Malkia Elizabeth na Viongozi wa TAA, 1953

Nyerere alikuaje haongei nawezake au kwakua alikua mtu wakuja toka bara
 
Hebu niweke sawa hiyo hiyo dhifa (State Banquet) ya 1979 ilifanyika nyumbani kwa Ally Sykes au kwa Balozi wa Uingereza maana ulivyoandika inachanganya!




 
Hebu niweke sawa hiyo hiyo dhifa (State Banquet) ya 1979 ilifanyika nyumbani kwa Ally Sykes au kwa Balozi wa Uingereza maana ulivyoandika inachanganya!




Geza...
Rudia kusoma kwa utulivu utaelewa.

Ningeweza kukuambia lakini nataka utumie ubongo wako ili siku nyingine ikiwa hujaelewa kitu unarudia kusoma upya.
 
Nyerere alikuaje haongei nawezake au kwakua alikua mtu wakuja toka bara
Kina...
Uhuru ulipopatikana mwaka wa 1961 ulikuja na changamoto zake.

Nadhani umesoma hapa nikieleza kuwa Chuo Cha Kivukoni kilipoandika historia ya TANU jina la Abdul Sykes halikuwapo katika kitabu kilichochapwa mwaka wa 1981.

Hata Abdul Sykes alipofariki mwaka wa 1968 magazeti ya TANU - Uhuru na The Nationalist hawakuandika taazia ya kifo chake.

Mhariri wa magazeti haya alikuwa Benjamin Mkapa.
Kumbuka huyo ni mwanachama wa TANU mwenye kadi no. 3.

Zilikuja changamoto nyingi.
Halikuwa suala la watu wa pwani na bara.

TANU ilijengwa nchi nzima.
 
Gold...
Haya uiyoandika ungeweza kuyaandika kwa lugha ya kiungwana na ungeeleweka bila shida.

Ukoloni una athari zake na tunaishinazo hadi leo.

Babu yangu mkuu Mwekapopo Muyukwa aliingia Tanganyika siku hizo German Ostafrika akitokea Belgian Congo akiwa amebeba bunduki kuja kuupa nguvu utawala wa Wajerumani.

Mtoto wake babu yangu Salum Abdallah yeye kazaiwa Shirati Bomani mama Mtusi.
Babu yangu kapigania uhuru wa Tanganyika na historia yake inaanza na African Association.

Kleist Sykes kama baba yangu baba yake aliingia Tanganyika kama askari na Kleist akazaiwa Pangani, baba Mzulu mama Mnyaturu.

Kleist akaunda African Association 1929 na watoto wake wakaunda TANU 1954 na wakapigania uhuru wa Tanganyika hadi ukapatikana.

Lakini kubwa John Iliffe mwaka wa 1968 ametumia baadhi ya nyaraka hizi kuandika historia ya African Association.

Mimi nimetumia Nyaraka za Sykes kuandika historia ya uhuru wa Tanganyika.

Akina Sykes hawako katika historia ya TANU iliyoandikwa na Chuo Cha CCM Kivukoni lakini wako katika Dictionary of African Biography (2011).

 
Msiwe na uchungu na nchi isiyo ya mababu zako.

Hao mababu zako wote wameingia Tanganyika kama askari wa kukodiwa wa Mkoloni Mjerumani.

Kaa kimya mzee.

Kuna Watanganyika asilia hawapigi kelele kuhusu mchango na juhudi za Wazee wao kudai Uhuru wa nchi yao asilia ya Tanganyika bila kujali dini zao.
 
Gold...
Umeghadhibika na unatoa matusi na unachanganya na Kiingereza katika hamaki zako.

Mimi nasikitika kuwa kwa nini iwe hivi?

Mola wangu ni Allah Muumba mbingu na ardhi.

Mzee Kleist kafa mimi sijazaliwa lakini akiishi jirani na babu yangu Salum Abdallah Mtaa wa Kipata na New Street (sasa Kleist Sykes Street na Lumumba Avenue).

Mkewe Bi. Mruguru bint Mussa na bibi yangu Zena bint Farijallah walikuwa mashoga na watoto wao wakicheza pamoja na kusoma shule moja ya msingi Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika Muslim School katika miaka ya 1930s.

