Malumbano ya Spika Sitta na Mzee Mrema

Malumbano ya Spika Sitta na Mzee Mrema

He had option ya kuresign and make it very clear he is against what the so called baraza la wabunge CCM trying to robe from Tanzanians.. yeye kukubali kusoma/kutangaza mjadala umefungwa na wakati anasema ni mpiganaji ni kutuzungua tuuu... the true mpiganaji anaweka maslai yake second after public interests/welfare ila kwake aliona ni mara kumi kulinda uspika wake, mshahara na posho yake
Kwa mazingira ya Tanzania, hiyo ilikuwa option mbovu kabisa kwake kisiasa na isingebadilisha lolote katika kile anachokipigania, ingekuwa ni sawa na kuwapa ushindi wa chee kina Lowasa.

Baada ya funzo la Mrema kujitoa na kuishia kumalizwa kisiasa,mtu mwenye akili hawezi kufanya tena jambo hilo katika wakati anaojua hawezi kuibwaga CCM katika kiti cha Uraisi,ata angejitoa na kugombea uraisi hasingeshinda kutokana na umaarufu wa J.K kwa wadanganyika,hivyo angeingia kwenye njia aliyoipitia Mrema kuelekea kifo cha kisiasa, atleast kwa sasa option waliyoitumia ni sahihi, mapambano yafanyike within CCM kuelekea 2015.
 
MWENYEKITI wa TLP, Augustine Mrema, ambaye katika siku za karibuni amekuwa akizungumzia sana masuala ya baadhi ya viongozi wa CCM, jana alitamba kuwa ana utajiri wa Sh37 milioni kwenye akaunti yake na hivyo ni tajiri kuliko Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

Alikuwa akijibu kauli iliyotolewa na Spika Samuel Sitta ambaye alimuelezea waziri huyo wa zamani wa mambo ya ndani kuwa amefilisika kisiasa na kifedha na ndio maana anahaha kujikwamua kwa kuipigia debe CCM.

Sitta, ambaye ameongoza kipindi cha mwisho cha uspika wake kwa mapambano dhidi ya watu aliowaita maadui wake wa kisiasa, alidiriki kumuelezea Mrema kuwa amefilisika na kwamba huenda anapata fedha kutoka chama hicho tawala.

Sitta alitoa tuhuma hizo nzito baada ya Mrema kuitisha mkutano na waandishi wa habari na kumtuhumu spika kuwa ana makundi ndani ya Bunge na kwamba anaendelea kuzungumzia sakata la utoaji zabuni ya kufua umeme wa dharura kwa Richmond Development LLC kwa kuwa mjadala huo ulishafungwa na Bunge.

Jana Mrema alikanusha tuhuma zote hizo na kudai kuwa yeye hajafulia wala hajafilisika kisiasa na kifedha na kwamba hajachanganyikiwa wala kuhongwa na CCM ili akipigie debe na akamtaka Spika Sitta atoe ushahidi wa tuhuma zake.

Pia Mrema alitangaza kuwa atamfikisha mahakamani Sitta kwa madai kuwa amemkashfu na kumvunjia heshima mbele ya jamii na pia atamshtaki kwa Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa kwa kuwa amevunja kanuni za vyama vya siasa kwa kutoa maelezo ya uongo dhidi yake.

"Mimi nilimuonya mheshimiwa spika kwamba aache kuwa na makundi ndani ya Bunge na asiendelee kulalamikia suala la Richmond kwa sababu mjadala huo ulishafungwa na Bunge. Na kama haridhiki yeye pamoja na wenzake wajiondoe CCM kama nilivyofanya mimi mwaka 2005,"alisema Mrema katika mkutano wake na waandishi jana.

"Lakini badala ya kujibu hoja, Mheshimiwa Sitta akaamua kunikashfu na kunitukana mimi kama mtu binafsi, jambo ambalo ni kinyume cha kanuni za vyama vya siasa zilizopitishwa na Msajili wa Vyama vya Siasa mwaka 2007, Ibara ya 5(d) inayotaka kutotoa maneno yoyote au maandishi ambayo ni ya uongo kuhusu mtu yeyote au chama chochote cha siasa."

Akifafanua kuhusu tuhuma hizo, Mrema alisema kifedha hajafilisika bali yeye ni tajiri kuliko hata Pinda kwa kuwa anamiliki Sh.37.75 milioni kwenye akaunti yake.

Mimi sijafulia. Kufulia kwa lugha ya mitaani ni kufilisika hata kukosa fedha ya Chakula. Namhakikishia mheshimiwa spika kwa kuwa sijafulia kama anavyodai kwani nina uwezo wa kujilisha na familia yangu pamoja na kusomesha watoto wangu na kujitibu ninapoumwa bila ya msaada wa mtu yeyote," alisema Mrema.

