kina kirefu
JF-Expert Member
- Dec 14, 2018
- 15,188
- 18,583
Nyerere alikuaje haongei nawezake au kwakua alikua mtu wakuja toka bara
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hebu niweke sawa hiyo hiyo dhifa (State Banquet) ya 1979 ilifanyika nyumbani kwa Ally Sykes au kwa Balozi wa Uingereza maana ulivyoandika inachanganya!MALKIA ELIZABETH NA VIONGOZI WA TAA 1953
Picha hiyo hapo chini ya Mwalimu Nyerere na Malkia Elizabeth imenirudisha nyuma sana hadi mwaka wa 1953.
Nimeitazama hiyo picha ya viongozi awa wawili nikaamua kufungua kitabu cha Abdul Sykes niangalie nimeandika nini kuhusu Mwalimu Nyerere na Malkia Elizabeth.
Siku chahe zilizopita niliandika katika mtandao kuwa Nyaraka za Sykes zina jina la kila mtu alyehusika katika siasa za Tanganyika.
Kuna mtu alichukizwa na maneno yangu haya na akaniandikia maneno ya kifedhuli na kejeli.lakini mimi kwa dhati na ukweli wa nafsi yangu nikawambia asidhani kuwa mimi natania nyaraka zile zina mambo mengi sana kuhusu harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika.
Sasa nilipoona picha hii ya Malkia akiwa na Mwalimu Nyerere wakati Malkia Elizabeth alipofanya ziara ya Tanzania mwaka wa 1979 nikasema hebu nifungue kitabu changu niangalie kuna nini kuhusu Malkia na Mwalimu Nyerere.
Ili uweze kupata historia yote vizuri inabidi nianze mwanzo wa maisha ya Julius Nyerere pale alipoingia katika siasa za Dar es Salaam na kuchaguliwa kuwa President wa TAA tarehe 17 April, 1953.
Tarehe 19 June, gazeti la Tanganyika Standard likachapa majina ya viongozi wa TAA kama ifuatavyo: J.K. Nyerere, President; Abdulwahid Sykes, Vice-President; J.P. Kasella Bantu, General Secretary; Alexander M. Tobias, Waziri Dossa Aziz, Joint Minuting Secretary; John Rupia, Treasurer, Ally K. Sykes Assistant Treasurer. Committee members Dr Michael Lugazia, Hamisi Diwani, Tewa Said, Denis Phombeah, Z. James, Dome Okochi, C. Ongalo na Patrick Aoko.
Katika Nyaraka za Sykes kuna barua iliyoandikwa na kwenda kwa Malkia Elizabeth isiyokuwa na tarehe iliyotiwa saini na viongozi wote wa TAA: Rais Julius Nyerere, Makamu wa Rais Abdulwahid Sykes, Katibu Mkuu Dome Okochi, Naibu Katibu Dossa Aziz, Mweka Hazina John Rupia, Naibu Mweka Hazina Ally Sykes ikimpongeza Malkia kwa kutawazwa kuwa Malkia wa Uingereza.
Katika barua hii jina la Dome Budohi ndilo linaloonekana kama Katibu Mkuu badala ya jina la Kasella Bantu kama lilivyotokea katika Tanganyika Standard.
Prof. Issa Shivji, Prof. Saida Yahya Othman na Dr. Ng’wazi Kamata waandishi wa kitabu cha maisha ya Julius Nyerere walipokuja kunihoji kuhusu Mwalimu niliwaonyesha barua hii.
Waliipenda sana na wakaniomba niwape nakala.
Nilipokuwa naiangalia picha hii ya Mwalimu Nyerere na Malkia Elizabeth nikawa najiuliza kama Malkia anakumbuka kuwa aliandikiwa barua na Mwalimu Nyerere mwaka wa 1953 akimpongeza kwa kutawazwa kuwa Malkia.
Sijui kama Malkia anaikumbuka barua hii.
Lakini nina uhakika ukienda Rhodes House Oxford barua hii itakuwapo.
Sasa tuje kwa Ally Sykes na ziara hii ya Malkia Tanzania mwaka wa 1979.
Ubalozi wa Uingereza ulifanya dhifa nyumbani kwake kwa heshima ya Malkia.
Ally Sykes ananihadithia.
Katika dhifa ile Julius Nyerere alikuwapo na mgeni wake na katika walioalikwa alikuwa Ally Sykes na mkewe Bi. Zainab.