Hawa ni wazee wangu na mimi najifaharisha na histori ya wazee wangu hawa kwa kuwa ni historia yangu pia na hii ndiyo sababu nikaandika kitabu kuwaenzi hawa wazee wangu.

Mwalimu Nyerere anaingia katika historia hii kwa kuwa yeye ni sehemu ya historia yetu.

Haiwezekani kumtaja Nyerere bila kumtaja Abdul, Ally na Abbas Sykes.

Haiwezekani kuitaja African Association bila kumataja Kleist Sykes.

Haiwezekani kuitaja TANU bila kumtaja Abdul Sykes na wadogo zake hawa na ukipenda na baba yao.

Hili limejaribiwa na balaa lake ndilo hili linakughadhibisha hii leo unataka makosa yarudiwe tena tuiandike historia ya uhuru bila ya kumtaja Abdul Sykes.

Nyerere kapokelewa na Abdul Sykes nyumbani kwake mwaka wa 1952 alipopelekwa na Joseph Kasella Bantu.

Tuifute historia hii ilhali Nyerere mwenyewe kaeleza hili?

Mazungumzo ya kumwingiza Nyerere kwenye uongozi wa juu wa TAA yalifanyika Nansio nyumbani kwa Hamza Mwapachu na waliokuwapo katika mazungumzo hayo ni Hamza Mwapachu, Abdul Sykes na Ali Mwinyi Tambwe.

Hii ilikuwa 1953.

Juma Mwapachu na kaka yake marehemu Harith Bakari Mwapachu walihamishwa chumba chao kuwapisha wageni kutoka Dar es Salaam.

Juma Mwapachu kaeleza historia hii.
Vipi tuifute historia hii?

Mwaka wa 1953, 17 April, Julius Nyerere na Abdul Sykes wakagombea nafasi ya president wa TAA Arnautoglo Hall na Nyerere akashinda uchaguzi ule.

Haya kaeleza Judith Listowel katika kitabu chake, ''The Making of Tanganyika,'' (1965).

Vipi tukipige marufuku kitabu hiki kisiingizwe Tanganyika?

Mikutano ya siri kuunda TANU ikifanyika nyumbani kwa Abdul Sykes na Nyerere akihudhuria akitokea Pugu.

Mama Daisy, mke wa Abdul Sykes ndiyo alikuwa akiwapa chai na vinywaji vingine nyumbani kwake.

Huyu mimi ni mama yangu.

Nyerere kaacha kazi ya ualimu kaenda kuishi nyumbani kwa Abdul Sykes.

Wenyeji wa Dar es Salaam wengi wamemjua Nyerere kwa kumuona na Abdul Sykes katika mitaa ya Kariakoo na ofisi ya Abdul Sykes Soko la Kariakoo akiwa Market Master.

Sasa tunafanyaje na historia hii.

Kadi No. 1 ya TANU ya Nyerere imeandikwa na Ally Sykes na kadi kanunua yeye kutoka fedha kutoka mfukoni kwake.

Kadi No. 2 Ally Sykes na kadi No. 3 Abdul Sykes, kadi No. 4 Dossa Aziz, Kadi No. 5 Denis Phombeah na Kadi No. 6 Dome Budohi.

Hii ndiyo historia ya wazee wangu sasa naifanyaje wakati naona historia ambayo si sawa inaandikwa na kusomeshwa?

Mimi sikukasirika wala kumtukana mtu.
Nilinyanyua kalamu yangu nikaiandika.

Ikiwa wewe unaona mimi sifa yangu chembelecho ni ''umbeya'' na ''uongo,'' andika historia ya kweli tusome.


Picha ya Dome Budohi kadi yake ya TANU No. 6 niko Nairobi nyumbani kwake Ruiru mwaka wa 1972 nina miaka 20.
 
Gold...
Mimi sipigi kelele nimeandika kitabu cha historia ya uhuru wa Tanganyika.
Kwani hairuhusiwi kuandika ukiwa wewe babu zako walitoka Belgian Congo?
 
