Mama amshauri mwanaye kuacha kazi kisa ndoa

Mama amshauri mwanaye kuacha kazi kisa ndoa

tpaul

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
24,225
Reaction score
22,632
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mama mzazi amemshauri binti yake kuacha kazi ili kumfuata nume wake ambaye amehamishwa kikazi kwenda mkoa mwingine.

Kituko hiki kilitokea mnamo mwaka jana baada ya mume huyo kuhamishwa kutoka mkoa wa nyanda za juu kusini keenda mkoa wa kanda ya ziwa. Mume alipopata uhamisho, mke wake mwenye mtoto mmoja, ,aliyeolewa yapata miaka 3 iliyopita, alijaribu kuomba uhamisho ili kumfuata mumewe lakini waajiri wake walionekana kuchelewesha uhamisho wake wakati yeye aliomba kumfuata mumewe haraka iwezekanavyo.

Alipoona uhamisho unachelewa alimuendea mama yake mzazi kumuomba ushauri nini afanye. Bila kumumunya maneno, mama yake alimshauri kuacha kazi mara moja. 'Mume wako yupo kanda ya ziwa, wewe upo kanda ya nyanda za juu, hapo hakuna ndoa. Kama uhamisho wako unachelewa, acha kazi mara moja umfuate mumewe; shauri yako!' Alisikika mama akimshauri mwanaye.

Bila kusita, binti aliandika barua ya kuacha kazi yake ya uhasibu (senior accountant (CPA) na kumfuata mume. Sasa hivi ninapoandika uzi huu, huyo mwanamke ni mama wa nyumbani na hana namna ya kuajiriwa tena kwani umri wake umesogea.

MAONI YANGU
Hivi akina mama kuna wakati wanafikiri kwa kutumia kiungo cha chini tu au ni namna gani wenzangu? Inakuwaje mama amshairi senior accountant kuacha kazi na yeye kweli anamsikiliza mama na kuacha kazi? Akina mama wamerogwa na nani hasa?

Huu ushauri ungetolewa kwa mwanaume nina hakika angeupuuzilia mbali. Kwa kuwa akina mama alkili zao zinaishia kwenye urefu wa pua zao, ndio maana wanaweza kushawishika kuacha kazi kwa sababu tu ya kufuata m.b00 ambayo hata ichepuke kiasi gani haiishi.

Je, ingekuwa wewe mwanaJF ndiye umepewa ushauri wa aina hii, ungemsikiliza mama yako au ungetupilia mbali ushauri wake?
 
Mimi kwa maoni yangu naona kuacha kazi na kufuata mume ni upumbavu uliovuka mipaka. Kama wewe unaona ni sawa, hayo ni maoni yako mkuu.
Inawezekana hajafata hicho ulichokisema, labda ana condition inayomuhitaji kukaa karibu na mumewe, mathalani mgonjwa wa kifafa (epilepsy), atawezaje kukaa mbali na familia yake..?
Na mifano ipo mingi ya condition zinazomfanya mtu atake kuwa karibu na mwenza wake.
 
Inaonekana hujui maana ya Ndoa bado.
Hebu nielimisha kuhusu ndoa mkuu. Kwa hiyo wanandoa wote hapa ullimwenguni wapo panoja wanaatamiana kama kuku anavyoatamia mayai? Hapa nchini hakuna wanandoa wanaoishi na kufanya kazi mikoa tofauti? Na hapa ulimwenguni hakuna wanandoa wanaishi na kufanya kazi nchi na mabara tofauti?
 
Inawezekana hajafata hicho ulichokisema, labda ana condition inayomuhitaji kukaa karibu na mumewe, mathalani mgonjwa wa kifafa (epilepsy), atawezaje kukaa mbali na familia yake..?
Na mifano ipo mingi ya condition zinazomfanya mtu atake kuwa karibu na mwenza wake.
Huyu ni mzima na buheri wa afya. Hana health conditon yoyote inayomfanya kuwa karibu na mumewe zaidi ya hamu uchwara
 
Kama familia yote inajiweza kwanini asiache kazi na kumfuata mumewe?.

Umasikini ndio chanzo wanawake kuwa watafutaji.
Yeye ndiye alikuwa na mshahara mkubwa kuliko mume wake. Baada ya kuacha kazi uchumi wa familia na mipango ya maendeleo vimeyumba vibaya sana. Usitetee kitendo cha ovyo kama hiki mkuu.
 
Yeye ndiye alikuwa na mshahara mkubwa kuliko mume wake. Baada ya kuacha kazi uchumi wa familia na mipango ya maendeleo vimeyumba vibaya sana. Usitetee kitendo cha ovyo kama hiki mkuu.
Wewe umejuaje yote haya ndugu yangu? Ila Mkuu kuna watu ajira na fedha sio vipaumbele vyao wala tusiwashangae na kuwalaumu.
 
Kwahiyo wewe unaamini maisha ni kuajiriwa tu ?

Huyo mama yupo logically kukuzidi wewe katazama mbali na kaangalia the future of her daughter in long run benefits


Mimi Dada yangu aliacha Kazi na kutoka ulaya kumfata mwanaume Tz na Leo she is well of

So kuna wanaume ni potential Sana usiwe na fikra za kimasikini kuwa Kazi ni kuajiriwa serikalini tu.
 
Yuko sawa we baba ukiwa muajiriwa na mke wako muajiriwa mnakua kama familia nzima iko utumwani hapo mmoja ametoka kwenye utumwa wanaweza kuanzisha biashara yao na mke akasimamia fresh.
Mkuu usitetee jambo la ovyo kama hili. Hebu muonee huruma mwenzako. Sasa hivi anajuta kusikiliza maoni ya mama yake. Anatamani walau apate mtu amuajiri kama dada wa kazi, lakini wapi!
 
Back
Top Bottom