujenga ngoma ya Vatican, sijui mwenye taarifa kamili ajazie hapa, ila asili ya Katoliki ni warumi,
 
Pamoja sana mkuu, ni muhimu sana kujikumbusha hizi historia zetu
Ni kweli Mkuu nimekuwa nimepata mengi sana na weekend hii nikiwa nimetulia Home na bundle langu kuna baadhi ya post na zipitia km hili la uwongozi wa marekali Bado lina ni changanya juu ya uwongoz wao kidg
 
Back
Top Bottom