Geza...
Rudia kusoma kwa utulivu utaelewa.

Ningeweza kukuambia lakini nataka utumie ubongo wako ili siku nyingine ikiwa hujaelewa kitu unarudia kusoma upya.
nyumbani "kwake"? nani? Sykes? Archives zipo Baba Queen Elizabeth hawezi kuhudhuria State Banquet kwa Sykes wakati Ikulu Magogoni na High Commissioner Residency ipo! najua unataka kumaanisha hivyo ila ukweli upo online!
Pitia Central Office of Information : London - Queen with President Nyerere. [Royal Visit to Tanzania, 1979]
 
Geza...
Hakika Malkia Elizabeth hawezi kualikwa nyumbani kwa mtu binafsi.

Soma tena kwa utulivu utaelewa.
Jitulize soma makala hiyo utaelewa.

Hapa barzani kila msomaji kaelewa hakuna hata mmoja aliyeniuliza hii dhifa ilifanyika wapi?

Hizi makala nazirusha kwenye Whatsapp na huko jamaa wanachangamka sana kwa maswali.

Hakuna aliyeniuliza hili swali lako.

Watu maarufu Ally Sykes aliowaalika nyumbani kwake ni Sidney Poitier, Harry Belafonte na Albert Rothschild.

Si Malkia wa Uingereza.
Nadhani sasa umeelewa.

Ahsante kwa link ila ningependa nikufahamishe kitu.
Nimeishi Wales na Scotland, nikija London mara nyingi na nilikuwa "Royal Watcher."

Huu ulikuwa wakati wa ujana wangu.
Nilijifunza mengi kuhusu House of Windsor.

Mimi si mgeni wala mjinga katika mambo haya.
 
sasa ulishindwa nini kunielewesha? na kama muelewa, kwake is a loose indicator! Kwake who? wakati sentence ya juu inaongelea Sykes? Wewe unafikiri kwanini Nyerere alipuuzia watu wa caliber na ego ya Sykes? Je, angewaendekeza, angeweza kuendesha nchi ipasavyo?
 
..namuona CDF Lt.Gen.Abdallah Twalipo.

..adc wa Mwalimu, Major.Mwamdanga.

..pia yupo IGP Philemon Mgaya.
 
Geza...
Unazungumza umeghadhibika.
Huenda hata unaposoma kalamu yangu unakuwa umeghadhibika.

Ukiwa na hasira akili haifikiri sawasawa.
Sikutaka kukueleza mapema nilitaka nijifurahishe na wewe.

Katika pambano la Mohamed Ali na George Foreman, Kinshasa 1974 handlers wa Foreman waiamini ikifika round ya tatu Ali atakuwa keshapigwa na pambano limekwisha.

Ilipofika round ya tatu wakati wa mapumziko wale handlers wa Foreman wakawa wanampigia kelele Foreman wanamwabia, ''George finish him off!''

Daktari wa Ali, Dr. Pacheco akawa anamwambia Ali, ''Ali unayasikia maneno hayo?''

Baada ya miaka mingi kupita Dr. Pacheco anaeleza anasema, ''Baada ya mimi kumwambia Ali naneno yale, Ali alinishangaza kwa kuniambia, ''Mimi huyu nampiga.''

Dr. Pacheco akamjibu Ali akamwambia, ''Mpige basi twende zetu nyumbani.''
Ali akajibu, ''Let us have some fun first.''

Sikutaka kukujibu kwa haraka nilitaka tuburudike.
Umezungumza kuhusu ''kupuuza.''

Uhakika ni kuwa wote wawili walipuuzana kwa muda mrefu sana.
Lakini mimi sitaki tuiingie huko.

Nilimuhoji sana Bwana Ally kuhusu nini kilitokea baada ya uhuru kupatikana kusababisha yote yaliyotokea.

Haya pia singependa kuyaeleza na naamini wewe huyajui.

Baadhi ya mambo sikuyaandika katika kitabu kwani niliona hayana umuhimu wala hayaongezi elimu katika historia ya uhuru wa Tanganyika.

