Mama amshauri mwanaye kuacha kazi kisa ndoa

Mama amshauri mwanaye kuacha kazi kisa ndoa

Kwahiyo wewe unaamini maisha ni kuajiriwa tu ?

Huyo mama yupo logically kukuzidi wewe katazama mbali na kaangalia the future of her daughter in long run benefits


Mimi Dada yangu aliacha Kazi na kutoka ulaya kumfata mwanaume Tz na Leo she is well of

So kuna wanaume ni potential Sana usiwe na fikra za kimasikini kuwa Kazi ni kuajiriwa serikalini tu.
Hayo ni maoni yako mkuu. Mfano uliotoa hausadifu hiki ninachokisema hapa. Kuacha kazi kisa mume ni uwendawazimu. Cha ajabu huyo mume unayekaa naye bega kwa bega akiamua kuchepuka, lazima atachepuka tu. Kukaa pamoja sio ulinzi sahihi kwa mume kwani mume hulindwa na Mungu, sio mke.
 
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mama mzzazi amemshauri binti yake kuacha kazi ili kumfuata nume wake ambaye amehamishwa kikazi kwenda mkoa mwingine.

Kituko hiki kilitokea mnamo mwaka jana baada ya mume huyo kuhamishwa kutoka mkoa wa nyanda za juu kusini na kupelekwa mkoa wa kanda ya ziwa. Mume alipopata uhamisho, mke wake mwenye mtoto mmoja, ,aliyeolewa yapata miaka 3 iliyopita, alijaribu kuomba uhamisho ili kumfuata mumewe lakini waajiri wake walionekana kuchelewesha uhamisho wake wakati yeye aliomba kumfuata mumewe haraka iwezekanavyo.

Alipoona uhamisho unachelewa alimuendea mama yake mzazi kumuomba ushauri nini afanye. Bila kumumunya maneno, mama yake alimshauri kuacha kazi mara moja. 'Mume wako yupo kanda ya ziwa, wewe upo kanda ya nyanda za juu, hapo hakuna ndoa. Kama uhamisho wako unachelewa, acha kazi mara moja umfuate mumewe; shauri yako!' Alisikika mama akimshauri mwanaye.

Bila kusita, binti aliandika barua ya kuacha kazi yake ya uhasibu (senior accountant CPA) na kumfuata mume. Sasa hivi ninapoandika uzi huu, huyo mwanamke ni mama wa nyumbani na hana namna ya kuajiriwa tena kwani umri wake umesogea.

MAONI YANGU
Hivi akina mama kuna wakati wanafikiri kwa kutumia kwa kiungo cha chini tu au ni namna gani wenzangu? Inakuwaje mama amshairi senior accountant kuacha kazi na yeye kweli anamsikiliza mama na kuacha kazi? Akina mama wamerogwa na nani hasa?

Huu ushauri ungetolewa kwa mwanaume nina hakika angeupuuzilia mbali. Kwa kuwa akina mama alkili zao zinaishia kwenye urefu wa pua zao, ndio maana wanaweza kushawishika kuacha kazi kwa sababu tu ya kufuata m.b00 ambayo hata ichepuke kiasi gani haiishi.

Je, ingekuwa wewe mwanaJF ndiye umepewa ushauri wa aina hii, ungemsikiliza mama yako au ungetupilia mbali ushauri wake?
DUh mwanaume kuwa mbeya hivi haipendezi aisee , ila una hoja usikilizwe
 
kila mtu ana vipaumbele vyake. Na kwa afya ya familia na ndoa ni vyema wanandoa waishi pamoja
Please compare the cost of losing the job and the benefit of staying together with wife/husband. These are two incomparable entities. Dont compare thresh (marriage) with treasure (employment).
 
Mkuu usitetee jambo la ovyo kama hili. Hebu muonee huruma mwenzako. Sasa hivi anajuta kusikiliza maoni ya mama yake. Anatamani walau apate mtu amuajiri kama dada wa kazi, lakini wapi!
Jamaa anatakiwa atafute mtaji wafanye biashara
 
Mkuu ni wewe ndio umeambiwa uache kazi? Yeye mwenye mume kaona sawa, mama yake mzazi aliyemzaa na kumsomesha CPA kaona sawa wewe ambaye huusiki hata robo eti unakereka. Wewe ndio mwenye matatizo

Baada ya kuacha kazi wamekuja kukuomba hela ya kula?

Tuliza munkari we jamaa. Waache watu na maisha yao na mambo yao. Eti kaacha kazi kafata mbunye, ndio mawazo yako yameenda huko? Kama wewe unachukulia light mambo ya ndoa kuna wenzio wanachukulia serious. Nyie wenyewe kila siku mnasema hakunaga distance relationship sasa mtu akimfata mwenzie pia ni nongwa.

We jomba hebu jali mambo yako itakuzidishia afya
 
Wewe umejuaje yote haya ndugu yangu? Ila Mkuu kuna watu ajira na fedha sio vipaumbele vyao wala tusiwashangae na kuwalaumu.
Huyu ni ndugu yangu wa karibu. Niliposikia kuwa ameacha kazi kwa ushauri wa mamaye na nikitazama maisha anayoishi sasa namsikitikia sana
 
Umaskini na uoga wa maisha ndio unaweza kumfany mtu akashangaa ila n kawaida tu.

On my side nkishakuwa kikaz mkoa mwingine na mpenz yupo kwingne hapo huwa simpi attention yangu kama hapo awali sababu hata kucheatiwa n dk 0 tu huwenda Mama mtu kaliona hilo na hana njaa ya pesa.
 
Hayo ni maoni yako mkuu. Mfano uliotoa hausadifu hiki ninachokisema hapa. Kuacha kazi kisa mb.oo ni uwendawazimu. Cha ajabu huyo mume unayekaa naye bega kwa bega akiamua kuchepuka, lazima atachepuka tu. Kukaa pamoja sio ulinzi sahihi kwa mume kwani mume hulindwa na Mungu, sio mke.



We haujakomaa bado kuweza kudadavua mambo kwa kina.

Unawaza mambo negative kuwa ukiacha Kazi serikalini utakufa au maisha kuwa magumu .

Je haujiulizi kabla ya kupata Kazi serikalini alikuwa anaishi vipi.
 
Kama familia yote inajiweza kwanini asiache kazi na kumfuata mumewe?.

Umasikini ndio chanzo wanawake kuwa watafutaji.
Hii ndio fwact yenyewe....mwanamke ni pambo inabidi atulie nyumbani kidume uchakarike.
Haya mambo ya kuoa mke yupo mwanza mume dodoma ni kudanganyana tuu hapo everybody will cheat its a matter of time tuu
 
Back
Top Bottom