Maluweluwe ya vidonge vya ARV yanatokana na nini?

Maluweluwe ya vidonge vya ARV yanatokana na nini?

Jamani jamani jamani! Ukimwi unatisha! Ukimwi ni kuchungulia kaburi hata kama utajiliwaza vipi?

Mimi nilikuwa mtu wa bata saana! (Hata sasa hivi japo nimekua).

Siku hiyo nikawa pale Sinza mori (Lachaaz pub) kabla aijaungua! Nilikuwa mtu fulani hivi kwa mwonekano kila pisi kali ilikuwa inanishobokea! Basi!

Kwa mbali nikaona binti fulani kanikazia macho! Nikampotezea! Baada ya dakika 10, 20, 30, kila nikimtizama namkuta macho kodo akiniangalia! Nikasema isiwe shida nikampa ishara ya kumuita akaja mazima!

Mimi muda wote nilikuwa nimesimama kaunta napiga vyombo! Alivyofika akaomba tukae pembeni na baada ya story akaonyesha kunipenda (mh? Kumbe na wanawake wanapenda ila hawana ujasiri wa kutongoza).

Nikaondoka na kwa usafiri wa bajaji mpaka gesti moja iliyoko barabara ya njia panda Sinza Mugabe kama unaelekea standi ya Simu2000 nikaspend night naye!

Hila aliniomba nimwamshe mapema saa 11 alfajiri! Lakini kutokana na show ya kibabe tulikuja kushtuka asubuhi kama saa 1 hivi akaanza kupaniki na kukimbia na kuniacha guest!

Sikumbuki kama alidai malipo! Kwavile nilitembea naye peku (kwasababu nilijidanganya kwakuwa kisichana kidogo) nikaanza kuwa na ofu ya je?

kama kaathirika si nitakuwa nimeukwaa? nikizingatia nilihisi michubuko ('k' ya vibinti zinabana sana).

Nikakumbuka somo la kuwahi ARV ndani ya saa 72 nikaenda chap pale hospitali ya Palestina Sinza na kupewa dozi ya ARV nikaianza! Hila walinitaadharisha kuwa nitakuwa naota ndoto za kutisha na maluweluwe na kwamba ni kawaida ya ARV!

Saasaaa! Ebwaana weee! Kwa kipindi cha siku 30!!! Nilikuwa naota mandato ya ajabu yanatisha!! Mashetani si mashetani ni kama niko ulimwengu mwingine wa giza! Sasa cha kujiuliza.

Hivi vidonge vya ARV vilitengenezwa na nini kupelekea hali hii? Au vinatengenezwa kwa kutumia antibodies za watu waliokufa au nini?

Mwenye uzoefu wa kwanini mauzauza ya dozi ARV atujuze tafadhari!

Angalizo!

Huyo mdada tangu siku hiyo sikuwahi kumuona japo nilimuelewa saana! Na haina maana alikuwa mwathirika kwasababu mimi sikupima ila nilichukua tahadhari isije ikawa! Maeneo husika ni ya kweli ili kama huyu binti yuko humu aje pm tukacheke!
Anaitwa Nashaira
 
Kwani mkuu shetani ulishamuona popote hadi useme umeota ndoto za kishetani shetani, unajuaje kwamba uliemuona ndotoni ni shetani?
 
Kwani mkuu shetani ulishamuona popote hadi useme umeota ndoto za kishetani shetani, unajuaje kwamba uliemuona ndotoni ni shetani?
Mkuu! Mungu pekee ndo hakuna mtu aliyewahi kumuona! Na wengine wanamuona shetani wanadhani ni Mungu! Mungu hawezi kujigeuza kuwa shetani! Ila shetani hujigeuza oanekane mungu! Shatani hakuna asiyemjua! Hata mtoto mdogo kichanga anamjua shetani akimuona usiku uanza kulia! Unataka kuniambia wewe humjui shetani? BUSH BIN LADEN
 
Antiretroviral yenye hizo hallucinations (auditory and visual) yaani za kuona na kusikia hutokana na dawa ya Efavirenz.

Sasa mleta mada sijui umepewa combo gani , ukisoma package ya dawa ukikuta kuna hiyo Efavirenz ndio inakuletea shida ndio maana dawa za namna hiyo zinamezwa wakati wa kulala/ karibu na wakati wa kulala.
 
.
 

Attachments

  • cup-of-tea-teapot.gif
    cup-of-tea-teapot.gif
    157.7 KB · Views: 7
Antiretroviral yenye hizo hallucinations (auditory and visual) yaani za kuona na kusikia hutokana na dawa ya Efavirenz.

Sasa mleta mada sijui umepewa combo gani , ukisoma packaging ya dawa ukikuta kuna hiyo Efavirenz ndio inakuletea shida ndio maana dawa za namna hiyo zinamezwa wakati wa kulala/ karibu na wakati wa kulala.
Asante saana! Hila kwakweli kuanzia hapo nilikoma ubishi! Siwezi tembea na mwanamke peku! Never!
Aliyewahi kumeza hivi vidonge akapima akakutwa yuko fresh hawezi fanya tena ngono zembe!
 
Nitarudi kusoma comments za madaktari, phamasia na wenzako ambao wameshatumiaga.
Mimi siyo daktari, ila hizo ni side effects za contents za dawa. Hasa Efavirenz na rilpivirine.

Kwa bahati nzuri zinazotumika sana Tz ni mchanhanyiko wa dawa tatu , Tenofovir, Lamivudine na Delutegravir,

Na hata hivyo, hizo nightmares huwa ni kwa miezi ya mwanzo tu ya matumizi.
 
Back
Top Bottom