Hivi Wabongo kuna mtu anayefanikiwa halafu tusimhusishe na drugs, freemason au uchawi?! Hivi ni kweli hatuoni hizi hustles zake tangu anaingia kwenye game?! Tusisahau, Diamond ndie msanii wa kwanza kujitambua na kukataa malipo ya hela ya mboga! Sehemu ya habari kutoka
Bongo5 inasema:-
Nakumbuka vizuri chanzo cha hiyo habari ambayo ilikuja baada ya Eric Shigongo kutoa povu kweli kweli kwamba Wasafi hawana utu manake hata kwa shows za TZ, Diamond anataka pesa nyingi mno kiasi kwamba promoters wanashindwa kumlipa na hivyo kuwanyima uhondo mashabiki wake waliomfikisha hapo na badala yale kuelekeza sana nguvu zake na shows za nje!Mbali na hayo, Diamond amepata kuwa balozi kampuni mbali mbali including kampuni kubwa kama Vodacom, Coca Cola, na Pepsi let alone ubalozi wa Luc Belaire, na hapo sijataja publishing deal na Universal SA pesa anazotengeneza kupitia streaming, forget about YouTube!!
Kwanini hatudhani kwamba mafanikio yake yanatokana na hizo deals anazopata na tunataka kuona kilichomfikisha hapo ni upunda?! Tusisahau, duniani kote, sana inalipa kweli kweli na ndio maana hata watu kama akina Oprah na Kanye West wanatokeza kwenye orodha ya richest black billionaires kwa sababu ya sanaa tu!!! Wakina 50Cents, P Didy, Dr. Dre, na wengine wengi; hawa wangine wametoka kwenye familia za kawaida kabisa na wengine kwenye poor families lakini leo ni Dollar Millionaires!!