Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
MALKIA ELIZABETH NA VIONGOZI WA TAA 1953
Picha hiyo hapo chini ya Mwalimu Nyerere na Malkia Elizabeth imenirudisha nyuma sana hadi mwaka wa 1953.
Nimeitazama hiyo picha ya viongozi awa wawili nikaamua kufungua kitabu cha Abdul Sykes niangalie nimeandika nini kuhusu Mwalimu Nyerere na Malkia Elizabeth.
Siku chache zilizopita niliandika katika mtandao kuwa Nyaraka za Sykes zina jina la kila mtu alyehusika katika siasa za Tanganyika.
Kuna mtu alichukizwa na maneno yangu haya na akaniandikia maneno ya kifedhuli na kejeli lakini mimi kwa dhati na ukweli wa nafsi yangu nikawambia asidhani kuwa mimi natania nyaraka zile zina mambo mengi sana kuhusu harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika.
Sasa nilipoona picha hii ya Malkia akiwa na Mwalimu Nyerere wakati Malkia Elizabeth alipofanya ziara ya Tanzania mwaka wa 1979 nikasema hebu nifungue kitabu changu niangalie kuna nini kuhusu Malkia na Mwalimu Nyerere.
Ili uweze kupata historia yote vizuri inabidi nianze mwanzo wa maisha ya Julius Nyerere pale alipoingia katika siasa za Dar es Salaam na kuchaguliwa kuwa President wa TAA tarehe 17 April, 1953.
Tarehe 19 June, gazeti la Tanganyika Standard likachapa majina ya viongozi wa TAA kama ifuatavyo: J.K. Nyerere, President; Abdulwahid Sykes, Vice-President; J.P. Kasella Bantu, General Secretary; Alexander M. Tobias, Waziri Dossa Aziz, Joint Minuting Secretary; John Rupia, Treasurer, Ally K. Sykes Assistant Treasurer. Committee members Dr Michael Lugazia, Hamisi Diwani, Tewa Said, Denis Phombeah, Z. James, Dome Okochi, C. Ongalo na Patrick Aoko.
Katika Nyaraka za Sykes kuna barua iliyoandikwa na kwenda kwa Malkia Elizabeth isiyokuwa na tarehe iliyotiwa saini na viongozi wote wa TAA: Rais Julius Nyerere, Makamu wa Rais Abdulwahid Sykes, Katibu Mkuu Dome Okochi, Naibu Katibu Dossa Aziz, Mweka Hazina John Rupia, Naibu Mweka Hazina Ally Sykes ikimpongeza Malkia kwa kutawazwa kuwa Malkia wa Uingereza.
Katika barua hii jina la Dome Budohi ndilo linaloonekana kama Katibu Mkuu badala ya jina la Kasella Bantu kama lilivyotokea katika Tanganyika Standard.
Prof. Issa Shivji, Prof. Saida Yahya Othman na Dr. Ng’wazi Kamata waandishi wa kitabu cha maisha ya Julius Nyerere walipokuja kunihoji kuhusu Mwalimu niliwaonyesha barua hii.
Waliipenda sana na wakaniomba niwape nakala.
Nilipokuwa naiangalia picha hii ya Mwalimu Nyerere na Malkia Elizabeth nikawa najiuliza kama Malkia anakumbuka kuwa aliandikiwa barua na Mwalimu Nyerere mwaka wa 1953 akimpongeza kwa kutawazwa kuwa Malkia.
Sijui kama Malkia anaikumbuka barua hii.
Lakini nina uhakika ukienda Rhodes House Oxford barua hii itakuwapo.
Sasa tuje kwa Ally Sykes na ziara hii ya Malkia Tanzania mwaka wa 1979.
Ubalozi wa Uingereza ulifanya dhifa nyumbani kwake kwa heshima ya Malkia.
Ally Sykes ananihadithia.
Katika dhifa ile Julius Nyerere alikuwapo na mgeni wake na katika walioalikwa alikuwa Ally Sykes na mkewe Bi. Zainab.
Miaka mingi ilikuwa imepita na Ally Sykes, Bi. Zainab na Nyerere walikuwa hawajaonana kwa muda mrefu sana.
Walipokutana uso kwa uso Nyerere alimwambia Ally Sykes, ‘’Ally hawa Waingereza unakuja katika shughuli zao lakini shughuli zetu huonekani.’’
Ally Sykes akajibu, ‘’Hawa wananialika nyinyi hamnialiki mimi.’’
Mwalimu akacheka akamgeukia Bi.Zainab akamwambia, ‘’Bi. Zainab Ally hajabadilika karibu wewe Msasani.’’
Ally Sykes akaniambia baada ya siku ile hawakupata kuzungumza hadi Nyerere anakufa ingawa iko siku walikuwa ndege moja na viti jirani wote wakielekea London.
Hakuna kati yao aliyefanya juhudi ya kumsogelea mwenzake kumsalimu.
Hawa ni wanachama wawili ambao kadi zao za TANU zilifuatana.
Kadi no 1 Territorial President Julius Kambarage Nyerere kadi no.2 Ally Kleist Sykes.