Malkia Elizabeth kalala kuzimu. Je, karma itachukua mkondo wake?

Malkia Elizabeth kalala kuzimu. Je, karma itachukua mkondo wake?

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Dibaji
Karma ni imani ya kilimwengu ya kipagani na waamini miungu. Lcha ya kuwa ni imani lakini pia ni kanuni yenye kuakisi uhalisia. Kwamba baya hulipwa kwa baya na jema hulipwa kwa jema.

Kiwango cha mabaya ama mema ndio kitaamua utakuwa nani maisha yako ya baadae ama yajayo! Hakuna kitu msamaha kwenye hii kanuni ya kipagani HAKUNA
Mwisho wa dibaji.

Malkia Elizabeti aliyelala kuzimu jana mwenye imani ya Kikristo ya Kianglikana inayoamini katika msamaha wa dhambi, kuokoka na kufufuliwa siku ya mwisho (kama ipo) ni mmojawapo wa binadamu aliye iishi pepo akiwa duniani tangu kuzaliwa hadi kufa.

Kwa tafsiri nyepesi ni kwamba pesa kwake haikuwa tatizo na alipata chochote alichotaka kwa matamanio ya kawaida ya kibinadamu na hata yale ya ziada.

Kila alichotaka alikipata kwa wakati na kwa tani yake.. Na ni mambo machache mno aliyafanya kwa mikono yake mwenyewe kwakuwa maisha yake yote alizungukwa na watumishi tena wa kaliba ya juu mno. Maana alikuwa ni malkia wa taifa lenye nguvu na ukwasi duniani

Kwenye hii kanuni ya kiasili ya kilimwengu ya karma ni kwamba malkia Elizabeti maisha yake yaliyopita (karma inaamini katika reincarnation) kwamba kuna maisha kabla ya maisha na kuna maisha baada ya maisha.

Mama huyu aliishi maisha kabla ya haya akitenda mema mengi sana na ndio maana maisha haya yalijaa bata na faraja kuanzia kuzaliwa hadi kufa.. Kwamba yalikuwa ni malipo mema ya maisha yake yaliyopita.

Sasa basi baada ya maisha haya ya malipo mema aliendelea kufanya mema ama alijisahau na kutenda mabaya!? Kwa waafrika wengi anatajwa kama mtu dhalimu na katili, huko India pia hana jina jema. Biashara ya utumwa afrika ilimtia dosari kubwa, madhila mengi mabaya na magumu kabisa yaliyowapata watumwa yana vinasaba vyake. Mikono yake inanuka damu na maisha yake yalijaa udhalimu uliofichika.

Maono na maonyo ya karma yalijidhihiri ndani ya familia yake ya kifalme kuanzia tuhuma za kumuua Diana na maovu mengine lukuki kipindi chote cha uhai wake bila kusahau tuhuma za kusababisha baa la njaa India ili taifa lake liweze kuuza chakula.

Kwamba sasa maisha haya ya malipo mema alitengeneza karma mbaya itakayokuja kumuathiri vibaya katika maisha yake yajayo!

Karma hutanua makucha yake hata kwa wasiohusika moja kwa moja kwa maana ya wanafamilia. Hawa nao wanaweza kuathirika kwakuwa tu wana vinasaba na malkia.

Bila kujali kama kafa kwa imani yake ya Mungu mmoja na pengine kafanya kitubio cha mwisho kabla ya kukata roho lakini karma ni kanuni ya kiasili isiyojali msamaha wa kiimani.. Karma ni kafiri na kafiri hana msalie mtume! Ni vigezo na masharti tuu, cause condition and effect.

Unafique wa kibinadamu wa kutuma salam za pole na kuoneshwa kushtushwa na kifo cha malkia Elizabeth hazitamsaidia mwendazake kukiepuka kikombe cha karma.

Ila kwakuwa tunaishi kidiplomasia na kuuheshimu mwili uliolala basi sote kwa pamoja tunaungana na familia ya malkia Elizabeth katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao na mojawapo ya mtu muhimu sana duniani.

Sambamba na hili la kifo cha malkia Liz . nachukua nafasi hii pia kumpa mkuu PASKALI pole nyingi kwa kutochaguliwa kwenye kinyang'anyiro cha nafasi za uwakilishi wa kibunge ndani ya bunge la Afrika mashariki. PASKALI ni muumini na mwalimu mzuri wa karma
RIP QUEEN[emoji146] ELIZABETH mbele yako nyuma yetu.

giphy.gif
 
Kiwango cha mabaya ama mema ndio kitaamua utakuwa nani maisha yako ya baadae ama yajayo!
Maneno ya msingi sana Mshana Jr na ukweli usifaohamika kwa wengi. "Kama uliuza watumwa kwenye maisha haya, utazaliwa utumwani na kuuzwa kama mtumwa. Kama ulinyanyasa maskini na fukara, utazaliwa fukara, na kunyanyasika pia. Kama ulifanya abortion, you will be aborted by your parents in your next life"

Anything you do here, maybe paid here and hereafter, in this life or in your next life. Roho zetu zinahifadhi matendo yetu yote na kumbukumbu zote za maisha tuliyowahi kupitia.
 
Alikuwa ni mtumishi wa ngazi ya juu wa shetani akiwa na degree 33 za uchawi. Akivaa mavazi yenye nembo na mapambano ya kichawi vikiwemo crown, pete, ring, mikufu, vyeo. Huyu akutubu kabla ya kifo hawa uamini kwao shetani ni Mungu.
 
Watoto wa Malkia wana kamsemo kao
"Karma is a bitch...."

Hivi hua wanamaanisha nini mkuu maana maneno haya

Fafadua na hapo kidogo mkuu Mshana Jr
Nadhani wanasema 'life is a bitch'....
Ila kama ni hiyo yako nadhani wanamanisha kuwa karma ni kama Malaya (you dnt https://jamii.app/JFUserGuide her twice).
 
Back
Top Bottom