Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,692
- 23,038
Buckingham Palace ni makazi na ofisi wakiwa London na hutumika kwa shughuli za kitaifa.🥰🥰🥰🥰🥰🥰🥰🥰🥰🥰 thanks
Naicheck Bukhingham Palace watu wanaishi aisee
Makazi yake na mali za Elizabeth akiwa Malkia wa Uingereza rasmi ni Balmoral Scotland na Sandringham ambayo ipo Norfolk.
Hapa Norfolk ndipo babu George wa tano na baba yake Elizabeth, Mfalme George wa sita walikuwa wakiishi na walifariki wakiwa humo.
Balmoral ni makazi yake ya pili Malkia Elizabeth na familia yake na ndipo alipenda kwenda huko wakati wa kiangazi akila nyama choma na ndipo alipofia juzi. Makazi haya yalikaliwa na Malkia Victoria bibi yake Elizabeth.
Hivyo, utaona kwamba hapa Elizabeth aliua ndege wawili kwa jiwe moja na kutwaa mali ya upande wa baba na upande wa mama.
Hizi ni mali binafsi za familia.
Ndo maana huyu bibi alikuwa ni mmoja wa matajiri wakubwa sana duniani.
Yaani kale kaprince Louis (mtoto wa mwisho wa William) akiwa mtu mzima fweza ipo kwa benki tayari yamsubiri yeye na watoto wake.