Ashampoo burning
JF-Expert Member
- May 12, 2023
- 593
- 2,219
rip mwamba alikuwa jirani yangu pale ghorofa za utumish house magomeni alikuwa kuna wakongo walikuwa wanaishi pale miaka yote nilikuwa sijui kwamba ni muimbaji huyu jamaaaView attachment 2956136Mwimbaji nyota wa FM Academia, Malu Stonch amefariki dunia baada ya kuanguka ghafla jukwaani.
Hali hiyo imetokea katika ukumbi wa Target Mbezi, Beach, Jumamosi usiku wakati mwimbaji huyo akiwa jukwaani anaimba wimbo wa "Hadija".
Inaelezwa kuwa wakati anaimba wimbo huyo, Malu Stonch alidondoka ghafla na kupoteza fahamu.
Baada ya kupatiwa huduma ya kwanza huku akiwa bado hajitambui, ndipo akakimbizwa Masana Hospital.
Mwanahabari na mdau mkubwa wa muziki, MC Petit aliyekuwa miongoni mwa waliomkimbiza Malu Stonch hospital, ameithibitishia Saluti5 kuwa mwimbaji huyo amefariki.
"Pale Masana walipompokea tu, wakatumbia tumpeleke Lugalo Hospital kwa kuwa mgonjwa wetu ameshafariki," ameeleza MC Petit.
"Tulipofika Lugalo nao wakatuthibitishia kuwa Malu Stonch amefariki na hivyo tukafanya utaratibu wa kumpeleka chumba cha kuhifadhi maiti," alifafanua zaidi MC Petit.
Pumzika kwa amani Malu Stonch.
Said Mdoe
7/4/2024
Mara mwisho nimekuja kukutana nae goba kuna casino ndogo tukapiga story mbili tatu hapo goba casino ndogo texas walikuwa na project pale miezi kama mitano hivi imepita
Leo kafariki RIP.......