"Nimefanya kazi serikalini kwa zaidi ya miaka 30 nikiwa ofisa wa Usalama wa Taifa, mbunge, waziri na baadaye naibu waziri mkuu.

Wakati wote huo nilikuwa najiwekea akiba kutokana na mshahara na marupurupu niliyokuwa nikilipwa. Kufikia jana Machi 5 ninayo akiba ya Sh.37.751,451.79 kwenye akaunti namba 2017800187 ya benki ya NMB, tawi la Bank House.

"Kwa hiyo mimi ni tajiri tena kuliko waziri mkuu ambaye alitangaza mali zake na kusema ana Sh25 milioni kwenye akaunti yake, sasa iweje Sitta aseme eti Mrema amefulia... maana yake ni nini?"

Mrema alikuwa akisema hayo huku akionyesha taarifa yake ya benki inayoeleza kiasi kilichomo na masuala mengine.

Kuhusu kufilisika kisiasa Mrema alisema chama anachokiongoza ni cha nne nchini kati ya vyama 18, na kwamba hata katika uchaguzi wa serikali za mitaa, TLP ilifanya vizuri na ina viongozi katika ngazi zote tangu mitaa, vijiji na vitongoji.

Mrema, ambaye ameshagombea urais kwa tiketi ya NCCR Mageuzi na baadaye TLP kabla ya kutangaza kurudi kugombea ubunge kwenye jimbo lake la zamani la Vunjo, alisema kuwa chama chake kilishinda kwenye vijiji 20 na vitongoji 48 kwenye jimbo la Vunjo katika uchaguzi wa serikali za mitaa.

Kuhusu madai kuwa amechanganyikiwa na kuhongwa na CCM ili akipigie debe chama hicho tawala, Mrema alimtaka Spika Sitta atoe ushahidi wa tuhuma hizo kwa kuwa zimemdhalilisha, zimemvunjia heshima na kumpaka matope mbele ya jamii. Alisema atamshtaki mahakamani kwa kumkashifu na kumsingizia mambo ya uwongo.

"Kuchanganyikiwa maana yake ni kutokuwa na akili timamu. Sasa mimi kama ningekuwa sina akili timamu wanachama wa TLP wangenichagua niwe mwenyekiti wao? Namuomba Spika aonyeshe ushahidi wa cheti cha hospitalini kuonyesha kuwa mimi nimechanganyikiwa,"alisema Mrema.

Mrema pia alisema:"Mimi sijahongwa na CCM wala na mtu yeyote. Hizi ni tuhuma mbaya kwangu binafsi, kwa chama changu na kwa CCM. Namtaka atoe ushahidi aonyeshe ‘pay roll’ mahali ninakosaini huko CCM."

Mrema alisisitiza kuwa CCM ina uwezo wa kushinda uchaguzi bila hata ya kupigiwa debe na yeye wala TLP kudai kuwa imeweza kushinda katika uchaguzi mwaka 1995, 2000 na 2005 bila yeye kuipigia debe.

Alisema Spika Sitta anashindwa kumuelewa kwa kuwa yeye huzungumzia mambo ya kitaifa ambayo yako juu ya vyama vya siasa kama vile mshikamano, amani na utulivu, ambayo hayana chama kwa kuwa amani ikivunjika watu wote wanaathirika bila kujali nani yuko chama gani.

"Vile vile masuala ya Bunge hayahusu chama chochote cha siasa kwani bunge ni la wananchi wote, hivyo ninapomkosoa spika wa Bunge, siingilii mambo ya CCM kama ambavyo anadai," alisema Mrema.

Mrema alisisitiza kuwa yeye hajafilisika kisiasa bali Spika Sitta ndiye amefilisika kisiasa kwa kuwa anafanya siasa makanisani.

"Kwa muda mrefu spika amekuwa akifanya siasa makanisani kama alivyofanya hivi majuzi huko mkoani Ruvuma ambako alitangaza kuwa CCM walitaka kumfukuza uanachama kutokana na msimamo wake katika suala la Richmond. Spika aelewe kuwa nchi hii siyo ya Wakristo peke yao, hivyo kufanya siasa makanisani kunahatarisha mshikamano wa nchi yetu," alisema Mrema.
 
hawa ndiyo viongozi wetu - tutegemee nini?
 
he he heee,mtu wa pili kuplekwa mirembe huyooo,pinda mpe maneno yake,sasa ndio huyu angekuwa rais wetu huyu???

jamaa kaishiwa hana jipya

Pamoja na wehu wake, lakini hapa amenifanya nicheke sana. Hilarious!

Huyu ni kichaa mwacheni.