Lakini baada ya miaka mingi kupita katika makala ambayo Daisy Sykes aliandika kama kumbukumbu ya miaka 50 toka baba yake kufariki, Daisy aliandika maneno haya na nakuwekea hapo chini:

‘’Uhuru ulipokuwa dhahiri sasa unapatikana na hapo ulipopatikana, ulikuja na changamoto nyingi ambazo naamini baba hakuzitegemea.

Haitakuwa sawasawa ikiwa sitaeleza upeo wa juu wa baba yangu katika wema, huruma na unyofu aliokuwanao.

Hata nilipokuwa mtoto nilipata kushuhudia na kuona chokochoko na chuki dhidi yake bila shaka kwa ajili ya hasad kwani baba kwa kiwango chochote kile alikuwa mtu aliyefanikiwa kwenye ngazi nyingi ambazo wengi hawakuthubutu hata kuota kukanyaga, lakini sikumuona baba kukasirika wala kutaka kulipiza kisasi.

Katika unyofu wa hali ya juu aliendelea na maisha yake.’’

Kubwa ambalo naamini hili liliwachoma wengi ni kufutwa kwa historia ya Abdul Sykes katika historia ya uhuru wa Tanganyika.

Naamini bila shaka yoyote kuwa hili Ally Sykes lilimuudhi kupita kiasi.

Umetumia neno ''kuendekeza.''
Hili neno halifai kulitumia katika historia ya watu hawa wawili ni neno la kejeli na kebehi.

Sipendi kumtetea Bwana Ally lakini hili nitalisema kwa kuwa nalijua vizuri.
Ally Sykes alikua mtu ''humble,'' sana.

Uwezo wake katika mali na jinsi alivyokuwa ni vitu tofauti.
Hili nimeshuhudia katika kila hali.

Nimemuona mara chungu nzima Ally Sykes kakaa kibarazani kwa rafiki zake wa utotoni kawafata kuja kuwasalimia na gumzo limenoga.

Ally Sykes anabishana na rafiki zake kidole machoni.
Ikiwa humfahamu huwezi kuamini kama huyu ndiye Ally Sykes umsikiae.

Ukimwalika harusi hata Manzese Ally Sykes atakuja.
Nimeshuhudia harusi nyumbani kwake watu wakubwa wenye majina wamehudhuria.

Alikuwa hawana sehemu yao maalum ya kukaa.

Aliwaweka na ndugu zake wa Gerezani kama marehemu Kazi Kambi muuza mkaa na Kambi kadi ya harusi kapelekewa nyumbani kwake Mtaa wa Congo na Kiungani.



Ally Sykes na Julius Nyerere nyumbani kwa Nyerere Magomeni 1958


Kulia ni Nangwanda Lawi Sijaona, Abdulwahid
Kleist Sykes, Julius Kambarage Nyerere na Waziri
Dossa Aziz ukumbi wa Arnautoglo katika dhifa ya
kumuaga Nyerere safari ya pili UNO 1956.
 
Tatizo unaishi kwenye nadharia ya fantasy world umerithishwa matarajio ya Sykes ambayo hayakutimia na kuishia kuwa manung'uniko na hisia za kudhulumiwa mpaka kihama chake! Tanganyika ilikuwa kubwa na isingeweza kuzunguka kwa vijana wa K'koo peke yao! Ukielewa hilo itakuwa na maono tofauti kichwani na amani moyoni.
 
Geza...
Hapana si kweli wewe hutujui sisi.

Mimi babu yangu Salum Abdallah ni muasisi wa TANU Tabora 1954 na TRAU 1955 na haikuwa tegemeo lake kunufaika katika siasa.

Alikuwa mtu wa kujiweza na alitoa fedha zake katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Abdul Sykes hakuchukua siasa kama ajira halikadhalika Ally Sykes, Dossa Aziz na wengine wengi.

Hawa wameunda TANU kwa fedha zao na wakaijenga TANU kwa mali zao.
Wala mimi siishi katika ''fantasy world,'' kama unavyodhani.

Wala mimi sinung'uniki.

Mimi hapa nasomesha historia ya wazee wangu ili ifahamike na wapate heshima wanayostahili.