Miaka mingi ilikuwa imepita na Ally Sykes, Bi. Zainab na Nyerere walikuwa hawajaonana kwa muda mrefu sana.
Walipokutana uso kwa uso Nyerere alimwambia Ally Sykes, ‘’Ally hawa Waingereza unakuja katika shughuli zao lakini shughuli zetu huonekani.’’
Ally Sykes akajibu, ‘’Hawa wananialika nyinyi hamnialiki mimi.’’
Mwalimu akacheka akamgeukia Bi.Zainab akamwambia, ‘’Bi. Zainab Ally hajabadilika karibu wewe Msasani.’’
Ally Sykes akaniambia baada ya siku ile hawakupata kuzungumza hadi Nyerere anakufa ingawa iko siku walikuwa ndege moja na viti jirani wote wakielekea London.
Hakuna kati yao aliyefanya juhudi ya kumsogelea mwenzake kumsalimu.
Hawa ni wanachama wawili ambao kadi zao za TANU zilifuatana.
Kadi no 1 Territorial President Julius Kambarage Nyerere kadi no.2 Ally Kleist Sykes.
Geza...Hebu niweke sawa hiyo hiyo dhifa (State Banquet) ya 1979 ilifanyika nyumbani kwa Ally Sykes au kwa Balozi wa Uingereza maana ulivyoandika inachanganya!
![]()
![]()
Kina...Nyerere alikuaje haongei nawezake au kwakua alikua mtu wakuja toka bara
Gold...Walowezi Wazulu watawezaje kudai Uhuru wa nchi ambayo siyo yao?
Wazee wangu wameishi Tanganyika miaka elfu na elfu.
Unawezaje kudai Uhuru wa nchi ambayo siyo yako ilhali ukoo mzima mmeletwa Tanganyika na Wajerumani kama mercenaries/askari wa kukodi wa hao Wajerumani, halafu baadaye unalalamika mmewekwa nje kwenye historia rasmi ya nchi? Na majina ya Kijerumani mmeyang'ang'ania vilevile.
Msiwe na uchungu na nchi isiyo ya mababu zako.Gold...
Haya uiyoandika ungeweza kuyaandika kwa lugha ya kiungwana na ungeeleweka bila shida.
Ukoloni una athari zake na tunaishinazo hadi leo.
Babu yangu mkuu Mwekapopo Muyukwa aliingia Tanganyika siku hizo German Ostafrika akitokea Belgian Congo akiwa amebeba bunduki kuja kuupa nguvu utawala wa Wajerumani.
Mtoto wake babu yangu Salum Abdallah yeye kazaiwa Shirati Bomani mama Mtusi.
Babu yangu kapigania uhuru wa Tanganyika na historia yake inaanza na African Association.
Kleist Sykes kama baba yangu baba yake aliingia Tanganyika kama askari na Kleist akazaiwa Pangani, baba Mzulu mama Mnyaturu.
Kleist akaunda African Association 1929 na watoto wake wakaunda TANU 1954 na wakapigania uhuru wa Tanganyika hadi ukapatikana.
Lakini kubwa John Iliffe mwaka wa 1968 ametumia baadhi ya nyaraka hizi kuandika historia ya African Association.
Mimi nimetumia Nyaraka za Sykes kuandika historia ya uhuru wa Tanganyika.
Akina Sykes hawako katika historia ya TANU iliyoandikwa na Chuo Cha CCM Kivukoni lakini wako katika Dictionary of African Biography (2011).
View attachment 2144917
Gold...Badala ya kutuletea umbeya huu, bora Mzee MS angejikita kusifia utanashati, utajiri na magari ya kifahari kama Mercedes Benz SE ya Sykes whoever (Can't tell the difference between them, and wouldn't care less which is which.) ya enzi hizo. Mzee mbeya wewe na mwongo, tunakujua vizuri. Tupe za Nyerere bila kumtaja Sykes. Kama kweli una weledi mkosoe Nyerere kwa lolote bila kuwataja hao Miungu Watu wako Sykes.
Gold...Msiwe na uchungu na nchi isiyo ya mababu zako.
Hao mababu zako wote wameingia Tanganyika kama askari wa kukodiwa wa Mkoloni Mjerumani.
Kaa kimya mzee.
