Malkia Elizabeth na Viongozi wa TAA, 1953

Sasa kwa upeo wako unadhani nani alipaswa kuwa Rais badala ya Nyerere?
 
Sasa kwa upeo wako unadhani nani alipaswa kuwa Rais badala ya Nyerere?
Geza...
Ndiyo nakunasihi usome kwanza ndiyo uje katika mjadala.

Kitabu cha Abdul Sykes wataalamu wa historia wanaita, ''corrective history,''
yaani kusahihisha historia.

Si suala la nani alistahili kuwa Waziri Mkuu wa Tanganyika.
Historia inayojulikana ya TANU na uhuru wa Tanganyika haiko sawa.

Haiwezekani kuandika historia ya TANU ikawa Abdul Sykes hayumo.
Soma kitabu.
 
Gold...
Mimi niwalazimeshe Oxford University Press, Nairobi kunitia katika mradi wa kuandika historia ya Tanzania kwa ajili ya shule za msingi na wachape kitabu changu, ''The Torch on Kilimanjaro,'' (2006).

Mimi niwalazimeshe Oxford University Press, New York na Harvard kunitia katika jopo la waandishi kutoka kila pembe ya dunia kuandika Dictionary of African Biography, (2011) na kuchapa nilichoandika.

Mimi niwalazimishe waandishi wa ''Nyerere Biography,'' kwanza kunihoji kuhusu Mwalimu Nyerere na baadae waandike katika kitabu cha Mwalimu kuwa Maktaba yangu ni kati ya maktaba tatu bora - maktaba ya Salim Ahmed Salim, Brig. Hashim Mbita na Mohamed Said.

Mimi nilazimishe kualikwa Northwestern University, Evanston Chicago kuzungumza (2011) na kwengine kwingi.

Wote hawa nawalazimisha.

Mohamed Said anakimbia hoja barzani.




 
Babauuuuuu sikamooo!
 
Hiyo picha hapo juu si kabla ya Uhuru Mwl anajulikana lini alianza kuvaa makoti yasiyo na collar!
 
unakuta unaangaika kumwelewesha mtu anakaa ukweni.
 
Babauuuuuu sikamooo!
Smaki,
Ilitosha mimi kukukalia kimya nisikujibu.

Sababu ni kuwa umenionyesha huthamini adabu salama yangu usiendelee kunivunjia heshima yangu ni kukuepuka.

Nimesikitika sana kuwa nimekuandikia kwa heshima nikitegemea utarejea hapa kwa wema badala yake umerudi hapa kunizomea.

Nia ya kukuandikia ni kukushukuru kuwa umenisaidia kukuingiza katika utafiti tunaofanya sasa kipindi kirefu jinsi historia hii ya uhuru wa Tanganyika ilivyopokelewa.

Kwa mukhtasari ni kuwa ikiaminika kuwa TANU iliundwa na Julius Nyerere na mimi nikaja na kitabu kinachokwenda kinyume na historia hiyo.

Utafiti unaonyesha kuwa mwanzo historia hii niliyoandika ilikutana na vitisho kwa mwandishi kisha kukawa na kukataa kuwa ni kweli kisha pakawa na mchanganyiko wa hasira, hamaki na kuzomewa mwandishi kama ulivyofanya wewe.

Utafiti bado unaendelea ukikamilika utachapwa.
Wewe umeingia kwenye "data base," ya utafiti huu.

Nakushukuru sana kwa msaada wako huu.
 
Sababu ni kuwa umenionyesha huthamini adabu salama yangu usiendelee kunivunjia heshima yangu ni kukuepuka.

Nimesikitika sana kuwa nimekuandikia kwa heshima nikitegemea utarejea hapa kwa wema badala yake umerudi hapa kunizomea.
Wewe Mzee!! sijui una tatizo gani huko up stairs! nakupa heshima yako unasema nakuzomea mbona una hasira sana?? banae shikamoo tena bana!
 
Wewe Mzee!! sijui una tatizo gani huko up stairs! nakupa heshima yako unasema nakuzomea mbona una hasira sana?? banae shikamoo tena bana!
Smaki,
Yawezekana kwenu vile ulivyoandika ikawa ni sawa.

Yawezekana kwenu hivi ulivyonita, "We Mzee....na ukaandika ulivyoandika ni sawa pia.

Mimi kwetu nilivyofunzwa na mama yangu ni tofauti.

Jingine mimi si mtu wa lugha hizo za "bana."

Mimi nakuandikia kwa adabu na heshima ya kuandika.

Siandiki kihuni.
 
Mkuu, maktaba bora walizotaja zilikuwa nne. Hizo ulizotaja na nyingine ya Joseph Gagnija.
 
Mzee ukiwa humu ukubaliane na matokeo hii ni jamii......hata mie nina kwetu!....ukitaka jukwa la wazee lipo!
 
Mzee ukiwa humu ukubaliane na matokeo hii ni jamii......hata mie nina kwetu!....ukitaka jukwa la wazee lipo!
Smaki,
Si suala la uzee wangu.
Hili ni suala la kuheshimiana.

Ikiwa unapendezewa na ufedhuli sina la kufanya ila mimi kukunyamazia kuepusha shari.

Sitokujibu.
 
Uko compulsively obsessed na Mwalimu... You love him to death
 
Uko compulsively obsessed na Mwalimu... You love him to death
Veza...
Umesema kweli mapenzi yangu ni kwa Abdul Sykes na Julius Nyerere katika kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.

Jopo la Prof. Issa Shivji walipokuja kunihoji wakati wanatafiti historia ya Mwalimu Nyerere walipigwa na butwaa na taarifa nilizokuwanazo kuhusu Mwalimu toka siku ya kwanza alipopelekwa nyumbani kwa Abdul Sykes.

Wameitaja Maktaba yangu ndani ya kitabu cha Julius Nyerere kama ni kati ya maktaba tatu bora.

 
Nashindwa kuamini kuwa muonekano huo wa Nyerere alikuwa na miaka 30.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…