Haya uyasomayo hapa wewe hukuwa unayajua.
Huondoki hapa kwa kuwa unajua kuwa hapa ipo elimu ambayo wewe hukuwanayo kabla.

 
sasa mbona kila siku unaongelea maumivu ya Sykes? Mnampambanua kama serikali ya Nyerere ilimdhulumu? Au upeo wa kuelewa hisia zako wengine hatuna? Huyo Sykes ana tofauti gani na Machifu ambao waliathirika na serikali za Uchifu kufutwa na wakaacha yapite? Wahenga husema tenda wema uende zako!
 
Unalazimisha mambo Mzee.

Hao Wazulu unaowapigia debe kila sentensi hawana nafasi kwenye historia ya Tanganyika.

Mbona inakuwa ngumu sana kuelewa?

Mzee MS ni wazi una matatizo makubwa sana ya kisaikolojia ila hutaki kutambua hilo.

Iweje wewe mtu mmoja ujiamini kuwa upo sahihi kila mara ilhali unapingwa hoja kwa hoja, na unakimbia hoja ukizidiwa?
 
Geza...
Sijui kwa nini unasema maumivu.
Unazungumzia dhulma.

Unauliza tofauti kati ya Abdul Sykes na labda Chief Thomas Marealle au Chief Abdallah Said Fundikira.

Nimeandika kitabu cha maisha ya Abdul Sykes kinaitwa, "The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika."

Tatizo kubwa hapa ni ukiwaambia watu wasome hili haliwezekani.
Ingekuwa umesoma kitabu hiki usingeniuliza maswali hayo ya dhulma.

Ungekuwa umesoma kitabu ungejua tofauti iliyopo baina ya Chief Marealle na Chief Fundikira na Abdul Sykes.

Historia ya machief wote zinafahamika na hakuna hata moja iliyofanana na historia ya Abdul Sykes.

Sasa jiulize kweli historia ya Abdul Sykes ni "Untold Story?"
Je, kweli kulikuwa na, "Muslim Struggle?"

Vyuo vyote nilivyozungumza huwa naulizwa maswali haya.
Halafu unaniuliza mimi kuhusu uwezo wako wa kuelewa.

Nakuwekea hapo chini Daisy anavyoeleza uhusiano wa baba yake na machifu wa Tanganyika:

''Kutokana na hadhi hii ya baba yangu na umaarufu wake na kule kupenda kukirimu watu, nikawa si mgeni kwa machifu mashuhuri na nikawa nawahudumia walipokuwa mara nyingi wakija nyumbani.

Wageni hawa mashuhuri waliokuwa wakija nyumbani ni pamoja na Mangi Mkuu Thomas Marealle, Machifu Abdiel Shangali, John Maruma kutoka Moshi, Adam Sapi Mkwawa kutoka Iringa, Kidaha Makwaia kutoka Usukuma, Abdallah Fundikira, Harun Lugusha kutoka Tabora, Humbi Ziota kutoka Nzega, Michael Lukumbuzya kutoka Ukerewe na Patrick Kunambi kutoka Morogoro na wengine wengi.

Hawa machifu kwa kawaida walikuwa wakija na wake zao, wanawake warembo ambao hawakuacha kunifanya mimi kuwashangalia.

Nakumbuka katika machifu wale, alikuwapo chifu mmoja na wa pekee mwanamke - Mwami Theresa Ntare kutoka Kasulu Kibondo.

Katika hali kama hii iliyokuwa tabu kufahamika, tukiwa watoto tulipata kujua maisha ya jamii nyingine, lugha zao, utamaduni wa makabila mengi ya Tanganyika kabla ya watu wengi kutoka sehemu nyingine za pwani hawajajua chochote kuhusu watu hawa.''

Soma kitabu cha Abdul Sykes.

Ni kitabu pekee Tanzania kilichochapwa matoleo manne mfululizo moja baada ya jingine toka kichapwe 1998.


Kushoto waliosimama Abdul Sykes, Tewa Said Tewa
Chief Fundikira waliokaa wa kwanza kulia hijja 1964.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…