Kweli huyu anafaa kupelekwa Milembe ikishindikana zaidi basi ahamishiwe Mathale

Sio kichaa, anawachizisha nyie

Kweli kila shetani na mbuyu wake

ngoja nitafute kwenye magazeti

Mrema.??????????!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! ama kweli kaishiwa mashairi.!!!!!!!!!

Sioni tatizo hapo kwa Mrema kutaja falanga anazo miliki mbona Pinda kataja hamjasema apelekwe Milembe? au kwa vile mmechoka mzee wa Kilalacha?
 
Teh teh teh,yaani Mrema ni kiboko kwa kugonganisha watu.So anataka ionekane kwamba Sitta nae kamtukana Pinda indirect? yaani opportunity yoyote ya kujenga hoja kisiasa hawezi iacha.Lakini si kuna kipindi alitangaza kuwa ana milioni 300?sasa zimeshuka ghafla au yalikua mazungumzo ya kisiasa?lol

juzi kati alienda india kutibiwa, na zingine ndo zinamweka barabarani!!

anahela kuliko pinda hahahahaha
 
Labda nisaidiwe kidogo na wale weledi wa elimu ya afya ya binadamu. Jee maradhi yanayomkabili Mheshimiwa sana Lyatonga, yaani kisukari (kama sikosei) yana effect yeyote na ubongo? Maana nashindwa kuelewa, mtu wa hadhi yake na nafasi yake Kitaifa pamoja na rekodi yake ya nyuma ,kuingia malumbano yasiyo na tija kwa wafuasi wake na taifa kwa ujumla kwa kiwango cha chini namna hiyo, kwa kweli sipati picha.
Tuelezeni, kama ni ugonjwa huo ili tumsamehe. Ila kama si hivyo tumhukumu.
 
Jamaa anapigania maisha yake katika kipindi cha mwisho wa uhai wake kwa kuwafanya watanzania wamdharau na kutomuheshimu kama zamani
 
Kwa hiyo Mrema anatuthibitishai kwamba yeye kaiba zaidi ya Pinda
 
Jamaa anapigania maisha yake katika kipindi cha mwisho wa uhai wake kwa kuwafanya watanzania wamdharau na kutomuheshimu kama zamani

Hapana!!! Hili jitu ni haribifu tu. Anatia aibu kwa wanasiasa wa kweli. Sina nia ya kudharau walimu wa shule za msingi ambao wamepaa hadi kuwa wanazuoni. Yeye hata angedanganya vipi eti anaongeza elimu ya juu, uwezo huo hana, na kama lilivyo tabaka la wapumbavu, haelimiki kamwe .... huu upumbavu wake asingeendelea kutuonyesha.
 
Angalau Mrema anaiona tabia ya ukigeugeu isiyotabirika ya Speaker wetu Sitta. Spika wetu hana analolianza akalimaliza.
 
Luteni,

Nafikiri Mrema had a right to do this... he is in politics and he was mtumishi wa UMMA for almost his adult life (working life).. sasa kwanini asitangaze? Alafu kumbuka watu hata umu JF anamesema amefulia mara ohh awezi kujitibu, hawezi kulisha familia yake etc... and that was based on what??? i am not sure!!!

Sasa amewaambia how much he has in saving account and its above Pinda.. sasa bado amefulia? na kama that the case Je Pinda amefulia pia..

.....and you believe him whole heartedly??😀
 
the question to ponder is if ccm is doing fine then is there any need for him to be on opposition side?
 
kwa mujibu wa spika kumbe CCM huwapa fedha viongozi wa upinzani ili waipigie debe CCM??
 
Mheshimiwa Mrema najua unasoma Jamii forum na pia ni member...hebu tueleze zaidi na nyumba unazo ngapi??usiishie kutaja fedha tu
 
just one question for you.. why most opposition political leaders sasa hivi hawagombei urais bali ubunge?[/QUOTE said:
Shehe yahaya ameshatabiri kwamba mtu yeyote akitaka kugombea urais kumpinga JK atakufa.na kupotea ..kwa hiyo wengi wameogopa...
 
Nadhani hapa mnaongelea ushabiki, Sitta kasema Mrema kafulia naye kasema ana mil.37 benki na PM ana mil.25. je kama ni kufulia si PM angekuwa wa kwanza kufulia? Halafu kingine defintion ya kufulia ni ipi? Inatkiwa mtu awe na kiasi gani cha fedha? Tulimsifu sana PM alivyotangaza fedha na mali zake. Nadhani hapa kuna point Mrema ameileta na wachambuzi wa mambo wanaweza wakachambua vizuri tuone pumba na mchele bila kuweka ushabiki wa kisiasa wala wa mtu mmoja mmoja.
 
Back
Top Bottom