Mama Bonge wa Kariakoo asimama na Rais Samia Uwekezaji wa DP World Bandarini

benzemah

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2014
Posts
1,533
Reaction score
3,187
Mfanyabiashara maarufu wa Kariakoo, Sinyali Kimambo, maarufu kama Mama Bonge amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kutorudi nyuma katika msimamo wake wa kuleta mageuzi ya uchumi nchini, ikiwemo kuvutia uwekezaji wa kampuni ya DP World kwenye bandari ya Dar es Salaam

Mama Bonge, ambaye huagiza vipodozi, vitenge na bidhaa nyingine kutoka nje ya nchi kupitia bandari ya Dar es Salaam, amesisitiza kuwa kampuni ya DP World ni mwekezaji sahihi atakayeongeza ufanisi wa bandari ya Dar es Salaam na kuleta ahueni kwa wafanyabiashara nchini, ambao kwa sasa wanacheleweshewa mizigo yao

Your browser is not able to display this video.
 
Mtu yeyote anayepitisha container bandarini lazima aunge mkono uboreshaji wa bandari, wengi wetu ambao hatutumii bandari directly tunapiga tu kelele nyiiiingiiii!

Wafanye haraka uboreshaji wa huo mkataba mwekezaji aingie tusonge mbele tuachane na wenye mawazo ya kijamaa.

Nilimsikiliza mzee wa TICS karamagi anasema ameacha mkataba akiwa amepandisha capacity ya makontena toka 70k hadi 700k kwa mwaka! Hizi zitakuwa ni containers za kwemda congo tu tukiboresha bandari.
 
Mleta maada ndiyo maana umejichubua kama mama bongo
Huyu si yule mcheza singeli matiti yako nje! Anajuwa nini kuhusu uchumi wa bandari. Yeye mwenyewe kaathiriwa na bidhaa zake mwenyewe kama kweli ni muagizaji wa bidhaa zilizojaa makanikia!
 
Wewe ni la saba na hujui unachoongea.

Kinachokataliwa ni mkataba sio mwekezaji.

Uliacha shule kwa sababu ya kiti moto Kiborloni - moshi
 

Attachments

  • IMG_1599.MP4
    12.5 MB
  • 536F524F-79BB-4A10-AA4E-17D4334619E9.jpeg
    33.2 KB · Views: 6
Ndio hawa idadi ni kubwa
 

Attachments

  • CCD5A05D-6348-4190-A21E-A4A2DC4A63E0.jpeg
    76.6 KB · Views: 5
  • 7E38591C-C512-4773-AA48-F35B06D82481.jpeg
    138.8 KB · Views: 5
Tutusa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu si yule mcheza singeli matiti yako nje! Anajuwa nini kuhusu uchumi wa bandari. Yeye mwenyewe kaathiriwa na bidhaa zake mwenyewe kama kweli ni muagizaji wa bidhaa zilizojaa makanikia!
yule ndio mshika dau mkubwa, we nyau ambaye hujafika hata bandarini ni bora ukae kimya tafuta hela nawe ifike siku moja uagize bidhaa kupitia bandari ya Dar Es Salaam
 
Yuko sahihi wateja mnaona mnanunua tu bidhaa changamoto tunazipata sisi tunategemea kupungua gharama za usafirishaji maaana duuh 1kg n kama 30k+.
 
Unaongea usichokijua nahoji nnayojua zaid ya huyo bonge wenu!!
mfanyabiashara mkubwa anayeitumia bandari mara kwa mara, tukuulize we ni nani umeshafika hata bandarini? Ulishawahi agiza mzigo?
Ana impact gan kwa Taifa mpaka tumuamini kuhusu port investment? Angeongea kitaalam kuhusu mkataba wa DP world na changamoto zake tungemuelewa!!
 
Hamna mtu hataki wawekezaji. Tunachokataa ni mikataba ya kijinga. Huwezi kabidhi mtu bandari jumla jumla lazima pawe na muda specific.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…