Mama Diamond: Mzee Abdul alinikuta nina mimba ya Naseeb (Diamond) na aliikataa. Ricardo Momo na Diamond ni ndugu, baba yao ni Salum Idd Nyange

Je wazazi wanasema nini?

Mama Diamond



Baba Mlezi
 
Halafu tujiulize kuwa undugu wa Queen Doreen na Diamond umetoka wapi? hahahaha yani hawa wote ni machizi tuu.... huyu mzee kinachomponza nikutaka asaidiwe .....lakini hii familia ni wazi ina laana kabisa hahahaha
 
Hapana hii ni well staged, Mama huyu nimemdharau sana kweli jambo kama hili la kwenda Momo kuliongelea studio kama hajaambiwa na huyo Mama na Diomond mwenyewe kwenda kuliongelea.

Hii sio family kwa kweli miaka yote hiyo unakuja kuongea leo. kwanini leo? kipi kipya leo? yule mzee yupo tu na shida zake na una bahati alikupokea una mimba. Kama ningemshauri yule mzee aachane na hawa watu. Huyo diamond mpaka mtoto wake akaampa jina la baba yake leo wanamkana.

Hapa nimeelewa mtu mbaya Mama tena sumu hafai na Mungu analipia hapahapa ndoa hazidumu. Mzee achana na hawa watu rizki anatoa Mungu sio binadamu.

Namuonea huruma sana huyu mzee kwa watu kutumia media zao kumkana mpaka kwa mwanae. Diaomond akikaa kimya katika hili ni walewale.
 
Halafu tujiulize kuwa undugu wa Queen Doreen na Diamond umetoka wapi? hahahaha yani hawa wote ni machizi tuu.... huyu mzee kinachomponza nikutaka asaidiwe .....lakini hii familia ni wazi ina laana kabisa hahahaha
Na ilikuake Diamomd alikua anaenda kumuomba ada ya shule mzee Abdul wakati walikua wanajua sio baba yake. Huyu mama Dangote ni ana sumu kali kuliko nyoka, kapandikiza sumu weee kaona haiui, kaamua kutoka kivingine
 
Na kama ni kweli Mzee Abdul sio baba yake Diamond huenda mama Diamond alikataliwa hii mimba na mzee Salim Nyange akaamua kumtupia zigo mzee Abdul na bila shaka mzee alikubali kiroho safi ila huenda alikuwa anaambiwa mengi na ndugu pamoja na rafiki.
Ngoja tuunganishe dots!

1. Mzee Nyange kampa kitu Bi Sandra,
2. Bi Sandra kaona Mzee Nyange boya tu, hata pesa hana! (NB: Inasemekana Mzee Abdul hapo zamani alikuwa na mkwanja!
3. Mzee Abdul akadondoshewa jumba bovu, akaanza kulea
4. Miaka kadhaa baadae, Wambeya wakamtonya Mzee Abdul kwamba anahudumia mtoto wa mwanaume mwenzake!!
5. Mzee Abdul akaamua kula kona mamoja
6. Diamond akaamini baba ake Mzee Abdul amemtelekeza kumbe baba halisi aliyemtelekeza ni Salim Nyange
7. Bi Sandra nae akaendelea kumwaminisha mtoto Naseeb kwamba huyo aliyemkimbia (Mzee Abdul) ndie babake hasa!!
8. Naseeb akaja kuwa Diamond, na mambo yakaanza kumnyookea
9. Mzee Abdul akaanza kujileta tena kwa Diamond baada ya kuwa amemkacha Naseeb
10. Kwa nongwa tu, huku akitaka mazuri ya Diamond ayafaidi peke yake, hatimae Bi Sandra akaamua kupasua ukweli kwamba kwanza "huyo mzee Abdul mwenyewe sio baba yako mzazi"!
11. Kama ambavyo Bi Sandra alitarajia, Mond nae akaamua kumpotezea Baba wa Kuazima!!!

Je, ina-make sense?! Halafu itakuwa Bi Sandra alikuwa anapenda sana Washkaji wa Kariakoo kwa sababu kuna kila dalili hata Uncle Nyange nae ni mtoto wa Kariakoo!!! Huyo uncle Nyange baba ake atakuwa Mpare mama yake, Mmanyema!!! Au Nyange sio Wapare?
 
Ukweli mchungu
 
Kweli si kila mzee ana akili kuna wezee wengine ni wapumbavu tu. Sasa hapa mbona anajidhalilisha na huyo mtoto wake kisa umaarufu.

Kama Diamond mwenyewe anafurahia huu upumbavu unaomdhalilisha basi ni bora kuwa masikini kuliko kuwa na pesa na mashetani zenye Masharti magumu kiasi hiki.
 
Halafu tujiulize kuwa undugu wa Queen Doreen na Diamond umetoka wapi? hahahaha yani hawa wote ni machizi tuu.... huyu mzee kinachomponza nikutaka asaidiwe .....lakini hii familia ni wazi ina laana kabisa hahahaha
Kwa kweli
 
Na ilikuake Diamomd alikua anaenda kumuomba ada ya shule mzee Abdul wakati walikua wanajua sio baba yake. Huyu mama Dangote ni ana sumu kali kuliko nyoka, kapandikiza sumu weee kaona haiui, kaamua kutoka kivingine
Shida inakuja hapa (IMO); ujauzito haukuwa wa Mzee Abdul, na yeye akaukataa ujauzito huo na akakataa kushiriki kwenye malezi ya Diamond; ni sawa kabisa. Kwa hiyo Bi Sandra alimsingizia mimba mzee Abdul; na hata baada ya mzee kukataa, ilikuwaje diamond akapewa ubini wa Abdul ikiwa Mzee Abdul alimkataa, na huku baba yake mzazi huyo Nyange akiwepo? Na Diamond alikuwa anaenda kwa mzee Abdul kumuomba matumizi kama nani ikiwa si baba yake mzazi wala mlezi? Na undugu wa Queen Darleen na Diamond unatokea wapi ikiwa baba Darleen hakuwahi kujihusisha kimalezi na Diamond?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…