TANZIA Malu Stonch (Nuhu) afariki Dunia. Alikuwa akitumbuiza jukwaani

TANZIA Malu Stonch (Nuhu) afariki Dunia. Alikuwa akitumbuiza jukwaani

Pumzika Kwa amani malu stonch nuhu...sauti yako ilikuwa amazing mwamba
 
Duh. Inasikitisha.
Ametoka nyumbani na wala hakuaga.

Treasure every moment, hujui ya baadae.

R.I.P Utakwepo masikioni mwetu daima.

Wewe Hadija nae!
 
View attachment 2956136Mwimbaji nyota wa FM Academia, Malu Stonch amefariki dunia baada ya kuanguka ghafla jukwaani.

Hali hiyo imetokea katika ukumbi wa Target Mbezi, Beach, Jumamosi usiku wakati mwimbaji huyo akiwa jukwaani anaimba wimbo wa "Hadija".

Inaelezwa kuwa wakati anaimba wimbo huyo, Malu Stonch alidondoka ghafla na kupoteza fahamu.

Baada ya kupatiwa huduma ya kwanza huku akiwa bado hajitambui, ndipo akakimbizwa Masana Hospital.

Mwanahabari na mdau mkubwa wa muziki, MC Petit aliyekuwa miongoni mwa waliomkimbiza Malu Stonch hospital, ameithibitishia Saluti5 kuwa mwimbaji huyo amefariki.

"Pale Masana walipompokea tu, wakatumbia tumpeleke Lugalo Hospital kwa kuwa mgonjwa wetu ameshafariki," ameeleza MC Petit.

"Tulipofika Lugalo nao wakatuthibitishia kuwa Malu Stonch amefariki na hivyo tukafanya utaratibu wa kumpeleka chumba cha kuhifadhi maiti," alifafanua zaidi MC Petit.

Pumzika kwa amani Malu Stonch.

Said Mdoe
7/4/2024
Nilidhani ni huu utabiri kumbe ni FM Academia

 
Back
Top Bottom