Kuna Watanganyika asilia hawapigi kelele kuhusu mchango na juhudi za Wazee wao kudai Uhuru wa nchi yao asilia ya Tanganyika bila kujali dini zao.
nyumbani "kwake"? nani? Sykes? Archives zipo Baba Queen Elizabeth hawezi kuhudhuria State Banquet kwa Sykes wakati Ikulu Magogoni na High Commissioner Residency ipo! najua unataka kumaanisha hivyo ila ukweli upo online!Geza...
Rudia kusoma kwa utulivu utaelewa.
Ningeweza kukuambia lakini nataka utumie ubongo wako ili siku nyingine ikiwa hujaelewa kitu unarudia kusoma upya.
Geza...nyumbani "kwake"? nani? Sykes? Archives zipo Baba Queen Elizabeth hawezi kuhudhuria State Banquet kwa Sykes wakati Ikulu Magogoni na High Commissioner Residency ipo! najua unataka kumaanisha hivyo ila ukweli upo online!
Pitia Central Office of Information : London - Queen with President Nyerere. [Royal Visit to Tanzania, 1979]
sasa ulishindwa nini kunielewesha? na kama muelewa, kwake is a loose indicator! Kwake who? wakati sentence ya juu inaongelea Sykes? Wewe unafikiri kwanini Nyerere alipuuzia watu wa caliber na ego ya Sykes? Je, angewaendekeza, angeweza kuendesha nchi ipasavyo?Geza...
Hakika Malkia Elizabeth hawezi kualikwa nyumbani kwa mtu binafsi.
Soma tena kwa utulivu utaelewa.
Jitulize soma makala hiyo utaelewa.
Hapa barzani kila msomaji kaelewa hakuna hata mmoja aliyeniuliza hii dhifa ilifanyika wapi?
Hizi makala nazirusha kwenye Whatsapp na huko jamaa wanachangamka sana kwa maswali.
Hakuna aliyeniuliza hili swali lako.
Watu maarufu Ally Sykes aliowaalika nyumbani kwake ni Sidney Poitier, Harry Belafonte na Albert Rothschild.
Si Malkia wa Uingereza.
Nadhani sasa umeelewa.
Ahsante kwa link ila ningependa nikufahamishe kitu.
Nimeishi Wales na Scotland, nikija London mara nyingi na nilikuwa "Royal Watcher."
Huu ulikuwa wakati wa ujana wangu.
Nilijifunza mengi kuhusu House of Windsor.
Mimi si mgeni wala mjinga katika mambo haya.
Geza...Geza...
Hakika Malkia Elizabeth hawezi kualikwa nyumbani kwa mtu binafsi.
Soma tena kwa utulivu utaelewa.
Jitulize soma makala hiyo utaelewa.
Hapa barzani kila msomaji kaelewa hakuna hata mmoja aliyeniuliza hii dhifa ilifanyika wapi?
Hizi makala nazirusha kwenye Whatsapp na huko jamaa wanachangamka sana kwa maswali.
Hakuna aliyeniuliza hili swali lako.
Watu maarufu Ally Sykes aliowaalika nyumbani kwake ni Sidney Poitier, Harry Belafonte na Albert Rothschild.
Si Malkia wa Uingereza.
Nadhani sasa umeelewa.
Ahsante kwa link ila ningependa nikufahamishe kitu.
Nimeishi Wales na Scotland, nikija London mara nyingi na nilikuwa "Royal Watcher."
Huu ulikuwa wakati wa ujana wangu.
sasa ulishindwa nini kunielewesha? na kama muelewa, kwake is a loose indicator! Kwake who? wakati sentence ya juu inaongelea Sykes? Wewe unafikiri kwanini Nyerere alipuuzia watu wa caliber na ego ya Sykes? Je, angewaendekeza, angeweza kuendesha nchi ipasavyo?
Nilijifunza mengi kuhusu House of Windsor.
Mimi si mgeni wala mjinga katika mambo haya.
Tatizo unaishi kwenye nadharia ya fantasy world umerithishwa matarajio ya Sykes ambayo hayakutimia na kuishia kuwa manung'uniko na hisia za kudhulumiwa mpaka kihama chake! Tanganyika ilikuwa kubwa na isingeweza kuzunguka kwa vijana wa K'koo peke yao! Ukielewa hilo itakuwa na maono tofauti kichwani na amani moyoni.Geza...
Unazungumza umeghadhibika.
Huenda hata unaposoma kalamu yangu unakuwa umeghadhibika.
Ukiwa na hasira akili haifikiri sawasawa.
Sikutaka kukueleza mapema nilitaka nijifurahishe na wewe.
Katika pambano la Mohamed Ali na George Foreman, Kinshasa 1974 handlers wa Foreman waiamini ikifika round ya tatu Ali atakuwa keshapigwa na pambano limekwisha.
Ilipofika round ya tatu wakati wa mapumziko wale handlers wa Foreman wakawa wanampigia kelele Foreman wanamwabia, ''George finish him off!''
Daktari wa Ali Pacheco akawa anamwambia Ali, ''Ali unayasikia maneno hayo?''
Baada ya miaka mingi kupita Dr. Pacheco anaeleza anasema, ''Baada ya mimi kumwambia Ali naneno yale, Ali alinishangaza kwa kuniambia, ''Mimi huyu nampiga.''
Dr. Pacheco akamjibu Ali akamwambia, ''Mpige basi twende zetu nyumbani.''
Ali akajibu, ''Let us have some fun first.''
Sikutaka kukujibu kwa haraka nilitaka tuburudike.
Geza...Tatizo unaishi kwenye nadharia ya fantasy world umerithishwa matarajio ya Sykes ambayo hayakutimia na kuishia kuwa manung'uniko na hisia za kudhulumiwa mpaka kihama chake! Tanganyika ilikuwa kubwa na isingeweza kuzunguka kwa vijana wa K'koo peke yao! Ukielewa hilo itakuwa na maono tofauti kichwani na amani moyoni.
sasa mbona kila siku unaongelea maumivu ya Sykes? Mnampambanua kama serikali ya Nyerere ilimdhulumu? Au upeo wa kuelewa hisia zako wengine hatuna? Huyo Sykes ana tofauti gani na Machifu ambao waliathirika na serikali za Uchifu kufutwa na wakaacha yapite? Wahenga husema tenda wema uende zako!Geza...
Hapana si kweli wewe hutujui sisi.
Mimi babu yangu Salum Abdallah ni muasisi wa TANU Tabora 1954 na TRAU 1955 na haikuwa tegemeo lake kunufaika katika siasa.
Alikuwa mtu wa kujiweza na alitoa fedha zake katika kupigania uhuru wa Tanganyika.
Abdul Sykes hakuchukua siasa kama ajira halikadhalika Ally Sykes, Dossa Aziz na wengine wengi.
Hawa wameunda TANU kwa fedha zao na wakaijenga TANU kwa mali zao.
Wala mimi siishi katika ''fantasy world,'' kama unavyodhani.
Wala mimi sinung'uniki.
Mimi hapa nasomesha historia ya wazee wangu ili ifahamike na wapate heshima wanayostahili.
Haya uyasomayo hapa wewe hukuwa unayajua.
Huondoki hapa kwa kuwa unajua kuwa hapa ipo elimu ambayo wewe hukuwanayo kabla.
View attachment 2145208
Unalazimisha mambo Mzee.Geza...
Hapana si kweli wewe hutujui sisi.
Mimi babu yangu Salum Abdallah ni muasisi wa TANU Tabora 1954 na TRAU 1955 na haikuwa tegemeo lake kunufaika katika siasa.
Alikuwa mtu wa kujiweza na alitoa fedha zake katika kupigania uhuru wa Tanganyika.
Abdul Sykes hakuchukua siasa kama ajira halikadhalika Ally Sykes, Dossa Aziz na wengine wengi.
Hawa wameunda TANU kwa fedha zao na wakaijenga TANU kwa mali zao.
Wala mimi siishi katika ''fantasy world,'' kama unavyodhani.
Wala mimi sinung'uniki.
Mimi hapa nasomesha historia ya wazee wangu ili ifahamike na wapate heshima wanayostahili.
Haya uyasomayo hapa wewe hukuwa unayajua.
Huondoki hapa kwa kuwa unajua kuwa hapa ipo elimu ambayo wewe hukuwanayo kabla.
View attachment 2145208
Geza...sasa mbona kila siku unaongelea maumivu ya Sykes? Mnampambanua kama serikali ya Nyerere ilimdhulumu? Au upeo wa kuelewa hisia zako wengine hatuna? Huyo Sykes ana tofauti gani na Machifu ambao waliathirika na serikali za Uchifu kufutwa na wakaacha yapite? Wahenga husema tenda wema uende zako!